Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) pamoja na Maoni na Mapendekezo yaliyomo katika Taarifa hiyo; na Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) pamoja na Maoni na Mapendekezo yaliyomo katika Taarifa hiyo

Hon. Aeshi Khalfan Hilaly

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sumbawanga Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) pamoja na Maoni na Mapendekezo yaliyomo katika Taarifa hiyo; na Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) pamoja na Maoni na Mapendekezo yaliyomo katika Taarifa hiyo

MHE. KHALFAN H. AESHI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kuniona na kwa kunipa dakika tano zilizobaki na naomba kuchangia maeneo machache sana. Kubwa napenda kuchangia suala la kilimo na Wizara ya Kilimo kwa ujumla pale ambapo Serikali tumepoteza zaidi ya shilingi bilioni sita kwa mahindi yaliyoharibika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ilipitia taarifa hii, kimsingi tumesikitishwa sana na hatua zilizochukuliwa kwa Wakurugenzi wa Idara ile. Mwaka 2013/2014 Serikali ilitoa maagizo kwamba wananchi wasiuze mazao yao nje ya nchi na Serikali itanunua mahindi yote. Kwa bahati nzuri wananchi walilima mahindi mengi sana na kwa bahati nzuri Serikali ilianza kununua mahindi yale, lakini kwa bahati mbaya mahindi mengi yalirundikana Serikali ikawa haina uwezo wa kuyanunua. Ikafikia mwezi wa Novemba mvua zikaanza kunyesha, mahindi yakaharibika yakiwa nje hayajapokelewa na NFRA.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikiwa Bungeni Serikali ilitoa tamko kwamba mahindi yote yaliyoko nje yanunuliwe na Serikali. Hapo ndipo kilipotokea kituko kwamba wananchi waliiuzia mahindi NFRA kwa mkopo, hatukuwa na uwezo wa kulipa mahindi yale. Mwaka 2014 kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa sehemu nyingi tulipoteza nafasi zile kwa sababu wanachi walisema tumewakopa mahindi hatujawalipa. Cha kushangaza mahindi haya yalivyotunzwa yakiwa yameloana na mvua yaliharibika, lakini juzi miezi mitano iliyopita Serikali iliamua kuyauza mahindi yale mabovu. Tukapoteza takribani shilingi bilioni sita na pesa za ziada. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini nachangia jambo hili? Waziri wa Kilimo aliyekuwa wakati huo, Mheshimiwa Mwigulu Mchemba aliidhinisha mahindi yale mabovu yauzwe. Baadaye Waziri wa Kilimo akahamishwa akachaguliwa Waziri mwingine mpya, Mheshimiwa Tizeba, haikuchukua siku mbili akawafukuza kazi Wakurugenzi wote bila makosa. Sasa nataka aje Waziri atueleze ni njia ipi aliyotumia au ni utafiti upi aliofanya na kuwasimamisha kazi Wakurugenzi wale bila kosa lolote kwa sababu mahindi yale yaliharibika kutokana na idhini ya Serikali tununue mahindi yaliyoloana na mvua. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, inauma mtu ambaye amefanya kazi kwa muda mrefu, mtu ambaye amelitumikia Taifa hili kwa uaminifu na kwa kazi ya kutukuka lakini anakuja mtu kumtumbua jipu bila kosa lolote. Nataka niseme tunamuomba Waziri wa Kilimo aje atutolee sababu ipi aliyotumia kuwasimamisha kazi Wakurugenzi wa Idara ile ya NFRA? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini lingine kubwa ambalo ni la kushangaza, tuna Meneja anatokea Mkoa wa Rukwa, amekaa Mkoa wa Rukwa takribani miaka 15, hana kosa lolote, kahamishwa kwenda Mkoa wa Songea ndani ya wiki mbili lakini kosa lile la kununua mahindi mabovu linamkuta yeye na yeye anasimamishwa kazi. Haki iko wapi? Mtu afanye nini ili alitumikie Taifa kwa uaminifu mkubwa? Kwa hiyo, sisi kama Kamati tunamuomba Mheshimiwa Waziri aje atujibu hatua zipi alichukua yeye kwenda kuwasimamisha kazi watu bila kuwa na kosa? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kila mtu anataka aonekane anafanya kazi ndani ya Serikali. Kila mtu anataka aonekane anachukua jukumu lake kusimamia watu wengine, lakini hili sisi kama Kamati tunamtaka Mheshimiwa Waziri wa Kilimo aje atujibu kwa nini aliwachukulia hatua wale bila kuwa na kosa lolote wakati kosa lilitokea tukiwa hapa Bungeni mwaka 2014. Tumuulize Waziri wa Kilimo aliyepita kwa nini aliruhusu mahindi yale yauzwe mabovu? Mbona yeye hakuwasimamisha kazi? Yeye hakuliona hili? Aliliona lakini wale walishindwa kwa sababu walikuwa wanasubiri ripotiā€¦
Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa na mengi ya kuongea kwa sababu muda wa dakika tano ni mfupi, naamini jioni nitakuja hapa kuongea tena dakika 15 zingine lakini namuomba Mheshimiwa Waziri aje atujibu katika hili. Ahsante.