Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mkataba wa Ubia wa Uchumi baina ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya.

Hon. Saada Salum Mkuya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Welezo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Mkataba wa Ubia wa Uchumi baina ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya.

MHE. SAADA MKUYA SALIM: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kupata fursa hii na mimi nichangie katika mjadala uliopo mbele yetu. Na mimi naunga mkono hoja hii ya Serikali kwamba tusisaini mkataba huu kama ulivyo.
Mheshimiwa Spika, kabla ya kuendelea mbele naomba ku-quote maneno ya Rais Mstaafu ambayo yalikuwa posted kwenye gazeti la East African, Mheshimiwa Mkapa alisema kwamba EPA is bad news for entire region. It is just bad news for entire region wala siyo for Tanzania, but for entire region.
Mheshimiwa Spika, mkataba kama huu kama ungekuwa una terms nzuri, basi nadhani ingekuwa faida kwa region, lakini faida vilevile kwa Tanzania. Terms zake hazifanani na haziendani. Mheshimiwa Rais Mkapa alisema vilevile kwamba the EPA for Tanzania and the EAC never made sense, the maths just never added up yaani zile hesabu zake haziendi kutokana na hali yetu ya kiuchumi.
Mheshimiwa Spika, pengine ingekuwa sisi kama East Africa tunahitaji zaidi EU wana soko la watu karibu milioni 700, East Africa tuna watu karibu milioni 300 plus, tungekuwa tunawahitaji zaidi kama angalau kungekuwa kuna ule uchumi unaoendana, lakini hatufanani. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, isipokuwa tumeuleta huu mkataba hapa na tutaukataa kabisa, lakini tuchukue hii kama ni nafasi ya Tanzania kuweza kujijenga zaidi.
Kwanza, kwenye viwanda, lakini pili pengine Mheshimiwa Waziri ulichukue hili iwe ni changamoto, ingekuwa vyema kwamba huu mkataba tunaukataa, lakini wataalam wetu watuletee alternative, yaani zile terms zinakuja, hizi haziwezekani, what do we want? Tunakoelekea regional integration ndiyo itakuwa inapata nafasi zaidi kuliko bilateral cooperation.
Mheshimiwa Spika, leo hatuuhitaji mkataba kama huu lakini ninaamini sera yetu ya kujenga viwanda itakapokuwa imefanikiwa, tutakuwa tunahitaji mikataba ya aina hii. Kwa maana hiyo, tutakapokuwa tunakwenda, tuone ni jinsi gani tunaweza kujenga uwezo wa watu wetu, kwanza, kuangalia critically mikataba ya aina hii, lakini secondly iendane na policy zetu ambazo pengine tungeweza ku-compete zaidi na mikataba mingine au na masoko ambayo yanaambatana na mikataba kama hii.
Mheshimiwa Spika, mkataba kama EPA unamaanisha nini? Tunakokwenda development cooperation inapungua na badala yake inakuja trade cooperation. Kwa maana hiyo, kama leo tutakuwa tunategemea zaidi development cooperation, kwa maana ya nchi matajiri kusaidia masikini, lakini kesho na nchi matajiri na wao zitataka ku-benefit kutoka kwa nchi masikini kama ilivyo sasa hivi.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hii ni changamoto kwetu sisi. Tutakuwa tumeshinda leo, lakini ninaamini kwamba ni nafasi nzuri ya kujiweka vizuri zaidi kuona kwamba tutakapokuwa tunakwenda mbele, watakuja wengine na mikataba kama hii, tutaweza ku-face vipi? Hatuwezi kukataa kila siku, lakini ninaamini kwamba tunaweza kuchukua fursa hii kama changamoto na tukajiweka vizuri zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kupitia kwako namuomba Mheshimiwa Waziri, ninaamini kwamba mkataba huu utakwenda kuathiri development cooperation na EU. Nadhani tumekuja mwaka 2013, Mheshimiwa Waziri wa Fedha by then, tulikuja tukataka ridhaa ya Bunge kwa ajili ya kuridhiria Cotonou Agreement ambapo ndani yake tunapata misaada mbalimbali. Sasa kama sasa hivi tunakataa huu mkataba ambao ni trade related, sina uhakika wala hatuombi, lakini inawezekana tukaathiri aid cooperation na EU, wanatusaidia!
