Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Hon. Saada Salum Mkuya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Welezo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na mimi namshukuru Mwenyezi Mungu katika Ijumaa hii ya leo kupata nafasi hii adhimu ya kuchangia Mpango huu wa Maendeleo ya Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nachukua fursa hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na wasaidizi wake wote kutokana na kasi ya utendaji na utekelezaji wa mipango yetu ya maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza kuchangia Mpango, Mheshimiwa Turky aligusia kidogo tittle ya kitabu hiki ni Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa mwaka 2018/2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani Taifa hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaundwa na pande mbili. Cha kusikitisha na cha fadhaa kabisa ni kuona hakuna hata eneo moja lililopangiwa mpango angalau tu ikaelekezwa katika upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano na hili nataka niliseme wazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia kwako, Mheshimiwa Waziri wa Fedha wakati tunajadili bajeti mwezi Juni, 2017 baadhi ya wenzangu tunaotoka katika upande wa pili wa Jamhuri tulichangia maeneo fulani fulani, lakini kwa masikitiko makubwa hakuna hata eneo moja lililoguswa likajibiwa hoja angalau kule upande wa pili wakasikia. Mimi nilichukua hatua ya kwenda kumuuliza Mheshimiwa Waziri wa Fedha mbona hujajibu angalau basi hoja mbili ili wananchi wa upande mwingine wa Muungano waone kwamba na wao they are part and parcel ya Jamhuri ya Muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa Fedha aliniambia muda mchache na majibu yalikuwa mengi. Nilijisikia vibaya kwa sababu kama una responsibility ya pande mbili za Jamhuri maana yake angalau ungechukua hoja mbili ukazijibu. Sasa aliniambia kabisa kwamba muda mchache, hoja zilikuwa nyingi kwa hivyo mimi nitakupa document usome, this is exactly jambo ambalo ameniambia nimesikitika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunachangia hapa na nimeona tendency ya Wabunge ambao wanatoka upande mwingine wanachangia. Tuombeni Mungu angalau hoja mbili, tatu zijibiwe muda uwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukienda katika Mpango kuna jambo lingine kabisa la kusikitisha, kwenye eneo la utalii, biashara na masoko, hivi kwa namna gani au kwa namna yoyote unapotaka ku-promote utalii unaiachaje Zanzibar? Yaani hakuna na haielezeki! Utakuwaje na mpango wa ku- promote utalii Tanzania bila kuiingiza Zanzibar, haiwezekani! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, majibu yanaweza yakawa very simple ukisema habari ya Zanzibar majibu yanakuwa very simple kwamba hilo siyo jambo la Muungano. Hivi jamani kama kutakuwa kuna Wizara tatu za Muungano kwa nini sisi Wabunge tusiwe watatu tu humu ndani kutoka Zanzibar? Kwa nini tuko 53? Kuna masuala mengine hayahitaji lazima iwe ni Wizara inayoshughulika na Muungano. Kuna issues nyingine zinahitaji coordination za pande mbili. Kama hii issue ya utalii, hivi kweli kutakuwa na programu au project yoyote bila kui-include Zanzibar? Is not possible, haipo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine kwenye elimu ya juu, hii imo kwenye jambo la Muungano, there is nothing, Waheshimiwa hakuna jambo lolote ambalo limeguswa. Sasa sijui huu Mpango wa Taifa lipi hatujui.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna eneo lingine kwenye masuala ya habari, utamaduni, sanaa, ustaarabu, burudani na michezo. Sasa hivi tumeona Tanzania inaingia katika ramani ya michezo, lakini hakuna specific plan ambayo itaweza ku-accommodate angalau kujenga uwezo wa wachezaji wa michezo mbalimbali katika kuitangaza Tanzania, hakuna. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hii sanaa ya uigizaji, hawa waigizaji wameachwa kabisa. Toka juzi tunasikia wao wenyewe wamekwenda Kariakoo, sijui wanapambana na wale piracy na kadhalika, lakini sisi kama Serikali hakuna mpango wowote wa kuwasaidia wasanii wa Tanzania. Leo GDP ya Nigeria imekuwa rebased kutokana na contribution ya sanaa katika uchumi wao. Sisi tumefanya rebase kwa ajili ya kuingiza sectors mpya ikiwemo hii ya sanaa lakini hakuna mpango wa kuendeleza sanaa hii. Kwa hiyo, katika Mpango wetu wa Maendeleo naona hilo limeachwa kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna masuala ya ushirikiano wa kimataifa, inasikitisha na inashangaza kuona katika eneo muhimu la diaspora limeachwa. Diaspora Ethiopia wameungana pamoja wanajenga hospitali kubwa kabisa ambayo ownership ni karibu asilimia 90 ya Waethiopia wanaoishi nchi za nje, sisi kwetu hakuna jambo lolote ambalo angalau tumeweka consideration ya kuangalia mobilization ya resources kutokana na diaspora, hakuna! Vile vyanzo vyetu vya mapato ni vilevile tokea Taifa hili lilipozaliwa.

