Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 20 16/2017 - Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora

Hon. Joseph Osmund Mbilinyi

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Mbeya Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 20 16/2017 - Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, I am going to try to be polite today ili nichangie kuona nchi yetu inaenda namna gani. Nitajikita kwenye masuala ya biashara; kubwa, kati na ndogo ambayo yana-reflect kwenye masuala ya ajira kwa namna moja au nyingine. Nitaanza na tatizo lililopo bandarini sasa hivi kwenye suala la mizigo kupungua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, bandarini mizigo imepungua sana na nashukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu amekuwa mfuatiliaji sana wa namna bandari ya Dar es Salaam inavyokwenda na naamini amebakiza trip mbili kwenda ataitwa Mr. Bandari. (Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna tatizo bandarini ambalo nimelifanyia utafiti baada ya kuingiwa shaka na rafiki yangu mmoja dereva wa malori ya kwenda Congo. Huyu bwana alikuwa hana tatizo, anasafiri, anaishi maisha yake akifika Dar es Salaam ana gari yake, maisha yanaendelea kama kawaida hanisumbui, lakini eventually akaanza tabia ya mizinga. Haipiti siku mbili kaniomba 20,000 nikamwambia naomba tuonane, nikamwambia umefukuzwa kazi? Kasema sijafukuzwa kazi, lakini niko bench nina miezi mitatu toka Januari sijapata mzigo kwenda Congo. Ikabidi nifuatilie kwa namna zangu, nikagundua tatizo ni kitu ambacho kimekuwa introduced bandarini kinaitwa single custom territory hususan kwa mizigo ya Congo upande wa Katanga. Sasa hili limekuwa ni tatizo kwa sababu lina taswira ya siasa za ndani ya Congo.
TAARIFA...
MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbilinyi, unapokea taarifa hiyo?
MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Hapana. Niendelee Mheshimiwa Mwenyekiti?
Mheshimiwa Mwenyekiti, sipokei taarifa yake kwa sababu naishauri Serikali hapa, Waziri Mkuu yupo pale, I am very serious kwa sababu suala lolote linaloleta impact kwenye masuala la ajira lina-affect mitaa na hii ni Serikali za Mitaa; siyo tu kuchagua tu kusimamia vyoo vya stand na kadhalika, masuala ya ajira pia TAMISEMI inahusika direct or indirect.
Kwa hiyo, tunaposimama kuchangia hapa halafu mtu anasimama anataka kupata point kwa sababu Mbunge wa Mbeya Mjini anaongea, that is wrong and very bad for the development of our country. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii single custom territory inaonekana tuliingia kisiasa kwa kuingilia siasa za ndani ya Congo katika masuala ya kukomoana. Jana mmeniona nimekaa muda mrefu na AG pale, nilikuwa najaribu kumpa hii picha kama mshauri wa Serikali ili tuangalie kwamba tunafanyaje kuondoa hili. Kwa sababu kwa kuzuia mizigo ya upande mmoja wa Congo wakati sehemu nyingine ya Congo, Kinshasa na wapi hawajakuwa affected na hii single custom territory, maana yake wale wafanyabiashara wa upande ule wa Katanga wakiona hapa panabana, wanachofanya wanahama bandari. Wamehama bandari, wameenda Beira, wameenda Mombasa; sasa hii ina-affect kwenye ajira ambayo Serikali za Mitaa watu wapo mitaani. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ina-affect namna gani? Kwa hawa wafanyabiashara kuhama na kwenda Bandari za Beira mpaka Soweto - South Africa, kinachofanyika ni kwamba hata Makampuni yetu ya clearing and forwarding ambayo yanaajiri watu around ten thousands nafikiri au kati ya 6,000 na 10,000 hawa wote ajira yao inakuwa shaken. Ajira yao inapata madhara na ndiyo sasa inakuja mpaka kwa madereva wa malori ambao wanaendesha magari ya mizigo kwenda katika maeneo hayo ya Congo. Wanapokosa mizigo ina maana wanakaa bench. Ni familia zile ambazo zinakuwa zimepata madhara kutokana na hiki kitu; halafu mtu anasimama anataka ku-interfere. Malori yakikosa kazi mama ntilie wanakosa kazi humo katika barabara zote. Watarudisha vipi hizo hela za TASAF mnazopeleka mnasema sijui VICOBA wakope; watarudisha vipi kama hizo ajira zao zinakuwa affected?
