Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchukua fursa hii kukushukuru wewe kwa kunipatia nafasi hii ya kutoa mchango wangu kwa kuchangia Taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli za Kamati za Kudumu za Kilimo, Mifugo na Maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuwapongeza Wajumbe wa Kamati wote kwa kuandika na kuichambua na kuiwasilisha kwa umakini mkubwa katika Bunge lako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuchangia taarifa hii, napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Benki ya Maendeleo ya Kilimo ni miongoni mwa vitu ambavyo ni tegemeo kubwa kwa wakulima hasa wakulima wa kipato cha chini. Hivyo naungana na ushauri wa Kamati juu ya Serikali kuipatia benki hii uwezo wa kila aina ili iweze kuwavusha wakulima katika azma zao za kilimo chenye faida. Aidha, kwa kuwa Serikali yetu inaelekea kwenye uchumi wa viwanda, lazima tujue kwamba msingi mkubwa wa kuendesha uchumi wa viwanda ni kilimo chenye manufaa. Hivyo, kuiwezesha Benki hii kutupeleka huko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sekta ya Uvuvi ni moja katika sekta muhimu katika nchi yetu na ulimwenguni kwa jumla. Sehemu kubwa ya wananchi wetu ni wavuvi, lakini bado wavuvi wa kipato cha chini hawajaweza kutimiziwa haja zao na Serikali kwa kuwapatia nyenzo za uvuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu katika Sekta hii ya Uvuvi ni kwamba Serikali iwapatie zana za uvuvi kama vile mashine na mitego ya kisasa ili waweze nao kuepukana na kuvua kizamani. Aidha, Serikali iendelee kuwaelimisha wavuvi hawa namna bora ya uvuvi ili kuepuka kuvua kwa mazoea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.