Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nachukua fursa hii kukushukuru wewe kwa kunipa nafasi ya kuchangia katika taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, napenda kuipongeza Kamati kwa kuandika kwa umakini na kuiwasilisha taarifa hii kwa ubora na kwa kufahamika vizuri na Wabunge wote. Katika kuchangia taarifa hii napenda kutoa mchango wangu katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, migogoro ya ardhi; Serikali imezoea kupima na kuelekeza matumizi ya ardhi katika shughuli za ujenzi, mashamba na mipango miji, lakini kuna tatizo kubwa ambalo linasumbua na kuleta athari kubwa katika maeneo kadhaa ya nchi yetu; tatizo hilo ni tatizo la maeneo ya wakulima na wafugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu katika suala hili, Serikali ianze mpango maalum wa upimaji wa maeneo hayo na kuyaelekeza kwa jamii hizi mbili za wakulima na wafugaji. Hii itaondosha usumbufu mkubwa kwa watu hao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume ya Matumizi ya Ardhi, Kamati katika taarifa yake ukurasa wa 23 imeshauri kuhusishwa kwa kampuni binafsi ya upimaji na upangaji wa matumizi ya ardhi. Mimi binafsi sikubaliani na ushauri huu kwa sababu zifuatazo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapotumia kampuni binafsi katika kazi hii tunaongeza gharama za uendeshaji (operation coast) ambazo mwisho wake zinaenda kwa mtumiaji wa ardhi ambaye ni mwananchi wa nchi hii. Ushauri wangu katika suala hili ni Serikali kuwatumia vijana wetu
kwa kuwapa mafunzo ya kazi hii na mwisho wake kuwapatia ajira. Hii itakuwa ni moja ya vyanzo vya kuongeza ajira katika nchi (source of job creation).

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.