Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira

Hon. Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Spika, katika Wizara hii naomba kuchangia kama ifuatavyo; kwanza Wizara inatakiwa kuangalia uwezekano wa namna ya kunufaika na miradi ya kupunguza hewa ya ukaa iliyopo duniani ambayo wapo baadhi ya wawekezaji wameanza kuwekeza nchini, tunayo misitu ya asili mingi ambayo kwa maoni yangu inakidhi vigezo vya kulipwa fidia.

Mheshimiwa Spika, pili, kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya Wilaya zenye vyanzo vingi vya maji kama Wilaya ya Kilolo ili kuendelea kulinda vyanzo hivyo na kuwa na njia mbadala za kiuchumi ambazo ni rafiki kwa mazingira.