Mheshimiwa Spika, sasa namuomba Mheshimiwa Waziri, mkataba huu ambao tutaukataa hapa Bungeni leo, ninaamini afanye namna atakavyofanya aende akawaelimishe wananchi wa Zanzibar kupitia Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi. Kwa sababu ninaamini nao watafurahia jambo hili ambalo limekuwa decided na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Zanzibar kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanapaswa kufahamu jambo ambalo linaendelea ambalo lina maslahi ya Kitaifa.
Mheshimiwa Spika, namuomba Mheshimiwa Waziri, Baraza la Wawakilishi linaketi mwisho wa mwezi huu, aende akawape semina Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ili na wananchi wa Zanzibar na wao waweze kuona kabisa kwamba Serikali pamoja na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limefanya jambo la maana kabisa kutoku-rectify mkataba kama huu.
Mheshimiwa Spika, la pili, hii inakwenda zaidi kwenye regional integration. Na sisi tunahitaji zaidi tu haya mahusiano. Sasa kwenye hili, pamoja na mambo mengine kama nchi tufanye jitihada zetu kuweza sana kuhimiza South South Cooperation, yale mahusiano yetu na nchi ambazo tunafanana nazo kiuchumi, kimazingira na kiitikadi ili tuone kwamba hatuendi tu mbele tukawa tuna mahusiano na European Union watu ambao tupo tofauti kiuchumi hata kiitikadi, lakini vilevile tuwe tuna sera madhubuti ya kuweza kuimarisha uhusiano wetu na nchi ambazo Kusini Kusini, yaani tunaita South South Cooperation. Mheshimiwa Waziri hilo nakuomba sana ulichukue.
Mheshimiwa Spika, vilevile Mheshimiwa Waziri la tatu; kwa vile tunategemea athari kubwa itatokana na kutoku-rectify hapa, bajeti yetu itakayokuja tuhakikishe kwamba ile miradi ambayo ilikuwa inafadhiliwa na EU, tuiwekee mikakati ili Serikali yetu iweze kuibeba iende ikafadhiliwe na Serikali yenyewe, ama angalau tutafute alternative. Zanzibar tumefaidika sana na Cotonou Agreement; tumejengewa bandari, vilevile kuna miradi mingi ya maji ambayo EU imesaidia, lakini vilevile kuna miradi mingi ya utawala bora kupitia NGOs imesaidiwa. Tunaomba sana Serikali ijipange ili tuweze kutafuta mbadala wa nani na vipi itasaidia kuweza kuendeleza miradi kama hii.
Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo, naunga mkono hoja. Yangu yalikuwa machache sana, kwamba Serikali isisaini, lakini tuchukue hii kama changamoto kuweza kusimama zaidi, kujiimarisha zaidi na watu wetu.
Mheshimiwa Spika, ningependa zaidi kwamba kama unakuja mkataba huu tunaukataa, lakini angalau kungekuwa na mapendekezo mbadala, yaani tuseme kifungu hiki hatukiwezi, hatukitaki, basi tuwe na kifungu kama hiki ili tuendane nacho. Kwa maana na sisi kama block tunawahitaji wenzetu. Leo huu ni mkataba, siyo mzuri, lakini ninaamini wakati ambapo sera zetu zitakaposimama sawasawa na kufanikiwa, tutawahitaji wao na wengine.
Kwa hiyo, naomba zaidi tuwe tunafanya kazi ya ziada. Technical Committees zinapokaa ziwe zinafanya kazi ya ziada na siyo kukataa, lakini vilevile walete mapendekezo kwamba ingekuwa bora jambo kama hili lingekuwa limekaa namna kama hii. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Namwomba Mheshimiwa Waziri, tunasubiri semina kule Zanzibar ili hili liweze kujadiliwa, lifahamike na wananchi nao wapate kufaidika kutokana na maelezo haya. Nashukuru.