Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

Hon. Lucy Fidelis Owenya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kupata nafasi ya kuchangia. Ili mtu aweze kuendelea ni lazima kwanza awe na afya bora. Hivyo basi, sekta ya afya ni muhimu sana kuhakikisha Serikali inatenga bajeti ya kutosha. Je, ni lini Serikali itatimiza Azimio la Abuja?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu magonjwa yasiyoambukizwa None Communicable Diseases(NCD); magonjwa haya kama sukari ya kupanda na kushuka, shinikizo la damu ya kupanda na kushuka, magonjwa ya moyo na kadhalika, mengi ya magonjwa hapa yanayoweza kuepukika tu kama elimu ya kutosha inaweza kutolewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, siku hizi imekuwa ni kawaida watu kununua vyakula vya barabarani kama chips, mihogo, sambusa na juice zenye sukari nyingi, unywaji wa pombe na ulaji wa nyama nyekundu kupita kiasi, vitu vyote hivi vinachangia kuongezeka kwa magonjwa haya, hata watoto wadogo mpaka wenye miaka 10 wanapata magonjwa haya. Je, Serikali ina mikakati gani ya kupunguza au kutokomeza magonjwa haya?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano nchi za Ulaya sasa hivi wanahimiza watu kufanya mazoezi, wanashauri wafanyakazi kutembea kwenda kazini, lakini hapa kwetu ni vigumu sababu barabara zetu siyo rafiki kwa matembezi ya miguu. Ni kwa nini Wizara ya Afya isishirikiane na Wizara ya Miundombinu ili wakijenga barabara wahakikishe wanajenga barabara za wapita kwa miguu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ndoa za utotoni na mimba za utotoni. Ni wakati muafaka sasa kuhakikisha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 inarekebishwe ili isiruhusu watoto wa kike kuolewa wakiwa na miaka 14, tukumbuke wasichana hawa wakipata mimba utotoni mara nyingi wakati wa kujifungua huchukua muda mrefu sababu uchungu huchukua muda mrefu na hali hii huweza kusababisha kifo cha mama au mtoto au wote wawili kama matibabu ya dharura ya upasuaji kwa ajili ya uzazi hayatafanyika na ukizingatia vijijini huduma hizi sehemu nyingi hazipo na umbali wa kutoka kijijini mpaka Wilayani miundombinu ni mibovu pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watoto hawa pia hukosa fursa ya elimu kwa kuwa wengi wao hufukuzwa shule, wazazi husita kuwaendeleza na hii hupelekea baadhi ya watoto hawa wa kike kufungua mlango wa kuingia katika umaskini na kuzaa ovyo bila mpangilio.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo kubwa zaidi wengi hupata fistula (vescovaginal fistula (VVF) au rectovagina fistula (RUF), hii husababisha msichana kutokwa na haja ndogo au kubwa bila kujizuia. Haja kubwa pia inaweza kumtoka msichana kwa kupitia tupu ya mbele na hii kuharibu sana afya ya mwili na hisia za msichana. Hayo ni machache tu kati ya matatizo ya mimba za utotoni, ni imani yangu Serikali itayaona haya na kuleta marekebisho ya sheria mapema iwezekanavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upungufu wa vifaa tiba na madawa. Hospitali nyingi hazina vifaa vya akina mama vya kujifungulia, hata baadhi ya hospitali hazina madawa. Mfano, tarehe 28 Februari, 2017 kulikuwa na mashindano ya Kilimanjaro Marathon na pale uwanjani kulikuwa na kitengo cha huduma ya kwanza, jambo la kusikitisha pale kwenye huduma ya kwanza hawakuwa na mtungi wa kuongeza hewa (oxygen). alikuwa na kijana aliyekimbia na alikuwa mahututi na alihitaji oxygen lakini wahudumu wale hawakuwa na mtungi wa oxygen na kibaya zaidi ambulance ilivyofika na wao pia hawakuwa na oxygen cylinder na kupelekea kijana yule kufariki pale uwanjani. Mungu alilaze roho yake mahali pema peponi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama magari yote ya kuokoa yangekuwepo na vifaa vyote, pengine kijana yule angeweza kupona. Je, katika bajeti hii ni kiasi gani kimetengwa kwa ajili ya vifaa hivi hata MRI kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya KCMC? Kipimo hiki ni muhimu sana kwa Hospitali ya Rufaa kutokuwa nacho unakuta wagonjwa wanaagiziwa kwenda kwenye hospitiali za binafsi kufanya vipimo hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuipongeza Hospitali ya KCMC kwa kuanzisha kitengo cha saratani kama ilivyo Ocean Road, ni vizuri kitengo hiki kianzishwe Mwanza na Mbeya. Serikali iwasaidie kwa kupeleka wataalam, vifaa tiba na ruzuku kwa ajili ya kitengo cha kansa kule KCMC.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shilingi milioni 500 hazitoshi zinahitajika shilingi bilioni saba za kujenga jengo la kuweka vifaa walivyovipata vya msaada.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamekuwepo na ongezeko kubwa sana la kansa ya shingo ya kizazi, tumepoteza akina mama wengi lakini ugonjwa huu unaweza kuepukika kama ukigundulika mapema, lakini huduma ya kansa ya kizazi sio hospitali zote zinatoa huduma hapa nchini na kupelekea vifo vingi. Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka huduma hizi hata mpaka kwenye ngazi ya vituo vya afya?

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado maambukizi ya UKIMWI yapo juu sana, lakini kuna tatizo kubwa la upatikanaji wa kondomu za kike, je, Serikali ina mpango gani ili tuokoe watoto wa kike?