Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira

Hon. Juma Ali Juma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dimani

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira

MHE. JUMA ALI JUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kupata ufafanuzi wa Ibara ya 48 ya kitabu cha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mfuko wa Mazingira wa Dunia (Global Environment); je, sifa zipi zinazotakiwa kwa vikundi vya kijamii vinavyotarajiwa kuandika miradi midogo midogo ili viweze kunufaika na ufadhili wa G.E.F katika mwaka wa fedha. Je, katika vikundi 53 vya kijamii vilivyoshauriwa na Ofisi ya Makamu wa Rais ni vikundi vingapi kutoka Zanzibar vilifaidika na ushauri huo.