Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Hon. Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na suala la usaili wa ajira (interview).

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nampongeza Mheshimiwa Jenista Mhagama, Waziri, Naibu Waziri na timu nzima kutoka Wizarani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hii kuwasilisha mchango wangu kuhusiana na usumbufu wanaopata vijana wengi wanapoomba nafasi za ajira na kuitwa kwenye usaili ambapo idadi inayoitwa ni kubwa kuliko idadi inayotakiwa. Mfano idadi ya vijana wanaoitwa inaweza kuwa 5,000 wakati wanaotaka kuajiriwa ni robo ya hao tu. Hii si sahihi kwa kuwa vijana wengi wamekuwa wakitumia gharama kubwa huku ikijulikana wazi hawawezi kuajiriwa. Hivyo inawakatisha tamaa na kuwapa umaskini walezi wa vijana hao kwa gharama wanazotumia kuhudhuria usaili na kurejea bila chochote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kujua pia kama ajira mpya zinazingatia jinsia kwa maana ya wanawake na wanaume katika nafasi zinazotangazwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo naona ni wakati muafaka baadhi ya taasisi kama TRA, Bunge na Mahakama kupewa mamlaka ya kuajiri kama ilivyokuwa awali kwa kuzingatia mahitaji hivyo kuupunguzia mzigo Wizara. Naomba kuwasilisha.