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ukiacha zile direct impact kuna indirect. Mfanyabiashara wa Congo anapokuja kuchukua container zake kumi kutoka China anachofanya, kuna viwanda vyetu local hapa vinatengeneza mafuta ya kula; sisi wenyewe si tunakula mafuta sijui ya Malaysia siku hizi tunanunua supermarket; yale local yanayotengenezwa hapa na viwanda vyetu, akina Zakaria, wale Wacongo, akifuata container zake kumi anachukua na lita kadhaa za mafuta maelfu na maelfu ya mafuta kula anapeleka Congo na michele, viungo na viazi. Utasema utakavyosema. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hawezi kwenda Beira au Mombasa kwenda kufuata container kumi halafu atoke tena kule aje Tanzania kununua mafuta ya kupikia au kuja kufuata viazi au kuja kufuata mchele. Kwa hiyo, haya mambo yana multiply effect kwa watu wetu katika masuala ya ajira. Kwa hiyo, tuangalie hii single custom territory, kwa sababu ninavyosikia katika uchunguzi wangu, ilikuwa ni katika kukomoana tu; siasa za ndani, utawala unataka kukomoa upande mwingine kwa siasa za Urais. Sisi hatutaki kuingia huko Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje unaweza ukalifuatilia hili ukaona unawashauri vipi katika maeneo hayo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, viwanda vyetu vinadoda, lakini katika biashara nyingine ndogo na za kati pia nyingi zinakufa. Kwa hiyo, wakati tunashughulika huku na big sharks wakubwa wanaoishi kama malaika na wananchi waishi kama shetani. Hawa wanaoishi huku chini wanapata anguko kubwa sana kwa kadri biashara zinavyoanguka. Nitatoa mfano mmoja, juzi nilikuwa niko safarini nakuja Dodoma, nikalala pale Morogoro kwenye hoteli ninayolala. Nitangaze interest, na mimi najaribu kuingia kwenye biashara ya hoteli msije mkasema ndiyo maana. (Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimelala katika ile hoteli, ina vyumba zaidi ya 45; nafika mimi na dereva wangu, sioni porter, nikasema porter yuko wapi? Wanasema Mheshimiwa tuna hali ngumu, hapa mnapoingia ni ninyi tu ndiyo mnalala humu ndani. Mimi na dereva wangu, nikasema kulikoni? Akasema Morogoro nzima biashara ime-shut down huduma. Sasa Morogoro ilikuwa ni eneo linalotegemea viwanda; viwanda vyote sijui Moproco, Moro Shoes vimekufa, imebaki biashara ya huduma (hospitality) kama hoteli, huduma sijui ya vyakula (restaurant), sasa vile vyote vinakufa pale Morogoro; hata hoteli ya Mzee Makamba Katibu Mstaafu,, itafungwa very soon na watageuza hosteli. Sasa huwezi kugeuza hoteli zote hosteli kwa sababu zile hoteli pia wamechukua mikopo, wale hawajajenga kwa cash, wana mikopo benki. Kwa hiyo, utakwenda ku-affect hata mabenki katika system ya mikopo. Sisi wengine tunaoenda kuchukua mikopo tutapata taabu kupata mikopo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hii yote ni kwa ajili ya nini? Eti mmefuta semina, sijui mmefuta warsha; tatizo siyo semina na warsha. Tatizo ni pale Mheshimiwa Waziri unaposahau bahasha Dar es Salaam halafu unaagiza V8 (gari) liilete na dereva na wasaidizi wanakuja Dodoma wanakaa wiki; hilo ndiyo tatizo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mnaposema hakuna warsha, hata zile zilizokuwa zinaandaliwa chini ya UNDP sijui na Mashirika mengine watu wanaogopa kuzi-implement; sasa madhara yake ni kwamba siyo tu majadiliano ya uendeshaji nchi hayafanyiki, lakini pia madhara yanakwenda kwenye huduma na moja kwa moja tunapata madhara kwenye ajira za watu wetu. Kama mfano niliotoa wa Morogoro, kwa hiyo, hili tuliangalie kidogo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la TBC halafu nawaona sana Team Lowassa wenzetu wengi tu wanavyojitahidi kunyanyuka nyanyuka, nasikia wameambiwa watashughulikiwa; sasa kila mtu akisimama anasimama na sisi, hatupumui ili kwamba ajisafishe. Kama ulibugi, umebugi tu utashughulikiwa. Maana yake kila mtu akisimama mnamtaja Lowassa leo humu. Aliwaambieni akimaliza siasa anakwenda kuchunga ng‟ombe, mnataka arudi au mnaogopa kivuli? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi niseme tu suala la TBC; haya yote niliyoyasema matatizo ya ajira na kadhalika ndiyo kinachoendelea huko chini kama hamwambii Mheshimiwa Rais. Sasa mkiacha sisi humu tuonekane tunawaongelea, wananchi wanapata relief, wanapumua. Wakipumua wanajua hili suala linaongelewa litashughulikiwa hata mkipita miaka mitano tena bila kulishughulikia lakini angalau tunawasaidia, kuwatuliza wananchi kuliko kuwaacha katika sintofahamu; hawajui ndani humu mambo yao yanayojadiliwa ni yapi, matokeo yake huko nje kutakuja kulipuka ndugu zangu. Sitaki kuchafua hali hewa kama mnavyosema. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.