Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa Kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

Hon. Ali Hassan Omar King

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Jang'ombe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa Kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza mimi ilikua nianze kwa neno moja ambalo ni maarufu sana ambalo hizi hoja zote zinazozungumzwa zinaingia katika al-jununu fununu (uendawazimu una matawi mengi sana), lakini akili fani yake moja tu; leo wako wengine wanaotaka kupongeza huko, wako wengine hawataki, wako wengine wanasema wasishurutishwe, wako wengine wanatakiwa wasilaumiwe sasa mko wapi wenzetu? Hizo ni fani za wendawazimu zote, lakini CCM ni fani moja tu, sisi tunapongeza kwa Rais kitendo alichokifanya, kwa hiyo, ninyi msipopongeza ni kazi kwenu kwasababu al-jununu fununu (wendawazimu una matawi mengi) kwahiyo gawaneni hayo matawi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wapo watakaodandia la kupongeza, watakaodandia la kusema kwamba lawama, endeleeni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kingine msiseme uongo, mnasema mnafanya research ninyi? Mnasema kwamba bajeti inatakelezwa kwa asilimia 38, ni bajeti ipi? unaijua bajeti? Kuna bajeti ya maendeleo, kuna bajeti yenyewe kuu mnazungumza nini? mnasema mmefanya research hao waliowafanyieni research ni wakaotaji kuni wa usiku wamewafungieni na nyoka humo humo. (Kicheko/ Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawajui, hakuna jambo la maana ambalo wameeleza. Tazama bajeti pesa zilizotoka, halafu ukaangalie maendeleo...

T A A R I F A .....

MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri hafahamu kidogo al jununu maana yake ni uwendawazimu una matawi mengi, kwa hiyo wewe tena utajijua kama upo kama tawi la uwandawazimu utakuwa mwendawazimu. Sasa tunasema hivyo ndivyo bajeti inavyotekelezwa.

Mheshimiwa
Mwenyekiti, ahsante nilindie muda wangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa kimezungumzwa kitu ambacho hakihusiani kabisa, kumezungumziwa uchaguzi wa Zanzibar. Sawa, tarehe 25 Oktoba, kulikuwa na NEC kuna ZEC hata kuku wanataga mayai na mayai mengine yakawa viza. Kwa hiyo, uchaguzi ule kwa Wanzanzibar kule ZEC ulikuwa ni viza, na kitu viza huwa si riziki. Naogopa kusema kwamba na aliochaguliwa labda ilikuwa si riziki maana hakupata. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nizungumzie jambo moja kwa Mheshimiwa Waziri wa Fedha, kuhusu takwimu za viwanda. Tunaelekea katika nchi ya viwanda lakini bado tunategemea takwimu kutoka katika taasisi binafsi. Takwimu kutoka katika taasisi binafsi haziwezi kutusaidia kwa sababu kila mmoja ana takwimu zake. Tunacho kitengo chetu cha takwimu za Serikali, kwa nini tusitumie katika kufikia katika Fiscal Policy zetu? Tutumie kitengo hicho cha Serikali, namshauri Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na lingine kwa Zanzibar kuna VAT ambayo ilianzishwa mwaka jana ya Section 55(a) ambayo bidhaa za kutoka Bara kwenda Zanzibar na zinazozalishwa Zanzibar kuja Bara zilikuwa zimewekewa zero rated. Lakini zero rated hiyo wako watu ambayo ni registered VAT na wengine hawakuwa registered, hawa ambao hawako registered hawatambuliwi, kwa hiyo, wanalipishwa VAT mbili analipishwa na TRA analipishwa pia na ZRB. Kwa hiyo hapa tuangalie, tusiweke double standard tukiweka double standard tutumie destination principles kwa wote, tuwatambue kwa vitambulisho ambavyo wanavyo ili tuwasaidie wafanyabiashara hawa wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine nizungumzie utalii. Ili kuweza kukuza mapato yetu na Pato la Taifa liweze kukua, tuna vivutio vikubwa vya utalii katika Tanzania. Tanzania kwenye dunia ni nchi ya pili kwa kuwa na vivutio vizuri baada ya Brazil. Kwa hiyo, tukitumia vivutio hivi vya utalii tunaweza tukaja tukafikia mahali pazuri ili Tanzania yetu nayo iweze kung’ara na tuweze kupata mapato mazuri katika nchi yetu hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mzungumzaji wa Kambi ya Upinzani katika introduction yake alitaja msemo mmoja ambao aliuzungumza Baba Nelson Mandela. Nelson Mandela amesema no easy walk to freedom kwamba hakuna easy walk katika kuuendea uhuru, lakini wenzetu wanataka uhuru upi? Wale waliofanya hivyo anawatetea ni watovu wa adabu ambao Bunge hili liliwapa adhabu. Sasa wao wanawatetea Waheshimiwa watatu ambao walipewa adhabu hapa kutokana na utovu wa adabu. Kwa hiyo wanawasema hapa kwamba no easy walk to freedom kwamba je wanataka uhuru wa kutukana humu ndani? Wanataka uhuru wa kutovuka adabu humu ndani? Wanataka uhuru wa kutokusikiliza kitu humu ndani? Kwa hiyo, hicho sio kitu kizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia tunazungumzia katika upande huo huo, kuna watu walisema kwamba bajeti…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.