Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

Hon. Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuchangia kwenye hoja hii iliyoko mezani ya Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara. Nina mambo matatu wakati Mheshimiwa Elibariki Kingu anachangia kuhusu mafanikio ya Mheshimiwa Rais kwenye Uwekezaji wa Sukari na hili waweze kutambua Watanzania ni kwa mara ya kwanza wakati wote wa Ramadhan hatujaona sukari ikihadimika. Hili ni jambo kubwa sana ambalo Mheshimiwa Rais amelisimamia la Mfungo wa Ramadhan umeenda vizuri hakujakuwepo na kelele yeyote kuhusu sukari. Kwa hiyo, ninaunga sana haya maelezo ambayo ameyatoa Mheshimiwa Kingu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mambo matatu jambo la kwanza ni jambo la lumbesa Mheshimiwa Waziri ni muhanga mkubwa sana wa changamoto ya lumbesa na ninavyozungumza saa hizi Wananchi wa Makete na Mikoa mbali mbali nchini yawezekana wanaweza wakawa na nyota ya nuru na ya matumaini kwamba labda Serikali inaweza ikatoa mwanga kuhusu suala la lumbesa kwenye Taifa letu. Mheshimiwa Waziri mimi nitahitaji kushika shilingi kwa sababu gani? ukikaa na Mheshimiwa Bashe anakwambia suala la lumbesa ni suala la Wizara ya Viwanda na Biashara na unakuta ana asilimia mia moja ni sahihi kwa sababu nyie ndiyo watu wa vipimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taifa letu la Tanzania ndiyo Taifa pekee ambalo tunapima mtu kwa kumkadiria kwamba gunia likifika kiwango hiki ndiyo limetimia gunia moja. Ukienda Kenya, ukienda East Africa zote nchi hakuna utaratibu wa kupima kwa kumkadiria mtu kwamba kwa kimo hiki ndiyo gunia la vitunguu limetosha pale Singida, kwa kimo hiki gunia la vitunguu limetosha pale Iringa na kwa kimo hiki viazi gunia limetosha. Mheshimiwa Waziri it’s a high time now tuchukue nafasi ya ku–introduce vipimo kwenye upimaji wa mazao yote nchini kwa sababu gani? Suala la lumbesa is a mindset mtu anadhani gunia likiwa limefungwa kile kilemba cha juu ndiyo lumbesa kumbe hicho hicho kilemba ukienda kuweka kwenye mizani yawezekana hakijafika gunia la kilo mia moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu concept ni hii kilo mia ndiyo sawa sawa na gunia moja hasa wakulima tuwatoe kwenye hili ombwe lakudhani kila kitu ni lumbesa tu–introduce vipimo Mheshimiwa Waziri una nafasi ya kukaa na Tamisemi kuna selling points maeneo tofauti tofauti kwenye Kata zetu, kwenye Vijiji vyetu wekeni mizani wakulima wasiibiwe na mfanyabiashara asiibiwe ili concept ya mind set ya suala la lumbesa iweze kufa kwenye Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri ninakuomba sana sana sisi Watu wa Makete navyo zungumza saa hizi wakulima kule, wafanyabiashara wanagombana na halmashauri ni lumbesa lumbesa sasa haieleweki yupi anaibiwa? yupi haibiwi? haieleweki kwa sababu gani? Hakuna mizani ya kupima concept yetu ni ile ile mbona sukari mnapima kwenye kilo? Mbona unga mnapima kwenye kilo? Mbona nyama mnapima kwenye kilo? Na hata parachichi nilisema limeanza na mguu mzuri linapimwa kwenye kilo. Ingekuwa parachichi haliuzwi kwenye kilo ingeleta matatizo makubwa kwenye Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba sana Wizara kesho mnavyokuja kutusaidia kufunga hoja mtupe majibu suala la lumbesa kwenye taifa letu hili Wananchi wangu wa Matamba, Wananchi wangu wa Makete, Wananchi wangu wa Kinyika waweze kupata suluhisho la suala la changamoto la lumbesa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo langu la pili kwa Mheshimiwa Waziri wakati nazungumza hapa kuna suala la Kariakoo nimesoma nimepitia Hotuba yako yote swali langu moja tu nataka nijiulize Wafanyabiashara wa Kariakoo anae watetea ni nani kwenye nchi hii? kwa sababu nimepita kwenye Hotuba yako sijaona chochote kinacho zungumzwa Kariakoo is our own Dubai. Kariakoo ndiyo