Mheshimiwa Dkt. Mpango wewe ni mweledi tumeshakuwepo sana katika semina na vikao vya resource mobilization lazima tuangalie njia mpya ya kuweza ku-tap resources zilizopo ili kuelekeza katika Mpango wetu wa Maendeleo. Kuna role ya diaspora iko wapi, wenzetu wanai- issue diaspora bond na katika article moja ya World Bank, Tanzania imo kabisa katika nchi ambazo zina potential kubwa ya kuweza ku-mobilize diaspora bond. Hebu liangalie hili tutapata pesa nyingi. Watanzania wenzetu wapo kule lakini hawaoni kama Serikali ina nia ya kuweza kuwasogeza karibu ili na wao wakasaidia kuchangia maendeleo pamoja na uchumi wa nchi yao kama ambavyo wanafanya wenzetu wa Nigeria, Ethiopia na Uganda. Naomba eneo hili tuliangalie kwa mapana yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika ujenzi wa Tanzania ya Viwanda, sera ambazo zinakuwa employed na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zina effect hata kule Zanzibar. Tumeona na tunasifu kazi nzuri sana ya Serikali kwenye list ya viwanda ambavyo vinaendelea kujengwa na ambavyo vimeshajengwa. Waheshimiwa, the list is long lakini hakuna hata sehemu moja tukasema angalau tutashirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ku-tap investors ambao wataweza kujenga kiwanda kitakachotumia malighafi ya karafuu, hiyo consideration hakuna, inasikitisha! Sasa Mpango huu wa Taifa, Taifa lipi bila ya Zanzibar, inasikitisha! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini juu ya hivyo, nimesahau jambo moja, nimepata kuulizia hivi jamani Mheshimiwa Waziri wa Fedha anashughulika na pande mbili za Muungano, at any point of time tokea ameteuliwa kuwepo pale ofisini alipata kwenda Zanzibar katika kikao cha kazi, siyo kikao cha kero za Muungano, kikao cha kazi? Nikaambiwa hajafika. Nadhani ni jambo ambalo linasikitisha. Nimeambiwa umekwenda katika vikao vya kero za Muungano, tunashukuru sana kwa sababu ku-participate ni katika hatua ya kutatua kero za Muungano, lakini kikao tu cha kuona kwamba kuna mashirikiano baina hizi Wizara mbili, ya Fedha ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibar nimeambiwa hatujamuona Mheshimiwa Waziri. Tunakuomba Mheshimiwa Waziri katika sehemu zako za kazi ni pamoja na Zanzibar uwe unafika angalau usikie. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna eneo moja ambalo tulipata faraja kusikia around two weeks ago kwamba Makamu wa Rais amezindua Sera ya Microfinance, lakini kwenye Mpango na katika maeneo ya vipaumbele kwa mwaka 2018/2019 hakuna sehemu ambapo kuna mkakati maalum wa kuweza kusaidia hizi microfinance institutions zikiwemo SACCOs pamoja na VICOBA. Hizi institutions zinasaidia sana hususani akina mama ambao wako vijijini lakini lazima wawe katika aidha policy framework au legal framework ili na wao waweze ku-access mikopo kutoka katika banks. Sasa haijawekewa kitu chochote katika Mpango huu wa maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu Mheshimiwa Waziri kama nafasi itakuruhusu utakapokuwa unajibu hoja, naomba ujibu pamoja na hili ili wananchi wakusikie hususani wanawake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo lingine kwenye promotion za utalii kule Zanzibar kuna vivutio, tunajaribu kuweka mambo mbalimbali pamoja na wakati wa low season watalii hawaendi lakini sisi tunajaribu kuweka matukio ili tupate ku-tap. Tuna Zanzibar International Film Festival (ZIFF) pamoja na Sauti za Busara, ni vitu ambavyo angalau basi vingekuwa taped katika haya masuala ya mipango ili kuona kwamba utalii umo katika Mpango wa Taifa kusaidia Zanzibar pamoja na Tanzania lakini imekuwa ni competition. Sasa hivi nimesikia kumeanzishwa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)