Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017

Hon. Joyce Bitta Sokombi

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017

MHE. JOYCE B. SOKOMBI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kupata nafasi hii nami nichangie kwa maandishi kuondolewa kwa vitabu vibovu mashuleni.Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge lililopita wachangiaji walisisitiza juu ya ubovu au kutokuwa na usahihi wa vitabu vya kufundishia mashuleni hivyo iliamuliwa viondolewe mashuleni, lakini cha kushangaza vitabu vile bado vipo mashuleni na kusababisha kufifia (kufifisha) kwa elimu yetu hapa nchini. Kwa hiyo, naishauri Serikali ihakikishe inaviondoa vitabu hivyo mashuleni haraka sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo cha Mloganzila; Chuo cha kujifunzia na kufundishia Madaktari Bingwa Mloganzila kimejengwa (kilijengwa) kwa madhumuni ya kufundishia Madaktari kwa mujibu wa kanuni za Madaktari ulimwenguni ya kwamba kila Hospitali Kuu ni lazima iwe na Chuo Kikuu cha kufundishia na kujifunzia Madaktari. Mimi naishauri Serikali kwamba chuo hiki kibaki kuwa chuo cha kufundishia na kujifunza na siyo kuwa Hospitali kama inavyotaka kufanywa sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ubora wa elimu; kumekuwa na changamoto kubwa sana ya ubora wa elimu hasa kwa shule za Serikali na hii inatokana na Serikali yenyewe kutotilia mkazo maslahi na motisha kwa Walimu na uhaba wa vifaa vya kufundishia mashuleni pamoja na umbali wa makazi na umbali wa shule.


Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo shule binafsi zimeboresha na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi, lakini nashangaa na inasikitisha sana kwa Serikali kutoa matamko ya kuzuia kukaririsha wanafunzi na kusababisha mrundikano wa wanafunzi wanaofeli mashuleni. Ushauri wangu Serikali iachane na kuzuia kukaririsha kwa shule binafsi ili waweze kuwajengea uwezo wale wanaoweza kufanya vizuri badala yake waboreshe shule za Serikali ili ziweze kutoa wanafunzi walio bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali iache kutoa adhabu kwa Walimu ambao shule zao zimefelisha badala yake Serikali ifanye utafiti ili kujua kwa nini wanafunzi wanafeli ndio itoe adhabu na siyo kutoa adhabu bila kufanya utafiti.