Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kukushukuru wewe kwa kunipa fursa hii ya kutoa mchango wangu kwa maandishi kuhusiana na hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua nafasi hii kumpongeza Waziri pamoja Watendaji wake kwa kuandika hotuba hii kwa ufundi na utaalam mkubwa, namwombea kila la kheri katika kuiongoza Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuchangia hotuba hii, napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ni kuhusu rasilimali watu katika sekta ya afya. Rasilimali watu ni miongoni mwa jambo muhimu katika nchi hasa katika Wizara kama hii ambayo inahitaji utendaji wa kitaaluma zaidi. Ushauri wangu katika Wizara hii ni kuongeza juhudi ya kuwasomesha Watanzania katika fani zote hasa ya udaktari ili kupunguza pengo kubwa lililopo kati ya Madaktari na wanaohudumiwa. Takwimu zinaonesha kuwa uwiano (ratio) kati ya Madaktari na wagojwa ni mkubwa sana. Hivyo juhudi za makusudi zinahitajika ili kuondoa kabisa tatizo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, naomba kuongelea kuhusu uboreshaji wa huduma za uchunguzi. Uchunguzi wa maradhi ni hatua muhimu sana katika matibabu. Mgonjwa anapochunguzwa na kuonekana kinachomsumbua ni mwanzo mzuri wa matibabu. Ushauri wangu katika jambo hili ni kwa Serikali kuongeza fedha za kutafutia vifaa vya kisasa zaidi vinavyoweza kuchunguza maradhi kwa ubora zaidi. Kuna matukio mengi ambapo wagonjwa wanachunguzwa na kupewa majibu ambayo ni tofauti na maradhi yanayowasumbua. Hii ni kutokana na kutumia vifaa ambavyo havina ubora. Hivyo juhudi za makusudi zinahitajika ili kuondoa tatizo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu ni kuhusu udhibiti wa UKIMWI. Naipongeza Wizara kwa juhudi kubwa inayochukua kudhibiti na kuwahudumia waathirika wa maradhi ya UKIMWI. Napenda kuishauri Wizara kuongeza juhudi ya kutoa elimu kwa wananchi hasa wa vijijini ili kuelewa zaidi sababu zitakazowafanya wapate maradhi hayo. Inaonekana kuwa elimu ya UKIMWI inatolewa zaidi katika miji na kidogo sana katika vijiji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.