Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Itifaki ya Nagoya ya Kusimamia Upatikanaji na Mgawanyo Sahihi wa Faida zitokanazo na Matumizi ya Rasilimali za Kijenetiki.

Hon. Rev. Peter Simon Msigwa

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Iringa Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Itifaki ya Nagoya ya Kusimamia Upatikanaji na Mgawanyo Sahihi wa Faida zitokanazo na Matumizi ya Rasilimali za Kijenetiki.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, in principle sina tatizo na itifaki zilizoletwa, lakini nilitaka tu tujitafakari kama Bunge. Hili Bunge letu la Bajeti ni Bunge la muda mrefu na Bunge huwa linajua ratiba itakuwaje. Lakini kumekuwa na mazoea kila siku mnapoleta itifaki hizi mnatuletea siku hiyo ya kupitisha hizo itifaki. Hii inaonesha jinsi gani ambavyo Bunge linaonekana halitimizi wajibu wake na kwamba Serikali inatuchukulia poa tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi vifungu ukiwauliza Wabunge unavipitia saa ngapi, kila wakati itifaki zinapokuja zinaletwa siku hiyo hiyo, hivi vifungu unavipitia saa ngapi? Unasoma saa ngapi? Unapewa dakika tano kuchangia wakati ingegaiwa mapema kwenye Kamati watu wangepitia tunapojua ratiba inavyokwenda tuje tusome, lakini imekuwa business as usual tunapiga makofi na Bunge tunakubaliana mikono yetu na nguvu yetu ya Bunge inapungua nguvu kwa mambo kama haya ya kuridhia mambo ambayo hayawezekani, kwa sababu ni mambo ya msingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Watalaam wanasema the past is where you have learn the lesson and the future is where you apply the lesson. Asubuhi hapa tumejaribu hata kuomba miongozo, mambo ya Hati za Dharura tunarudia tena kana kwamba mambo ya nyuma hatujajifunza kwa sababu tunaenda haraka haya mambo! Wabunge hebu tujiulize, hivi wananchi huko wakituona tunaondoka tumebeba mavitabu haya, tunasoma saa ngapi? Tunasoma saa ngapi hivi vitabu! Tunaletewa muda mfupi! (Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, hii ni kulifanya Bunge liwe crippled, Bunge ambalo haliwezi kuisimamia Serikali, kwa hiyo hapa sisi tumekuja ku-rubber stamp. Tukubaliane kwamba, Bunge hili linaongozwa na Serikali, Bunge haliwezi kuisimamia Serikali kwa sababu tunakuja hapa tuna-rubber stamp… (Makofi)

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachoomba hili Bunge letu, Serikali iwe inafanya vitu kwa utaratibu, kwa sababu Serikali zote duniani huwa zinapenda


kulifanya Bunge liwe kibogoyo ili zifanye mambo yake vizuri. Na sisi kama Wabunge tuna wajibu wa kuhakikisha tunachukua role yetu kuisimamia Serikali. Hatuwezi kuchukua role kama tunauziwa mbuzi kwenye magunia. Huku ni kuletewa mbuzi kwenye magunia, halafu tunashangilia katika vitu ambavyo hatujasoma, na ni kukwepa wajibu wa Bunge. (Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, tunaposema mikataba na sheria ziletwe Bungeni hatumaanishi iletwe kama hivi itupwe hapa! Tuna maana iletwe tupate muda wa kuisoma na kuitafakari ili tuone ni jinsi gani tunawawakilisha wananchi ambao wametutuma, lakini ikiletwa tu hapa inakaa mezani, inaletwa hapa, halafu wanasema tunaazimia, watu tunapiga makofi, tunasema ililetwa Bungeni, hiyo siyo maana halisi ya kuletwa Bungeni. Hakuna kati yetu hapa aliyesoma hapa tukisema lipi ambalo tunaazimia hapa, waliosoma ni wachache sana kwenye Kamati idadi kubwa ya Wabunge hatujasoma. (Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, hilo ndiyo naliomba tuliinue Bunge letu kiwango. The more tutakuwa na Bunge dhaifu, the more tutakuwa na Serikali dhaifu. Hawa Mawaziri lazima tuwashughulishe wafanye kazi. Hawa Mawaziri hawatafanya kazi kama Wabunge tutakuwa weak. Ni lazima tuwe after them, watakuwa na nguvu ili kuishauri Serikali na ndiyo wajibu wetu. (Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi. (Makofi)