Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Hon. Khatib Said Haji

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Konde

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

MHE. HAJI KHATIB KAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Awali ya yote nianze kumshukuru Mwenyezi Mungu, muumba wa mbingu na dunia kwa kuniamsha salama siku ya leo nikiwa na afya na kuweza kufunga funga ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Vilevile niwatakie Ramadhan Mubarak waislamu wote duniani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kutoa mchango wangu kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri na Wizara kwa ujumla baada ya kuhoji kwa muda mrefu na kutaka wananchi wa Kisiwa cha Pemba waweze kufikishiwa elimu ya Mtangamano wa Soko la Afrika Mashariki. Namshukuru sana Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kumshukuru Mheshimiwa Waziri, niseme kwamba elimu ya mtangamano ya Afrika Mashariki haikuwafikia walengwa. Hii ni kutokana na kwamba wakati wa maandalizi Wabunge wa Pemba hawakushirikishwa, hasa mimi ambaye muda wote wakati nikiwa kwenye Kamati nimekuwa nikihoji ni lini wananchi wa Kisiwa cha Pemba hasa kule Kaskazini watafikishiwa elimu hii ambayo itaweza kuwasaidia na kuweza kujua wajibu wao na haki katika Soko la Afrika Mashariki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kisiwa cha Pemba, hasa Kaskazini Pemba, wananchi asilimia kubwa ni wavuvi. Wavuvi hawa kila mwaka, inapofika mwezi wa kumi hadi mwezi wa tatu wamekuwa wakisafiri kwenda nchini Kenya kufanya dago. Ni wazi kwamba wanakuwa wakipata matatizo na wananchi wangu wamewahi kufungwa nchini Kenya miezi sita na faini ya shilingi 20,000 juu. Kwa hiyo, hii ni kutokana na kwamba wananchi hawa hawajui wajibu na haki zao katika soko hili la Afrika Mashariki. Ndiyo maana nikasema kwamba wananchi wa Kisiwa cha Pemba hasa wale walengwa hawakufikiwa na elimu hii ya mtangamano wa soko la Afrika Mashariki ambayo ni muhimu kwa wananchi hawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema Desemba, 2015/2016 wapiga kura wa Jimbo langu wapatao 130 walifungwa kwa kuonewa. Hii yote ni kutokana na kwamba hawajui wajibu wao na ndiyo maana nikasema walengwa hawakufikiwa na elimu hii. Naomba nishauri kwa Mheshimiwa Waziri kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, endapo mara nyingine Wizara itaandaa utaratibu wa kwenda kutoa elimu ya mtangamano wa soko la Afrika Mashariki, basi ibadilishe maneno, badala ya kusema Wizara inaenda kufanya semina, basi maneno yasemwe kwamba tunaenda kutoa mafunzo. Hii itasaidia wale walengwa hasa kuweza kufikiwa na elimu iliyokusudiwa. Kwa kuwa Pemba ina sehemu kuu mbili, naomba na ninamshauri Mheshimiwa Waziri kwamba elimu hii igawanywe katika sehemu kuu mbili; katika Kisiwa cha Pemba kuna sehemu ya Kaskazini na Kusini, kwa hiyo, ni vyema katika taaluma hii au uelewa huu ugawanywe katika sehemu mbili ili taaluma hii iweze kuwafikia kama ilivyokusudiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, niseme kwamba katika taaluma hiyo hiyo ya Soko la Afrika Mashariki, yaani mtangamano ni vyema Wizara itapanga utaratibu na kuhakikisha kwamba Wabunge kutoka Pemba wote wanashirikishwa wakati wa maandalizi katika hoja hiyo ambayo itakuwa imepangwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema, ili kuondoa matatizo ambayo wavuvi wetu ambao wamekuwa wakiyapata hadi kufugwa jela nchini Kenya, ni vyema Serikali hizi mbiliā€¦

MWENYEKITI: Ahsante.