Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa shukrani zangu za dhati kwako kwa kunipatia fursa hii ya kuchangia katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Napenda kumpongeza Waziri, Naibu Waziri, pamoja na watendaji wao wote wa Wizara hii kwa kutayarisha hotuba hii kwa ufanisi na kuweza kuwakilisha kwa umakini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuchangia hotuba hii, napenda kugusia maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo cha Diplomasia ni chuo chenye walimu hodari katika Idara zake zote. Ni walimu wanaofanya kazi kwa bidii na kizalendo. Napenda kuchukua nafasi hii kupongeza walimu hao na kuwataka waendelee na juhudi hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miundombinu ya chuo hicho hayaendani na jina la kidiplomasia. Miundombinu ni mibovu kidogo, hivyo naiomba Wizara iboreshe miundombinu hii ili chuo kiwe bora zaidi Kitaifa na Kimataifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni kuhusu Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha. Neno Kimataifa ni neno lenye hadhi. Unaposema Kituo cha Kimataifa ni lazima uwe katika nafasi fulani ambayo ni kubwa ulimwenguni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha Mikutano cha Arusha bado kinahitaji marekebisho ili nacho kiwe cha Kimataifa. Serikali inajitahidi kuanzisha miradi ambapo ni jambo zuri sana, lakini bado jengo haliko safi upande wa vyoo; hakuna vyoo vya watu mashuhuri (VIP), vyoo vilivyopo ni kama vya shule za primary/secondary. Hivyo naomba Wizara nayo irekebishe suala hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni kuhusu uvumi wa udhalilishaji wa Watanzania katika nchi za Kiarabu. Kumekuwa na uvumi usiokuwa na uhakika katika mitandao na vyombo vya habari zinazoeleza juu ya uteswaji wa Watanzania huko Arabuni. Hili ni jambo linalotia wasiwasi sana katika jamii ya Watanzania. Hivyo namuomba Mheshimiwa Waziri akija kutoa majumuisho atueleze na atoe tamko la Serikali juu ya jambo hili ili liwaweke Watanzania katika utulivu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.