Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

Hon. Susanne Peter Maselle

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

MHE. SUSANNE P. MASELLE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuweza kuchangia katika Wizara hii. Kabla sijaanza kuchangia napenda kutoa pole kwa wananchi wa Mwanza kwa tetemeko ambalo limetokea jana na pia nitoe pole nyingi kwa askari wetu Joyce ambaye alifariki kwa kupata mshituko na majeruhi wengine ambao wamepelekwa hospitali, natoa pole sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri ulikuja Mwanza najua ulifanya mambo mazuri sana kama alivyoongea Mbunge wa Nyamagana, lakini kuna migogoro ambayo hukuipitia, kuna migogoro ambayo iko Ilemela. mwaka 2009 Jeshi la Wananchi lilifanya utambuzi wa maeneo yake na iligundulika eneo la Mlima wa Nyagungulu Kata ya Ilemela ilikuwa inafaa kwa makazi ya Jeshi. Sasa utambuzi huu baada ya kufanyika ilionekana kuna kaya 448 ambazo zilikuwa na makazi ya kudumu na tarehe 04 Novemba, 2014 ilifanyika tathmini ambapo Serikali ya Mkoa pamoja na Jeshi la Wananchi waliona kwamba wananchi hao wanapaswa kulipwa, na waliamua kwamba baada ya tathmini hiyo walisema kwamba ndani ya miezi sita wananchi hao wangekuwa wameshalipwa, lakini mpaka sasa bado hawajalipwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna nyumba zingine ambazo ni za udogo mpaka zimeanza kuanguka hawawezi kufanya marekebisho yoyote au kuzikarabati kwa sababu wanaogopa eneo hilo linachukuliwa na Jeshi. Sasa Mheshimiwa Waziri ninaomba umalize huu mgogoro kwa sababu hawa wananchi wanateseka na wananchi wengi wamekuwa wakilalamika, wameandika barua nyingi sana. Wameandika barua kwa Mkuu wa Mkoa, barua hizi hapa nitakuletea, wameandika kwa Mbungeā€¦

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)