Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Spika, napenda kukushukuru wewe kwa kunipatia nafasi hii ya kutoa mchango wangu katika hotuba hii ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha 2023/2024. Hii ni Wizara muhimu katika nchi yenye dhamana ya utulivu, amani na usalama.

Pili, napenda kumpongeza Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoongoza nchi yetu kwa umakini mkubwa sana na namuombea kila la kheri katika uongozi wake huu.

Mheshimiwa Spika, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Wizara hii pamoja na watendaji wake wote kwa namna walivyotayarisha hotuba hii kwa ubora wa hali ya juu na hatimaye kuiwasilisha hotuba hii katika Bunge lako tukufu kwa ufasaha na umakini mkubwa sana.

Mheshimiwa Spika, mimi katika kuchangia hotuba hii napenda kuchukua nafasi ya kuipongeza Wizara hii kwa kutekeleza kazi zake kwa utararibu mzuri. Wizara inaendelea kuimarisha amani na utulivu katika nchi yetu. Wananchi tunaishi kwa usalama, wananchi wanafanya mambo yao ya kujiletea maendeleo bila ya wasiwasi wala bughudha yoyote.

Mheshimiwa Spika, Wizara hii ni kiungo kikubwa kati ya nchi yetu na nchi jirani. Kazi hii kwa mtazamo wangu wanaifanya vizuri sana, wanaimarisha mipaka ya nchi yetu na nchi jirani. Nawaomba waendelee na kufanya kazi zao kwa mujibu wa utaratibu na sheria za nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, mimi leo mchango wangu ni kuipongeza tu Wizara hii kwa utendaji wake mzuri.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.