Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Fedha na Mipango

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Fedha na Mipango

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwako kwa kunipa fursa hii ya kuchangia hotuba hii ya Wizara ya Fedha. Nachukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri wake, pamoja na Watendaji wake wote kwa kutayarisha hotuba hii na kuiwakilisha kwa ufanisi mkubwa. Katika kuchangia hotuba hii, napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi kirefu sasa, mwenendo wa thamani ya fedha yetu imeendelea kuporomoka. Hii inaleta tabu kwa wafanyabiashara na wananchi. Napenda kumuuliza Mheshimiwa Waziri, Serikali ina mpango gani kuzuia mporomoko huu? Ni vema Serikali ikachukua hatua za haraka kuzuia jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taifa letu bado linaendelea kutegemea misaada kutoka nje ya nchi, hilo ni jambo baya na halifai kuendelea kuwepo. Serikali inatakiwa kuweka mipango mizuri ili kuondokana na utegemezi. Serikali yetu ina vyanzo vingi vya kiuchumi ambavyo kama tutavidhibiti, vitaweza kutuongezea pato na kuondokana na utegemezi huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya fedha ni miongoni mwa Wizara muhimu sana katika kuendeleza nchi hii. Hivyo namwomba Mheshimiwa Waziri kuendeleza mpango wa mafunzo kwa Wizara (training program) ili kuweka katika hali ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.