Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2017/2018

Hon. Yussuf Kaiza Makame

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Chake Chake

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2017/2018

MHE. YUSSUF KAIZA MAKAME: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina ajenda tatu tu za kuzungumza, ajenda ya kwanza ni huu mchanga wa dhahabu ambao kila mmoja anauzungumza. Ajenda ya pili ni ile sheria ambayo ilipitishwa na Bunge hili mwaka 2015 inayohusu mafuta na gesi na ajenda ya tatu ni hili deni la ZECO kwa TANESCO.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la mchanga; hapa hatuhitaji kunyoosheana vidole tena kama Bunge, hatuhitaji kunyoosheana vidole, hatuhitaji kuonesheana mchanga ulichukuliwa vipi au dhahabu iliibiwa vipi. Kinachohitajika sasa ni kuwa wamoja, hatuhitaji tena kukaa tofauti, kinachotakiwa tumeona kwamba tunaibiwa ni lazima Bunge liwe kitu kimoja, hatuhitaji kitu kingine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivi kwa sababu Mheshimiwa Profesa Muhongo kabeba wizi wote au uhanga wa miaka au nusu karne, miaka 50 tumekuwa tukiibiwa mhanga leo katolewa Mheshimiwa Profesa Sospeter Muhongo, kaondoka. Mbuzi wa kafara kashaondoka na tulishajua nini tulichoibiwa, tujitahidi tukae pamoja kwa ajili ya Taifa na manufaa ya watoto wetu wanaofuata. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri kwa Serikali; kwangu mimi na muono wangu, hii ni sehemu nzuri kabisa ya kuanzia. Haiwezekani unakuwa unaibiwa baadaye ukasema kwanza usizuie mali iliyoibiwa utafute namna ulivyotayarisha kuibiwa. Kwanza ukamate mali, baadaye u…, haya, ila mkubali makofi haya myakubali kwamba ninyi ndio mliotuingiza katika wizi wa miaka 50 na hili mpige makofi. Kama mlivyoleta ndege, mkubali kwamba ninyi CCM au Serikali ya CCM ndio mliotupeleka kwenye wizi huu wa miaka 50; na mkisimama mjisifu na mkubali udhaifu wenu, hilo ni moja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la pili, nashauri mikataba, sheria na zile sera zote tuzilete Bungeni na zile zinazotakiwa kwenda kwenye mamlaka ya utendaji zifanyiwe marekebisho ili mambo haya yasijitokeze tena. Hata hivyo, tujenge refinery zetu wenyewe, kwa nini tunashindwa? Wameamua kuhamia Dodoma bila bajeti wameweza, kwa nini wanashindwa kujenga viwanda vya kuchakatia dhahabu yetu hapa? Kwa nini wanashindwa hili? Wamewalipa wafanyakazi wa Wizara ya Fedha milioni 10, 15, 20 wengine kuhamia Dodoma, wanashindwa ku-maintain hii mali yetu tuliyonayo? Hii ni natural resources, ikiondoka hakuna tena. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine, nashauri, kwa nchi za wenzetu wenye maono ya mbali wanajenga, kwa sababu hizi zikiondoka hazirudi tena, baada ya miaka 50, 55 hatuna tena hiki kitu. Kwa hiyo, tusije tukawaonesha wenzetu historia ya mashimo, tuwaoneshe kwamba tulikuwa na dhahabu, tulikuwa na tanzanite, tulikuwa na whatever, kwa hiyo hivi vyote vinatakiwa vifanyike.

Mheshimiwa Naibu Spika, nichangie pia Sheria ya Gesi; Waheshimiwa Wabunge, Sheria ile ya Mafuta waliiingiza mkenge Zanzibar na lazima wakubali na walivunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 102(1), Ibara ya 105(2), Ibara ya 106(3), zote walizivunja…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)