Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Hon. Dr. Alfred James Kimea

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Korogwe Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii na mimi kuweze kuchangia kwenye bajeti ya Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, awali ya yote napende kumpongrza Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan, ambae ndiye Amiri Jeshi Mkuu na Kiongozi mkubwa wa Majeshi haya yote, niendelee kumpongeza kwa kazi kubwa ambayo anaifanya kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa salama. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia ninatumia fursa hii kumpongeza Kiongozi wa Wizara hii Waziri wetu Mheshimiwa Innocent Bashungwa, kwa kazi kubwa ambayo anaifanya pia tumpongeze Katibu Mkuu, Ndugu yetu Dkt. Faraji Mnyepe kwa kazi kubwa ambayo anaifanya na kwa ushirikiano wake mkubwa ambao anautoa kwa Kamati na Watanzania kwa ujumla. Niwapongeza pia Majemedari na Makamanda wote ndani ya nchi hii ambao wanafanya kazi kubwa kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa salama.

Mheshimiwa Spika, nina mambo machache sana ya kuchangia leo, jambo la kwanza, jambo hili limezungumzwa na Wabunge wengi, naomba Waziri wa Fedha apate kutuambie anafanya nini juu ya suala hili la changamoto ya kikodi.

Mheshimiwa Spika, tunafahamu kazi kubwa ambayo Jeshi letu linafanya, tuwasaidie hawa watu waendelee kuifanya kazi yao vizuri kwa kuwapatia msamaha wa kodi asilimia 100. Waziri wa Fedha, akae chini na Wizara hii wapate ku–define vifaa vya kijeshi ni nini? Vifaa vya kijeshi siyo bunduki au risasi peke yake. Kitu chochote kinachoagizwa na Jeshi letu hivyo ni vifaa vya kijeshi. Hivyo, Wabunge tunaomba ndugu zetu hawa wapatiwe msamaha wa asilimia 100. Wabunge wengi wamezungumza sitaki kuongea sana kwenye detail kwa sababu najua Waziri wa Fedha atakuwa amekwishachukua atalifanyia kazi.

Mheshimiwa Spika, suala la pili, limeongelewa na ndugu yangu Chumi hapa mwisho. Hawa ndugu zetu ili kuhakikisha vifaa vyao havikai bandarini muda mrefu, wametengeneza bonded warehouse zao lakini TRA bado Inawakatilia kupeleka vifaa vyao kwenye bonded warehouse zao wakiwa wanaendelea na process za clearing.

Mheshimiwa Spika, tunaomba watu wa TRA waweze kutoa go ahead Jeshi letu likapate kutumia bonded warehouse zao kuhifadhi mizigo yao wakiwa wanafanya process za kufanya clearing. Vifaa vyao kukaa kwa muda mrefu pale kwanza ni aibu kwa Taifa letu, kwa watu ambao wanajitoa kwa Taifa hili kuweza kuzuia mizigo yao halafu iko pale bandarini.

Mheshimiwa Spika, mwisho, muda mwingine huwa hatufahamu wanaagiza vitu gani kwa matumizi gani? Siku moja tutakuja kukimbiana pale bandarini inawezekana kuna vitu havistahili kukaa kwa muda mrefu pale kwenye bandari yetu, waruhusuni watu hawa kwa kuwa ni ngumu kuweza kumwelezea kila mtu kitu gani kiko kwenye ma - container yao kwa ajili ya issue za kiusalama, waruhusiwe wawe na bonded warehouse zao vifaa vyao vikija vyote vihifadhiwe huko kama mnataka watu wenu wa TRA wawe huko clearing ifanyike vifaa vyao vikiwa kwenye maghala yao na siyo ndani ya bandari yetu pia itapunguzia mzigo bandari yetu ambayo tunataka iwe ya kisasa na ihudumie mambo mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwenye suala la kikodi ninaamini kabisa Waziri wa Fedha leo katika kuhitimisha ataliongelea suala hili na atatuhakikishia kwamba moja, kutakuwa na msamaha wa asilimia 100 lakini pili, wataruhusu Jeshi letu liweke vifaa kwenye bonded warehouse zao. Hivyo ni vitu viwili ambavyo nilitaka kuchangia.

