Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Kilimo

Hon. Dr. Alfred James Kimea

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Korogwe Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Kilimo

MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia kwenye Wizara hii, lakini kabla nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa uhai na nguvu. Pia niungane na wenzangu kumshukuru Rais wetu, Mama Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo nchini kwetu. Kwa kipekee pia niwashukuru Mawaziri wetu, ndugu yangu Bashe pamoja na kaka Anthony kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya kuendeleza Sekta hii ya Kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na muda nina mambo mawili tu ambayo nataka kuchangia leo. La kwanza, ni skimu za umwagiliaji; kwenye Jimbo langu la Korogwe Mjini nina skimu tatu za umwagiliaji. Skimu hizo ni Mahenge, Gou pamoja na Kwamgumi. Kimsingi Jimbo langu ni kati ya majimbo ya mjini wengi tunajishughulisha na biashara, kilimo siyo sana kwa hiyo skimu hizi ni skimu ambazo tunazitegemea kwa kiasi kikubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, skimu hizi zimekuwa na matatizo kwa muda mrefu, watu hasa wa Mahenge na Goho ambao wapo kwenye Kata ya Kwamndolo wamekuwa wakilima mara nyingi mpunga lakini wanapata mafuriko, kwenye miaka mitano tumepata mafuriko zaidi ya mara tatu, nguvu zote walizozitumia kuandaa mashamba hadi wanakaribia kuvuna mafuriko yanakuja mpunga ule unakwenda na maji wote, kwa hiyo ni hasara kubwa wanaipata, kwa juhudi kubwa ambazo wanaziweka kuleta chakula ambacho kinalisha Taifa hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana niliiomba Wizara hii na ilinikubalia kwamba itaenda kutujengea skimu zetu, wakasema wataanza na skimu ya Mahenge. Tarehe 5 Julai, 2021 ilitoka list ya skimu ambazo zitaenda kufanyiwa kazi mwaka huu tulionao wa fedha na Mahenge ikiwa skimu Namba Nne kwenye hiyo list, lakini jambo la kushangaza juzi wametoa list ya skimu ambazo zinaenda kufanyiwa kazi na skimu yangu ya Mahenge haipo. Hili jambo limesikitisha sana wananchi wangu pia limenisikitisha mimi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu gani kimetokea tuliambiwa tunaenda kujengewa skimu ile, nilienda nyumbani Jimboni kwangu nikawatangazia wananchi kwamba hasara sasa ni basi, Serikali imepanga kujenga skimu hizo na tunasubiri fedha kwa mshangao mkubwa list inatoka ya skimu za…

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa Mheshimiwa Timotheo Mnzava.

T A A R I F A

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naomba nimpe mzungumzaji taarifa kwamba siyo skimu ya Mahenge tu hata skimu ya Kwamkumbo na ipo barua ya commitment ya Wizara na Tume ya Umwagiliaji kuwa skimu za Mahenge na Kwamkumbo lakini kwenye tangazo la zabuni hazipo, naomba nimpe taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Kimea unaipokea taarifa.

MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mikono yangu yote miwili napokea taarifa ya Mheshimiwa Timotheo Mnzava, Mbunge jirani wa Korogwe vijijini. Kimsingi ninajua jitihada kubwa za Kaka yangu Mheshimiwa Bashe, nafamu ni rafiki yangu sana na yeye anafahamu lakini najua jitihada za Ndugu yangu Mheshimiwa Antony najua wanafanya kazi kubwa, lakini kwa hili kesho ninatarajia kushika SShilingi hadi watuhakikishie na watupe majibu kamili kitu gani kinaenda kufanyika. Maana siwezi tena kwenda kurudi Jimboni kwangu mwaka jana niliwaambia inatekelezwa sasa ninawaambia nini, kwamba Serikali haina fedha wakati mwaka jana kulikuwa na list ya skimu 10, mwaka huu zimeletwa list ya skimu 13 za kutengenezwa ya kwangu haipo narudi nawaambia kitu gani wananchi wa Korogwe? Kwa hiyo ninatoa taarifa kwamba kesho nitashika Shilingi mpaka nitakapohakikishiwa siyo ahadi kuhakikishiwa kwamba skimu ya Mahenge itawekwa kwenye list na wananchi wangu wa Mahenge wataenda kujengewa skimu mwaka huu, ninashukuru kwa hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili na la mwisho ambayo ninapenda kuchangia, kilimo kwenye nchi hii, vijana wanatakiwa kuji-engage sana kwenye kilimo lakini changamoto kubwa inayowakumba vijana pia wananchi wetu wa vijijini ni ukosefu wa fedha mitaji, benki zetu zimekuwa haziwezi kukopesha vijana kwa ajili ya kutokuwa na vigezo hasa dhamana. Ninashauri Wizara yetu ianzishe mfuko ambao utakuwa na kazi kubwa mbili. Kazi ya kwanza kusimama kama dhamana hasa kwa vijana wetu wanaomaliza shule, wanaotaka kujiingiza kwenye kilimo hawawezi

kukopesheka kwa hiyo mfuko huo usimame kama dhamana ili waweze kukopeshwa. Pia Wizara imefanya kazi Serikali imefanya kazi kuomba benki nyingi kupunguza riba lakini baadhi ya Benki bado riba ipo juu, kwa hiyo huu mfuko pia utumike kama sehemu ya kupunguza riba, kama benki inakopesha asilimia 10 tunataka vijana wetu wakopeshwe kwa asilimia saba ili asilimia mbili mfuko huu ufanye kazi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona nchi nyingi zimefanya hivyo nikikutolea mfano nchi ya Ghana ina mfuko huo ambao moja unasimama kama dhamana kwa ajili ya wakopeshwaji lakini namba mbili ku-reduce interest rate endapo benki itakuwa willing kukopesha wakulima lakini interest rate zipo juu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu ni hayo mawili, lakini kikubwa sana ni skimu yangu ya Mahenge, kesho nitashika Shilingi endapo hili halitajibiwa, siyo kujibiwa tu Waziri aje na commitment kwamba skimu ya Mahenge itaenda kufanyiwa kazi mwaka huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana na Mungu awabariki, ahsante. (Makofi)