Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa spika, nakushuku kwa kinipatia fursa hii ya kutoa mchango wangu katika hotuba hii ya makadirio na mapato ya Wizara ya Elimiu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Mheshimiwa Spika, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na watendaji wake wote kwa kutayarisha na hatimaye kuiwakilisha hotuba hii katika Bunge lako tukufu kwa ufasaha na umakini mkubwa.

Mheshimiwa Spika, katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo; vyuo vya VETA.

Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali yetu inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kupia Wizara hii kwa kuendeleza utararibu mzuri juu ya uendeshaji wa vyuo hivi katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, vyuo vya VETA ni mwanzo mzuri wa kuwanoa na kuwapa matumaini juu ya hatima ya wanafunzi kimaisha. Lakini inaonekana kuwa baadhi ya masomo yanayofundishwa kwenye vyuo hivi hayawapi matumaini hayo wanafunzi. Madhumuni makuu ya kusoma baada ya kusoma ni kuweza kujikimu maisha yake aidha kwa kuajiriwa au kwa kujiajiri mwenyewe. Lakini bado lengo hili hafikiwi kutokana na nature ya course husika.

Ushauri wangu katika jambo hili kwa Serikali ni kuweka masomo ambayo yatakuwa rahisi kuwasaidia vijana wetu kupata ajira.

Pili ni kuhusu mikopo ya wanafunzi; napenda kuipongeza Serikali kwa kuweka mpango huu mzuri wa kuwakopesha vijana wetu ili waweze kutimiza ndoto zao za kimaisha.

Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa suala hili napenda kuishauri kwa Serikali mambo yafuatayo: -

(a) Serikali irekebishe vigezo vya kupata mikopo hiyo.

(b) Kuongeza kima cha fedha ili waweze kukopeshwa wanafunzi wengi zaidi.

(c) Wanafunzi wanaosoma elimu ya kati pia nao wapate fursa ya mikopo.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.