Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Hon. Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Na mimi niungane na wezangu kuwapongeza sana Mawaziri, ndugu yangu dada yangu Jenista pamoja na Naibu wake; jina lake la Kigogo ni gumu samahani sana. Niwapongeze kwa kazi nzuri nipo kwenye hiyo Kamati, kwa hiyo niwapengeze kwanza…

SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Thea Ntara, anaitwa Deogratius Ndejembi; kwa hiyo unaweza ukamwita Deo.

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nikupongeze sana Mheshimiwa Deo kwa kazi nzuri unayofanya kwa kusaidiana na Mheshimiwa Jenista. Kwanza niwapongeze hasa kwa usikivu tukiwa kwenye Kamati. Ni Mawaziri wasikivu sana, maoni yetu mengi waliyachukua kwa uzito waliostahili.

Mheshimiwa Spika, mimi nianze na suala moja ambalo tulizungumza kwenye Kamati na mlitoa ahadi; kuhusu harmonization ya mishahara kati ya wahadhiri na waendeshaji.

Mheshimiwa Spika, Katibu Mkuu alitoa ushahidi kwamba hilo suala tayari wanalifanyia kazi. Sasa mimi niseme tu, liamenza muda mrefu, na mnasema hao watu walikuja kuwaona; hebu niombe sasa mlifanyie kazi ili huko kwenye vyuo watu wafanya kazi kwa upendo. Nililisema, maana unakuta mhadhiri ana master na mwendeshaji ana masters lakini mishahara yao inakuwa tofauti mno kiasi kwamba ikapelekea watu kudharahuliana au kujengeana chuki. Kwa hiyo ni vizuri mkaangalia hilo suala lifike wakati sasa liishe.

Mheshimiwa Spika, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya hawa ni watumishi. Kwa muda mrefu wamekuwa wakipata political fund ya milioni tano ambayo ni ndogo sana. Mimi nilikuwa Mkuu wa Wilaya, hiyo milioni tano nilikuwa ninaiona; na Wakuu wa Mikoa milioni 20. Sasa ni muda mrefu Mkuu wa Wilaya au Mkuu wa Mkoa anakwenda na hicho kiwango.

Mheshimiwa Spika, mimi niwaombe wakae pamoja na TAMISEMI kuangalia kiwango cha huyu mtumishi kiwe angalau kipande. Mkuu wa Wilaya anakwenda mahali kwenye harambee huku hana hela, unakuta anatoa mia tano, mia tatu; na hiyo inawafanya wanaonekana wanyonge. Mkuu wa Mkoa anakwenda mahali anashindwa hata kutoa milioni moja. Sasa sijui Waheshimiwa Mawaziri political fund yao ni kiasi gani; lakini ningeomba hili litazamwe mkishirikiana pamoja na TAMISEMI kuona kwamba kwamba ifikie wakati sasa kile kwango kiongezeke. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kingine nipongeze sana kazi waliyoifanya wala CAG kama alivyosema Prof. Mkumbo. CAG walifanya kazi nzuri sana kuangalia idadi ya watumishi katika shule za msingi. Sasa ile asilimia 41 ya upungufu ni kubwa mno. Kwa hiyo, cha kufanya hapa sasa ni kuangalia namna gani hao CAG nao waende kwenye vyuo, na wakifika kwenye vyuo nako watoe hizi takwimu za upungufu wa watumishi. Sasa CAG akienda kwenye vyuo yeye anangaalia tu mambo ya consultancy; ajue vyuo na shule kazi yao ni ufundishaji na kujifunza. Kwa hiyo a-base kwenye kukagua vitu vinavyohusiana na ufundishaji na kujifunza. Kwa mfano anaenda pale Ardhi ili tujue watumishi wa pale ardhi wamepungua wangapi? Anacheki workshops zao zikoje, anacheki maabara; hivyo ndiyo vitu anatakiwa CAG atuambie ili tujue kabisa upungufu wa vituo hivyo katika vyuo vikuu na vyuo vya kati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine, niwaombe Ofisi ya Utumishi kule Hai Mkoani Kilimanjaro tayari wametenga eneo la kujenga Chuo cha Utumishi wa Umma na wametenga muda mrefu. Sasa, niwaombe Ofisi ya Utumishi, lichukueni hilo Mheshimiwa Waziri ili muone kama mnaweza kuanza angalau na zile process za mwanzo, kwasababu ni muda mrefu hilo eneo limetengwa. Bahati nzuri kwenye kamati tuliwaambia mimi naona ingependeza kama mtalichukua hilo na kuona kwamba tunaongeza idadi ya vyuo vya utumishi kwa kuwasaidia watumishi kupata elimu na pia kuongeza vyuo vya aina hiyo katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, mimi baada ya hapo nikushukuru sana kwa leo naishia hapo. Ahsante sana. (Makofi)