Mheshimiwa Spika, jambo la mwisho pia limeongelewa na watu wengi ni Shirika la Nyumbu. Naomba niongelee kwa uchache Shirika hili la Nyumbu. Kwanza, napenda kuipongeza Serikali hasa viongozi wetu waasisi wa Taifa hili kwa kuwa na maono haya makubwa ya kuwa na shirika hili. Nahisi watu wengi hawafahamu ndoto za Rais wetu wa Kwanza kuanziasha shirika hili. Alikuwa anatamani siku moja Tanzania iwe inajitosheleza kwenye masuala ya magari, vifaa vya kijeshi, kila kitu kifanyike ndani ya nchi yetu, lakini changamoto ya Serikali yetu baada ya hapo hatukuwa committed kwenye shirika lile. Ninaiomba Serikali iwe Committed ili shirika hili liende mbali zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda kuwapongeza viongozi wa Shirika hili. Shirika hili limejiongezea uwezo mkubwa sana, ukifika pale utaona mambo makubwa ambayo yanafanywa kwenye shirika lile. Wanatengeneza magari ya Kijeshi, wanatengeneza magari ya zima moto, wanatengeneza vifaa vya nyumbani, majiko na vitu vingine lakini kikubwa zaidi wanatengeneza hadi vifaa vya kilimo ambapo nchi yetu inatamani kupeleka suala la kilimo mbali zaidi.

Mheshimiwa Spika, Serikali iwe committed iwapeleke fedha mimi ninaamini kabisa nchi yetu itafika mbali sana tukiamua kuwekeza kwenye shirika hili. (Makofi)

MHE. ALI JUMA MOHAMED: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Nani mtoa taarifa? Mheshimiwa Ali Mohamed.

TAARIFA

MHE. ALI JUMA MOHAMED: Mheshimiwa Spika, napenda nimpe taarifa mchangiaji anaeendelea kwamba licha ya changamoto mbalimbali na mafanikio ambayo yanatokea nchini kutokana na Jeshi letu, lakini Jeshi letu limekuwa likiijengea sifa sana nchi yetu ya Tanzania hasa pale linaposhiriki katika mission mbalimbali za Kimataifa. Hii imepelekea kupata sifa kwenye Jumuiya ya Kimataifa, sasa ikiwa Jumuiya ya Kimataifa inathamini sana Jeshi letu, kwa nini Serikali yetu ishindwe kutoa uwezo wa kifedha kwa ajili ya Jeshi letu? (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Kimea, unaipokea taarifa hiyo?

MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA: Mheshimiwa Spika, ninaipokea taarifa kwa mikono yote miwili. Kwa hiyo, ninachotaka kusisitiza hapa Serikali yetu iwe committed kwenye shirika hili ninaamini kabisa tutaenda mbali.

Mheshimiwa Spika, tukiamua kwenye nchi hii kwamba: (i) Magari yote ya zima moto yasiagizwe kutoka nje ya nchi, yatengenezwe kwenye shirika hili. (ii)Magari yote ya kuzolea taka kwenye nchi yetu yaagizwe kutoka kwenye shirika hili. Tukisema ambulance zote zitengenezwe kwenye shirika hili, magari ya Majeshi yetu ya Jeshi la Polisi, Magereza yote yaagizwe toka shirika hili, ninaamini shirika linao uwezo, tumetembelea pale tumeona, tukiamua ku - invest pale ninaamini watatengeneza vitu kwa ajili ya nchi yetu na tutaweza kuuza hata nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, hivyo, ninaiomba Serikali iweze kulipatia fedha shirika hili nina amini kabisa katika uchumi wa nchi yetu kwanza litatengeneza ajira nyingi sana.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa na hayo machache ya kuchangia. Ninapenda kuunga mkono hoja hii na tupo pamoja Wanakamati tutaendelea kushirikiana nao. Ahsante sana kwa kunipa muda huu. (Makofi)