Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017.

Hon. Dr. Hussein Ali Mwinyi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwahani

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017.

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nichangie hoja na hususani nitajikita katika Kamati ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama. Kwanza niipongeze Kamati kwa kazi nzuri wanayoifanya na niwashukuru kwa ushirikiano wanaotupa mimi pamoja na watendaji wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja zilizotolewa ya kwanza ni kukosekana kwa Sera ya Ulinzi wa Taifa nchini na kuna athiri ufanisi katika utendaji. Tunakiri mpaka sasa hivi sera hiyo haijapatikana lakini nataka niseme kwamba sera hiyo tayari rasimu yake ipo imekwama katika jambo moja dogo nalo ni maoni ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi karibuni nilipata nafasi ya kuzungumza na Waziri mhusika kule Zanzibar akaniambia kwamba tayari wanajipanga kwenda kuijadili katika Baraza la Mapinduzi ili hatimaye waweze kutufikishia maoni yao na baada hapo itafuata utaratibu uliobaki ili tuwe tuna sera ya ulinzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nimshukuru Mheshimiwa Angelina Mabula kwa kulijibu lile suala la beacons za mipakani kama mlivyosikia kazi imeanza kufanywa na vilevile nimpongeze Mheshimiwa Kandege kwa kujibu hoja za barabara za mipakani jambo hilo litashughulikiwa na TAMISEMI na tuna imani kwamba barabara hizo zitapitika ili ulinzi uweze kufanyika vizuri zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu madeni ya Shirika la SUMA JKT, ni kweli kuna madeni mengi kuna madeni ya matreka, kuna madeni ya huduma zinazotolewa na SUMA Guard ya ulinzi kuna madeni ya mbegu zinazozalishwa na SUMA na kuuzwa katika taasisi mbalimbali. Lakini hatua zimeanza kuchukuliwa za kukusanya madeni hayo tulikuwa tunawa andikia barua lakini sasa hivi tume-engage kampuni za ukusanyaji wa madeni ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa na fedha hizo zipatikane ili SUMA ijiendeshe vizuri zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu wananchi kutolipwa fidia katika maeneo yaliyotwaliwa wanajeshi na migogoro ya ardhi kwa ujumla, nataka hapa niseme Waheshimiwa Wabunge ipo dhana kwamba Jeshi lina maeneo makubwa ambayo hayatumiki. Nataka nisemie hivi kwamba jeshi lina maeneo makubwa kweli lakini yalichukuliwa kwa sababu maalum. Yako maeneo ya Jeshi kambi za Jeshi ambazo kazi zake ni utawala na logistic, lakini kuna kambi za mapigano, kuna vifaa vya milipuko, kuna kambi za mapigano, kuna vifaa vya milipuko, kuna kufanya mazoezi ni lazima wawe na maeneo makubwa.

Kwa hiyo, ninachosema hapa ni kwamba watu wasidhani kwamba kuna mapori wakadhani hayahitajiki wakavamia hiyo sio sahihi kwa sababu pale wanafanya mazoezi. Kambi zote lazima zifanye mazoezi, kwa maana hiyo ni kwamba maeneo makubwa yanahitajika jeshini na wananchi waelewe hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kwa wale wananchi waliovamia tungewataka na pamoja na nyinyi Waheshimiwa Wabunge niwaombe kwamba isiwe kawaida ya Wabunge kutetea upande wa wananchi peke yake, kwanza tuangalie tuhakikishe kwamba wananchi wana haki. Yako maeneo mengi wananchi ndio wamevamia maeneo ya jeshi, na ninyi mnatambua, kila kwenye Kambi ya Jeshi kwa sababu kuna huduma kuna afya pale, kuna shule pale, kuna maji pale wananchi wanakuwa haraka kuja karibu na wengine huwa wanalima katika maeneo yale. Kwa hiyo, tunaomba kwa sasa tuhakikishe kwamba wale wananchi ambao hawana haki ya kuwa katika maeneo hayo waondolewe na ndugu zangu mtusaidie.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kwa wale wanaodai fidia, kweli kuna maeneo ambayo Jeshi limetwaa tutahakikisha kwamba wanalipwa na haki zao watazipata na kwa kadri ya uwezo wa kifedha tutaendelea kulishughulikia suala hili ili wananchi wale waweze kupata haki zao.