Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maji

Hon. Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maji

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, awali ya yote ninamshukuru Mungu, kwa zawadi ya uhai na amani katika nchi yetu ya Tanzania.

Mheshimiwa Spika, ninampongeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi za kumtua mwanamke ndoo kichwani, na ninahimiza kazi iendelee. Pia pongezi kwa Waziri Mheshimiwa Aweso na timu yake yote, kwa utekelezaji wa viwango vya hali ya juu sana.

Mheshimiwa Spika, naomba kufikisha kilio cha wananchi wa Same, Mkoani Kilimanjaro. Mradi wa kimkakati wa Mwanga, Same, Korogwe umekuwa hadithi ya abunuasi. Ninamwomba Mheshimiwa Waziri atakapokuwa anahitimisha aseme neno moja tu kuhusu mradi ya hapo juu na roho za wananchi husika hapo juu zitapata amani.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.