Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.

Hon. Dr. Immaculate Sware Semesi

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi. Nina mambo saba ambayo nataka nigusie na nitajielekeza katika taarifa iliyotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi pamoja na Maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nigusie kwanza suala la NFRA. Kumekuwa na sintofahamu mwaka wa fedha 2016/2017 kuhusu njaa, kukatokea statements mikanganyiko kuhusu kuna njaa au hakuna njaa nchini. Hii ilijitokeza kwa sababu baadhi ya mikoa ilizalisha vizuri na mikoa mingi zaidi nchini kwetu ilikuwa kwenye hali ya ukame na kutokuwa na chakula. Nchini kwetu tumejiwekea tu mfumo mzuri wa kuwa na NFRA ambayo basically inatakiwa i-regulate mifumuko ya bei ya vyakula kwa kuhifadhi na kutoa vyakula hivi masokoni ili ku-balance bei ya chakula na kuhakikisha kwamba kuna chakula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kusikitisha ni kwamba budget allocation ambayo inatakiwa iende specifically kwa ajili ya NFRA ina utata, fedha hazitolewi kwa wakati na ni kidogo kwa hiyo mazao yanayonunuliwa ni machache na hayaendani sawasawa na msimu. Kwa hiyo, pesa zinapatikana nje ya msimu na kuathri mzungunguko mzima wa stock na mazao kwa ujumla wake. Naona tunaelekea kwenye dalili hizohizo kwa 2017/2018, kwa hiyo naomba Wizara iangalie tena hili kwa upya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ambalo nataka niligusie ni kuhusu taasisi zetu za tafiti ambazo ziko chini ya Wizara ya Kilimo ambazo pia zipo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Huwezi kufanya mabadiliko yoyote au decision yoyote bila kuwa na scientific back up ya information au kuwa na data mahsusi. Cha kushangaza tunapopitisha bajeti humu ndani, hizi taasisi mahsusi za kufanya utafiti kwa ajili ya fertilizers au mbegu kadhaa au kwa ajili viuadudu kadhaa, haipangiwi hata senti tano. Inashangaza tunasema kwamba Tanzania inategemea kilimo, majority ya wananchi wetu ni wakulima, huu uti wa mgongo mbona hatuuwezeshi kwa kuziwezesha hizi taasisi zetu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano tu, tuna shida, nafikiri juzi tumeona Waheshimiwa Wabunge Ulanga imeingiliwa na panya, wanavamia mipunga, Serikali iliwahamasisha wakulima wa pamba wakalima sana wakaingiliwa na wadudu (viwavijeshi) na kadhalika. Kwanza hatuna hata bajeti ya kuweza ku-handle, mfano kwenye issue ya pamba Serikali imetoa bilioni tatu tu ili kuweza ku-save mazao hayo kati ya bilioni 39. Kuna Mfuko wa Waziri Mkuu hapa kuhusu maafa hakuna kitu, Wizara iliombwa iweze ku-shuffle kidogo bajeti yake, Hazina haijatoa hata senti tano kwa ajili ya ku- deal na hao wadudu wanaovamia mazao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, NFRA ina hela tata, TPRI kwa mfano au taasisi nyingine za shughuli za tafiti hakuna hela, yametokea majanga hakuna hela. Sasa tunaongelea matumbo yetu kuhusu chakula na pia tunaongelea mazao ya biashara, hii nchi inasimamaje na wakati uti wa mgongo hatuuwezeshi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la tatu ambalo nataka niligusie kwa juu juuu pia ni bei elekezi na soko la bidhaa za mazao yetu. Tumeweza kulima mazao ya chakula, tumeweza kulima kidogo kwa kuchechemea mazao ya biashara. Serikali inaji-commit wakulima walime mazao fulani, mfano dhahiri ni mwaka jana na mwaka huu bado tuna-suffer na wakulima wetu wa mbaazi, soko halieleweki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana tulihangaika huku kuhusu mazao ya mahindi, tukatokea na sintofahamu Kambi ya Upinzani ilishauri ruhusuni hata kutoa mazao hayo, NFRA inunue na kutoa mazao bei iwe elekezi ambayo ni nzuri kwa wahitaji, tuuze mazao yetu, mahindi yetu nje ya nchi. Decision imekuja kuongelewa hapa tukabezwa upande wa Upinzani lakini baadaye mlikuja kusema go ahead, lakini it is too late. Kwa hiyo, kuna umuhimu wa kuweka mikakati madhubuti ya mifumo ya masoko yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nigusie kuhusu uvuvi haramu na njia zinazotumiwa na Wizara husika kuudhibiti. Kwa mfano, mwezi huu uliopita, Wizara yangu hii ya Mifugo na Uvuvi ilijikita Mwanza ilikuwa Ukerewe, ikisema inadhibiti uvuvi haramu. Sasa unajiuliza ni kudhibiti au ni kumkandamiza huyu mvuvi? Ni ipi njia sahihi ya kumdhibiti huyu anayeitwa mvuvi haramu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona kwenye taarifa ya habari kwamba Katibu Mkuu wetu wa Uvuvi ameteketeza nyavu haramu za shilingi bilioni 2.6 Mwanza kwa ujumla wake. Unajiuliza hizi nyavu za gharama hii zimeingiaje nchini? Miaka nenda rudi tunasema tunachoma moto tonnes and tonnes za hizi nyavu lakini unajiuliza kwamba unadhibiti vya kwenye maji, vya kwenye ardhi je? Kwa sababu ukiangalia hata hiyo mode mnayoteketeza mnaharibu pia mazingira. Kwa hiyo, kwanza mnaharibu mifuko ya wale walionunua hizo nyavu, mnaharibu uchumi wa wale wavuvi wahusika kwa sababu hamwendi tu kuharibu nyavu bali hata zile sehemu zao za kuvulia, camps zao mnachoma moto, vifaa vyao vya kuvulia kama maboti mnachoma moto, kulikoni? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, badala ya ku-solve issue permanently mnakuwa mnagusiagusia na kuweka gharama kubwa na kutia watu hasara na kuharibu mazingira mengine kwa kuchoma yale manailoni in open space. Kuna vikundi vya BMU, je, mmevihamasisha, mmeviwezesha kuweza kujikidhi kwa sababu vipo specifically kwa ajili ya ku-regulate uvuvi haramu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tano ambalo naomba nigusie ni kuhusu Benki ya Maendeleo ya Kilomo (TADB). Benki hii ilianzishwa nafikiri 2015 na ikapewa mtaji wa 60 billion na mpaka tunaongea sasa hivi benki hii haijawezeshwa, imeokoteza hapa na pale sasa hivi ina only 66 billion kama mtaji kati ya bilioni 800 ambayo inatakiwa iwe nayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaongelea maendeleo ya kilimo, yanatoka wapi? Hii benki iliwekwa mahususi kwa ajili ya kuendeleza kilimo… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)