Dubai ya Taifa letu na ndiyo iko chini ya Wizara yako, iko chini ya Wizara ya Fedha, iko chini ya Wizara nyingi tu ni Mpango gani Mkakati wa Serikali yetu kuhakikisha wanazidi kuinusuru Kariakoo? Kwa sababu kiuhalisia Mheshimiwa Waziri Kariakoo inazama hilo ndiyo ukweli ulioko wazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nenda kaangalie floo ya wafanyabiashara wa kigeni Kariakoo imepungua kwa asilimia zaidi thelathini zaidi ya asilimia arobaini kwanini wamepungua? Mheshimiwa Waziri ni vyema mkaenda mkafanya vikao na wafanyabiashara Kariakoo mkakubaliana ni nini kifanyike ili Kariakoo kama Dubai yetu iweze kuinua, ili kama Kariakoo Dubai yetu isizame saa hizi Kariakoo is moving to Uganda Kampala, Kariakoo now is moving to Lusaka, Kariakoo now is moving to Lilongwe biashara sasa watanzania imegeukia kwenda kwenye mataifa ya Jirani. Tumefungua milango kwenye mataifa ya Jirani ndiyo tukafate bidhaa wakati sisi ndiyo tulikuwa tunalisha East Africa nzima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii bidhaa nyingi tunachukua kutoka kwenye mataifa ya East Africa wapi tumekwama kama Taifa? Kama Mawaziri ninawaomba sana jisikieni uchungu kuona Kariakoo inazama kama kuna changamoto za kikodi kama Mbunge nashauri kaeni na Wizara ya Fedha, kaeni na TRA mjue jinsi gani mnaweza mkainusuru Kariakoo na changamoto za kikodi Kariakoo ikatengama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii unakaa na mfanyabiashara anasema naenda kufata shuka Uganda, naenda kufata mizigo Uganda why Uganda and not Kariakoo there is a problem tunaomba Mheshimiwa Waziri iangalie Karikoo kwa jicho la karibu kwa sababu utasema mbona unaizungumzia Karikoo tu kwanini uzungumzii Arusha? Kwanini uzungumzii Mbeya? Sisi Kariakoo kwa maana Kariakoo ndiyo inalisha Arusha, ndiyo inayo Ilisha Mbeya lile ndiyo shamba kubwa linalolisha Taifa letu ni lazima na ninyi muichukue hii kama Dubai yetu mkaiangalia kwa mtazamo wa karibu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wafanyabiashara wamepungua nenda Msimbazi Post, nenda central utakuta wafanyabiashara wa Kikongo, wafanyabiashara wa Nigeria wamekamatwa pale. Kama umekamata risiti ya mzigo iko hovyo deal na yule aliyetoa ile risiti ni nani usi-deal na wafanyabiashara wa kigeni. Ukimwi- intimidate huyu unazuia kesho kurudi, keshokutwa anatafuta njia nyingine ya kwenda. Tunakuomba sana Mheshimiwa Waziri ucheki Kariakoo kwa jicho la karibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo langu la mwisho ni kuhusu uwekezaji kwenye Mkoa wa Njombe. Mheshimiwa Waziri ninakuomba sana, suala la Liganga na Mchuchuma, na kwenye hotuba yako hapo ukipitia umezungumzia Liganga na Mchuchuma unasema hivi, matumizi ya chuma nchini yameongezeka kutoka tani 226,000 hadi tani 1,000,000; tangu nimezaliwa inazungumzwa Liganga na Mchuchuma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna miradi ya SGR, tuna miradi ya Bwawa la Mwalimu Nyerere, na uzuri SGR sio kwamba imekomea hapa, inaendelea. Hii miradi yote inayotumia chuma. Tunaomba Mheshimiwa Waziri Liganga na Mchuchuma ianze kufanya kazi ili tuweze kunusuru Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, nilikufuata kwenye meza yako nikakuomba; sisi Makete tuna wheather ambayo inaweza kuzalisha mianzi kwa ajili yakutengeneza toothpick lakini leo hii toothpick zinatoka China. Ninaomba kwa fursa ambayo unayo usi-concentrate sana kwenye coastal zone corridor kwenye uwekezaji. Kuna huku pembezoni mwa nchi kama Makete kuna sehemu nzuri ambazo unaweza ukawekeza na ukalisaidia Taifa letu kwenye maeneo ya kilimo na viwanda mbalimbali. Tunaomba sana utembelee kwenye maeneo yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo mimi sina mambo mengi sana ni hayo mambo yangu matatu, Mheshimiwa Mungu akubariki na ahsanteni sana. (Makofi)