Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Hon. Khatib Said Haji

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Konde

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

MHE. KHATIB S. HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia name kusimama hapa mchana wa leo siku tukufu ya Ijumaa ili name niweze kusema machache.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nianze kuwapongza kwanza Waheshimiwa Wabunge wenzetu wote walionekana na Mheshimiwa Rais wanafaa kuwa Mawaziri na wamepata uteuzi ule, nawapongeza sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipekee napenda nimpongeze kwa dhati kabisa Mheshimiwa Mbunge mwenzetu Lazaro Nyalandu kwa uamuzi wake mtukufu kabisa wa kuamua kuhama Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza kwa dhati na niwaombe wenzetu pale wenzetu wanapofanya maamuzi wa huku kuja huko au wa huko kuja huku isichukuliwe ni uadui tunabadilishana tu kila jambo na wakati wake, msianze kuwapa majina mabaya mukasema wanarembua macho, ni mafisadi hakuna.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna orodha ya wote mnaowadhania huku hawafai kuweko huko hawa hawatafaa kuweko huku, kwa hivyo mnabidi muwaeleze mapema kama ninyi hana sifa kuwepo. Msingoje akitoka huko akija huku ndio mnaanza kufichua mabaya yake kichokuwa shinda kukila msikitie hila. Ahsanteni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye Mpango, kwa mara ya kwanza baada ya Mheshimiwa Spika juzi kuwataka Wabunge wafunguke kuishauri Serikali kuhusiana na Mpango huu nimefurahi kuona kwamba hakukuwa na utofauti bali walikuwa ni Wabunge wote wa Bunge hili kutoa mawazo ya kuionesha Serikali pale inapokosea na inapotakiwa kujirekebisha. Kwa dhati kabisa niwapongeze Mheshimiwa Bashe, Mheshimiwa Serukamba, Mheshimiwa Msigwa, Mheshimiwa Sugu na wenzao wote ambao haionekani tofauti ya kiitikadi ya kivyama bali wote tunalenga katika kuilekeza Serikali maana na uhalisia wapi tunataka kwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika yote kwa dhati, nimwambie Mheshimiwa Mpango, katika mambo yaliyotusikitisha hapa wengine ni pale Wajumbe wa Kamati ya Bajeti wanaposimama hapa na wakasema kwamba unakaidi kupokea mashauri na maelekezo yao. Sasa kama Kamati ndiyo wawakilishi wa Bunge zima katika sekta wanayoisimamia kwa hivyo unapoanza kuidharau Kamati katika mashauri wanayokupa maana yake ni kwamba hata sisi humu utatupuuza lakini na sisi tunatimiza wajibu wa kusema yale tunayoona yanafaa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo dhamira ya Rais wetu na mpango mkuu wa kufufua viwanda hatuoni mafanikio yanayopatikana kama wenzetu walivyosema kwamba kuiachia Serikali kila kitu itekeleze kwa pesa yake hilo jambo haliwezekani. Hayo ni mashauri ya kutaka private sector iingie katika kuendesha biashara ili tukwamuke. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikupe mfano mdogo, leo ni mwaka wa 10 Mheshimiwa Mpango tumekuwa tukiimba nyimbo ya kukifufua Kiwanda cha General Tyre cha Arusha lakini hebu niambie leo tumefikia wapi?

Mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Viwanda na Biashara, tumefanya ziara mara kadhaa, tumependekeza mara kadhaa, kama kuna umuhimu wa viwanda vya sukari pia katika kiwanda muhimu katika nchi ni kiwanda cha matairi.

Leo hebu niambieni ni Mbunge gani anayefika hapa bila kutumia gari? Gari linakwendaje bila tairi? Mahitaji ya tairi ni makubwa sana. Kama tunashindwa kufufua kiwanda muhimu kama kile ambacho ukiangalia kwa umakini soko la matairi yatakayozalishwa pale ukienda kwenye Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma pekee hawawezi kulibeba soko la matairi yatakayozalishwa pale General Tyre, tunataka nini?

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)