Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

Hon. Bakar Hamad Bakar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

MHE. BAKAR HAMAD BAKAR: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii na mimi niweze kuchangia hotuba hii ya bajeti ya Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri na Naibu wake pamoja na timu yake nzima ikiongozwa na Katibu Mkuu na Naibu Makatibu Wakuu wote watatu. Tanzania ni miongoni mwa nchi chache ambazo zimebarikiwa na rasilimali nyingi mno, lakini rasilimali hizi tulizonazo bila ya kuweza kuzitangaza kwa nchi mbalimbali na zikajulikana duniani hatuwezi kufikia malengo na kuweza kuzitumia kwa maslahi ya Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ziara ambazo anazifanya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama yetu Mama Samia Suluhu Hassan, pamoja na kujenga uhusiano mzuri, ziara hizi kati yetu na nchi hizo ambazo anazitembelea lakini pia zinalengo la kutangaza rasilimali zetu kwa ajili ya maslahi ya Taifa letu kupata fursa za uwekezaji, lakini pia kwa kuangalia sana kwa watu wetu wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunazo fursa nyingi zikiwemo bahari, maziwa lakini tunayo ardhi, tunavyo visiwa mbalimbali vingi sana bila vitu hivi kuvitangaza haviwezi kujulikana na haviwezi kuonekana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi leo nitazungumzia zaidi kwenye suala la uwekezaji; bado pamoja na mama kwenda na kufanya ziara hizi mbalimbali zenye lengo hili la kuzitangaza rasilimali zetu, tunazo changamoto za fursa au zenye kujenga mazingira rafiki kwa wawekezaji ili kuweza kupata fursa hizo kuja hapa. Tunayo changamoto ya urasimu kwa maana ya bureaucracy, bado jambo hili ni changamoto kubwa sana kwa nchi yetu. Endapo tutatatua changamoto hii ninaamini ile kazi ambayo anaifanya mama basi inaweza ikawa rahisi sana kupata wawekezaji wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia tuna changamoto ya rushwa, bado rushwa ni tatizo kwa nchi yetu endapo pia tutatatua changamoto hii, tutaweza kuweka mazingira rafiki sana kwa wawekezaji wa ndani na wawekezaji wa nje.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna changamoto nyingine ambayo tulisema ni political stability, ili nchi yoyote iweze kuvutia watalii na kuweza kuvutia wawekezaji ni lazima kuwe na stability ya political. Tunashukuru sana kwa nchi yetu kwa sasa hivi amani na utulivu ambayo ipo ni jambo la kuweza kupongezwa na kuungwa mkono. (Makofi)

Niwaombe sana Watanzania niwaombe sana wanasiasa tuendelee kuidumisha amani tuliyonayo, tukiidumisha amani hii ndio ambayo tutawahakikishia wawekezaji kuja nchini na kuweza kuwekeza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna changamoto nyingine ambayo ni miundombinu ambayo bado miundombinu tulizonazo sio Rafiki, ukiangalia barabara zetu bado sio rafiki kwa wawekezaji, ukiangalia umeme, maji na miundombinu mingine. Tukiweza kurekebisha kwenye maeneo haya ya miundombinu ninaamini kwamba wawekezaji watakapokuja na watakapoona kwamba tumeweka sawa kwenye suala la miundombinu, ninaamini kwamba tutaongeza wawekezaji wengi sana wa nje na kuja kuwekeza katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu kwanza ni wakati sasa wa kuweza kuanzisha system (mifumo mbalimbali) itakayoondoa hivi vikwazo, hizi nenda rudi za wawekezaji, kuwarahisishia wao hizi njia za kuweza kupata vibali, lakini njia za kuweza kuona hizo fursa zinazopatikana katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia sheria tulizonazo ni wakati wa kufanya marekebisho ya sheria ili sheria hizi ziwe na fursa nzuri na ziwe na maslahi mapana kwa wananchi wetu, kwa nchi yetu lakini pia ziwe na maslahi mapana kwa wawekezaji ambao wanawekeza hapa nchini kwetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia FDI inflow ya trend ya Africa kwa sasa Tanzania ni kama vile haionekani. Unaona nchi kama Egypt, unaona nchi kama South Africa, unaona kama Nigeria, Congo, unaziona hizo kwenye suala hili la Foreign Direct Investment (FDI), sisi bado tuko chini sana. Ni wakati wa kupiga hatua kuondoka hapa tulipo na kuelekea huko mbele zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mara baada ya kusema hayo niunge mkono hoja hii, ahsante sana nakushukuru. (Makofi)