Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 na Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017.

Hon. Marwa Ryoba Chacha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Serengeti

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 na Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017.

HE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru sana. Naomba niseme machache kuhusu Kamati hii ya Miundombinu na hii ya Nishati.

Mheshimiwa Naibu Spika, huwa naona kuna Wabunge wamejiuzulu Ubunge wao na Madiwani eti wanamuunga mkono Magufuli kwamba amefanya mambo mazuri sana katika nchi hii. Huwa nakaa najiuliza mpaka leo sijapata majibu, kwamba Magufuli amefanya mambo makubwa kwelikweli. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikachukulia sample ya Mkoa wangu wa Mara mpaka leo haujaunganishwa na barabara ya lami na Arusha ambayo Muasisi wake ni Nyerere mwenyewe. Nyerere akafa akawaachia wengine kuongoza nchi hii mpaka leo na Magufuli amekuwa na historia ya kuwa Waziri wa Wizara hiyo kwa muda mrefu sana. Mwaka 2013 wameanza kutengeneza barabara ya kuunganisha Mkoa wa Mara na Mkoa wa Arusha wakaanza na kilometa 50. Imepita miaka sita kilomita 50 hazijakwisha hata kilometa sita tu wameshindwa kumaliza. Hiyo ndiyo Serikali ya CCM, nijiuzulu leo nimuunge mkono wakati barabara imemshinda. (Makofi/ Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2016/2017 ikatengwa shilingi bilioni 20 kwenye barabara hiyo, upande wa Mara bilioni 12 upande wa Arusha bilioni nane. Upande wa Arusha wakatangaza tenda wameshaanza kulima. Upande wa Mara bilioni 12 kipande cha Mugumu - Nata mpaka sasa hivi wanaendelea kutangaza tenda, bajeti ya 2016/2017. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi Ryoba niko tayari kujiuzulu kuwaunga mkono, lakini mbona sioni sababu ya kuwaunga? Nipeni sababu ya mimi kujiuzulu kuwaunga kama barabara ndogo tu ya kuunganisha Mkoa wa Mara na Arusha imewashinda. Kwa hiyo, bado, bado sana. Kwa hiyo, niwaambie wananchi wa Mkoa wa Mara adui yao ni CCM na Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi leo mkoa ambao ametoka Muasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hata Uwanja wa Ndege hakuna. Hakuna uwanja wa ndege wa maana Mkoa wa Mara. Nani leo, Waziri gani, Mbunge gani wa CCM asimame hapa aniambie Mkoa wa Mara haustahili kuwa na Uwanja wa Ndege tena wenye hadhi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2016/2017 ilitengwa bilioni mbili kwenye Uwanja wa Chato, baadaye nikasikia bilioni 39.15 zimetokea wapi mbona hatujawahi kuziona kwenye bajeti mniambie! Kama kweli mnampenda Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, unachukua bilioni 39 unapeleka Chato kuna nini? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, samahani Mheshimiwa Waziri wewe ni rafiki yangu lakini naongea mambo ya kitaifa kidogo inauma. Pale ambapo anatokea Muasisi wa Taifa hata uwanja wa ndege na barabara hakuna. Leo Mkoa wa Mara kwa mfano hakuna Jimbo hata moja ambapo wanakunywa maji safi na salama, hakuna! Asimame yeyote hapa aniambie Mkoa wa Mara kuna Jimbo lenye chujio, wapi? Tarime wanakunywa matope, Musoma Mjini wanakunywa jinsi yalivyo, wanaugua amoeba na minyoo hivyo hivyo, sasa ninyi niwaunge kwa lipi, si mnisaidie? (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, unajua nilikuwa napita kwenye hiki kitabu cha Kamati ya Miundombinu, ninyi Wajumbe wa Kamati mniambie, nimesikia mmeitisha mpewe taarifa ya Uwanja wa Chato, Waziri amegoma kuwaletea na umetumia bilioni 39! Kwenye kitabu humu naangalia naona viwanja vingine, hivi uwanja wa Chato unajengwa au haujengwi na kama unajengwa kwa nini haumo humu? Wajumbe wa Kamati nataka majibu, kwa nini hauko humu? Wabunge nataka majibu kwa nini hauko humu? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, halafu mkandarasi anayejenga huo uwanja unajua ni nani? Ni yule ambaye ameshindwa kumaliza zile kilometa 50 pale Mkoa wa Mara, ndiyo amepewa Mayanga nani mwingine si ndiyo huyo? Kisa rafiki yake na nani, Magufuli, ooh haya, twende kazi.

M W O N G Z O . . .

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Msigwa naomba ukae. Mheshimiwa Ryoba naomba ufute hayo maneno halafu uendelee na mchango wako.

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nifute.