Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.

Hon. Lucy Fidelis Owenya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kupata nafasi ya kuchangia. Mgogoro wa ongezeko la vijiji kuingia hifadhi, Mbarali Mbeya. TANAPA inaongoza vijiji 21 kuingia katika hifadhi lakini vijiji hivi ni vya wakulima wa mpunga na mgogoro huu umekuwepo kwa
zaidi ya miaka nane. Wakati wa kampeni za Urais 2015 Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli aliahidi kuwatengenezea barabara ya lami ambayo imeanza kutekelezwa na akatoa agizo vijiji vile visichukuliwe na hifadhi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakulima hawa wa mpunga wanazalisha magunia mpaka 1,300,000 sawa na tani 104,000 kwa mwaka. Katika vijiji hivyo vipo viwanda vya kukoboa mpunga vikubwa 42 na magodauni 56 makubwa. Kwa kuvichukua vijiji hivi tayari ajira zitapotea takriban watu 10,000 watakosa ajira. Ukizingatia agizo la Rais ni kuwa Tanzania ya viwanda. Je kwa kutaifisha vijiji hivi na kuvifanya hifadhi Tanzania ya viwanda itatekelezekaje? Serikali isitishe kuvichukua vijiji 21 kwa faida ya maendeleo ya wananchi wanaoishi pale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, michezo ni afya na kwa sasa hivi magonjwa yasiyoambukiza kama sukari ya kupanda na kushuka na shinikizo la damu la kupanda na kushuka magonjwa ya moyo magonjwa haya kwa sasa yanawapata hasa watoto wadogo lakini yanaweza kuzuilika kwa watu kufanya mazoezi na Serikali kupitia Makamu wa Rais, aliagiza watu wafanye mazoezi kwa nia nzuri tu lakini cha kujiuliza watu watafanyia wapi mazoezi. Halmashauri nyingi hazina viwanja vya michezo na Mheshimiwa Waziri Mkuu katika hotuba yake hajaelezea kabisa mikakati ya kujenga viwanja na ya kupata viwanja hivyo vya mazoezi?