Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua fursa hii kukushukuru wewe kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia katika Wizara hii muhimu katika nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, nampongeza Mheshimiwa Waziri wa Wizara hii pamoja na watendaji wake wote kwa kuandika hotuba hii na kuiwasilisha kwa utaalam mkubwa. Nawaomba waendelee na ari hii ili wafikie lengo tulilojiwekea.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuchangia hotuba hii, napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, mahitaji ya maji katika nchi yetu ni makubwa sana na yanaongezeka kila siku. Maji haya mbadala ni muhimu katika dunia kwani unapokosa maji na uhai haupo. Naipongeza Serikali kwa juhudi kubwa inayochukua katika kuondoa matatizo ya maji vijijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wa vijijini wanaendelea kujichimbia visima katika maeneo yao. Nashauri Serikali iendelee kuwaunga mkono kwa njia zote, yaani kwa utaalam na kifedha kwa sababu uwezo wao vijijini siyo mkubwa kifedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali yetu inatakiwa kuweka mipango mizuri ili kuweza kujitegemea, tuepuke kuwa wategemezi wa misaada kutoka nje ya nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika bajeti ya mwaka 2016 ilionesha kuwa Serikali ya India imetusaidia fund ya dola milioni 208,033 kwa miji sita katika nchi nzima pamoja na visiwa vya Zanzibar.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi viongozi wa Majimbo tumekuwa tukiwaeleza wapiga kura wetu juu ya fedha hiyo na kuwaomba waendelee kustahimili mambo yatatengemaa. Mpaka sasa baada ya mwaka mmoja kupita hakuna matokeo yoyote mazuri juu ya fedha hii. Hivyo,
namwomba Mheshimiwa Waziri atupe maelezo mazuri ni nini kimesababisha mpaka leo kutopatikana kwa fedha hii?

Mheshimiwa Naibu Spika, mabadiliko ya hali ya hewa yanaongezeka ulimwenguni. Misimu ya mvua imekuwa haitegemeki kwa kasi za ukulima. Hivyo, ni vyema Serikali ikachukua juhudi zaidi katika kuendeleza Sekta ya Umwagiliaji ili iweze kufikia kiwango kizuri cha mahitaji. Asilimia 24 iliyopo hivi sasa ni ndogo sana kwa sekta hii. Nchi yetu ina vyanzo vingi vya maji ambavyo vikiboreshwa vitaweza kusaidia sana katika nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.