Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022, Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022

Hon. Stanslaus Shing'oma Mabula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyamagana

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022, Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022

MHE. STANSLAUS S. MABULA - MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninakushukuru na ninaseme ahsante kwa fursa hii, nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wote kwa kuisikiliza taarifa ya mwaka ya Kamati na ninatambua michango ya Wabunge mmoja mmoja kwenye hoja za Kamati na kwa kuwataja wachache ni kama ifuatavyo; Mheshimiwa Ng’wasi Damas Kamani, Mheshimiwa Francis K. Ndulane, Mheshimiwa Jeremiah M. Amsabi, Mheshimiwa Issa Ally Mchungahela, Mheshimiwa Jesca J. Msambatavangu; na Mheshimiwa Mwita M. Waitara.

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge wameonesha namna ubadhilifu wa fedha za umma unavyofanyika katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, wameonyesha kuwepo kwa upotevu wa fedha za umma katika mifumo ya kielektroniki ya mapato, manunuzi, mikataba na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati zinapokuwa zimepokea taarifa ya Mkaguzi ya CAG maana yake ni kwamba taarifa hii imepitia hatua nyingi sana ikiwemo kuzipa fursa Halmashauri ya kujibu hoja ambazo zimejitokeza wakati wa ukaguzi. Hoja wanapewa zaidi ya siku 21 wakati mwingine ili waweze kuzitolea majibu, inaposhindikana kabisa majibu yake hakuna bado wanapata nafasi na CAG anapokwenda anakuwa na vikao mbalimbali, kikao cha kwanza, anachofanya wakati anaingia lakini kunakuwa na kikao cha pili ambacho sasa kina mpa nafasi ya kuendelea na kazi yake, hata anapomaliza ndani ya siku 30 alizopewa bado atafanya exit meeting ambayo ataeleza kwenye eneo husika nini alichokutana nacho na atawaachia nafasi ya kujibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kinachojitokeza Halmashauri nyingi hazitoi majibu kwa wakati na hazitoi vielelezo vya maswali magumu waliyoulizwa na Mkaguzi. Lakini bado wanapata nafasi ya kuja mbele ya Bunge lako kwa maana ya Kamati ili waweze kuelezea na Bunge lako linatumia nafasi hiyo kuhoji likimhoji pande zote mbili kwa maana ya CAG lakini linawahoji pia watu waliokaguliwa, bado taarifa na majibu ya hoja zlilizotolewa hayapatikani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo maana taarifa zinazoingia hapa ndani kwenye bunge lako tunaamini ni taarifa zilizotenda haki kwa pande zote mbili na ni imani yetu kwamba Wakurugenzi na Watendaji Maafisa Masuuli wakifanya wajibu wao sawasawa inawezekana kabisa hoja hizi zikapungua sana na hizi sintofahamu, hii ni kweli au siyo kweli ikawa imeonekana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ujumla Waheshimiwa Wabunge wamehimiza Serikali kuchukua hatua madhubuti dhidi ya ubadhirifu huo. Aidha Waheshimiwa Wabunge wameshauri Serikali kuzingatia utaalam katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Michango hii imeimarisha zaidi mapendekezo ya Kamati katika taarifa yake ya mwaka 2023.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninahitimisha kwa kauli kwamba ubadhirifu katika mapato na matumizi ya fedha za umma ni jambo lisilostahili kufumbiwa macho, hivyo nalishawishi Bunge lako tukufu liunge mkono mapendekezo ya Kamati kuwa Maazimio ya Bunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kufanya hivi tutasaidia sana iko mifano mingi kwa mfano, unakutana na hoja ya ukaguzi ambayo Mkaguzi amekuta Halmashauri Mtumishi aliyepaswa kulipa kwa mfano analipa Shilingi Laki Nne badala ya kulipa Shilingi Laki Nne anasema akaingiza namba ya simu ambayo tarakimu zake uki-count kwenye hela inakuwa, kwa mfano anaingiza namba 068… and so on, ambayo ukichukua 068 unatoa sifuri unazungumzia Milioni Mia Sita. Sasa cha kujiuliza kama yalikuwa ni makosa fedha hii imeingia kwenye account ya benki, baada ya masaa machache yaliyofuata fedha ile ile ya namba imeenda kutolewa benki kama cash money na kwenda sehemu ambayo haijulikani. Hizi ni moja ya changamoto ambazo ukweli zinaonyesha kabisa yako maeneo ambayo bado yanatakiwa kufanyiwa kazi, huu inawezekana ni utaalam mpya.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Waziri ya kuchukua hatua na kuendelea kufuatilia lakini tuna imani inawezekana mfumo wa TAUSI ukafanyiwa marekebisho zaidi na kutumia fursa na changamoto zilizojitokeza ili kudhibiti changamoto hizi za upotevu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza sana Ofisi ya CAG kwa kuwa jicho makini la Bunge katika hali kama hii, tuna imani Serikali itazidi kuiwezesha kifedha ofisi ya CAG ili kuwa na muda wa utekelezaji wa wigo mpana wa majukumu yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mara nyingine tena nawapongeza sana Waheshimiwa Wabunge na naomba kutoa hoja.

MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Naibu Spika, naafiki.