Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022, Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022

Hon. Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022, Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022

MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana kwa fursa hii na mimi niweze kutoa mchango wangu kwenye taarifa zilizowasilishwa hapa. Kwanza kabisa nianze kwa kuunga mkono hoja kwa Kamati zote tatu.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo nitaanza kwanza ku-recall katika Bunge la Bajeti ndani ya Bunge hili, tulipisha fedha nyingi zilizoenda kwenye Wizara ya kilimo ambayo inaenda takribani Bilioni 954. Kati ya fedha hizo asilimia 35 inaenda kwenye sekta ya umwagiliaji, tunatamani na Wabunge tunaamini kwamba fedha hizo zilizopitishwa zinaenda kuleta mabadiliko makubwa kwenye sekta ya kilimo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitarudi nyuma mwaka 2018/2019 CAG alifanya ukaguzi kwenye miradi Tisa ya umwagiliaji, ambayo ilifanyika chini ya Wizara ya Kilimo, Wizara ya Kilimo ilikuwa inasimamia miradi miwili na miradi Saba ilikuwa chini ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji. Alikutana na mambo mengi ya ajabu na hii itupe fundisho kwamba tunapoenda kutekeleza miradi ya umwagiliaji tuliopewa pesa Bilioni zaidi ya 300 tupate somo kwa miradi hii ambayo imefanyika na imepelekea Taifa hili hasara kubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaanza na miradi ile miwili ule wa Msolwa pamoja na Kingali iliyofanyika chini ya Wizara ya Kilimo. Ile miradi ilikuwa na mambo mengi ya ajabu. Kwanza Msanifu aliyepewa kusanifu alipewa kazi hajaona site, ni mtu aliyepewa kazi akiwa ofisini, mradi wa shilingi milioni 835 na baadae akaleta ripoti, ripoti ile alipowaletea wataalam Wizarani hawakufanya uhakiki, moja kwa moja wakaingia field na baadae akawaletea yeye binafsi kwa kufanya kazi ile variation ya karibia asilimia 58. Kwa hiyo, kutoksa milioni 835 alienda kulipwa zaidi ya bilioni moja na milioni mia tatu. Kwa hiyo, ikawa variation ya asilimi 56 na hiyo ni kinyume na Sheria ya Manunuzi iko-very clear.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria ya Manunuzi ili uweze kufanya variation ni plus fifteen or minus fifteen kwa maana fifteen percent kama unaongeza na kama unapunguza ni fifteen percent. Nje ya hapo scope hiyo haipo rudia upya tangaza tenda upya maana yake ni kitu kizima. Kwa hiyo, watu hawa wakafanya maksudi wakaingiza Serikali hasara kubwa!

Mheshimiwa Naibu Spika, hawakuishia hapo huyu mtaalam mwelekezi hakufanyiwa due diligence, katika application yake aliambatanisha CV za wataalam lakini kumbe wale wataalam ilikuwa ni gelesha, walioenda kufanya kazi actual field hawakuwa wale walio-submit zile CV. Kwa hiyo ilikuwa ni kuwa-fix wale watu wa evaluation wamu- award tender wakishamu-award wanaoenda ku-perform ile contract kwenye field ni watu wengine ambao ni makanjanja, haya mambo yamefanyika kwenye miradi ya umwagiliaji ambayo pesa ile pia ilikuwa ni mkopo.

Mheshimiwa Naibu Spika, mikopo inakopwa kuja kufanya kazi za maendeleo, kuna watu wajanja wanajiita wataalam wako huko Wizarani. Juzi nimekuona Mheshimiwa Bashe uko huko Ruvuma tayari wameshaanza kukuchezea, tayari Mkandarasi mwaka huu fedha hizi ameenda kufanya madudu Ruvuma na ume-terminate contract! Hiyo ni postmortem hatutakiwi kufanya postmortem, kuanzia stage ya kwanza tunapoanza initial procurement proceedings lazima tuhakikishe kwamba kuna compliance. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama tutaenda kwa staili hii ya kufanya postmortem ya ku-terminate contract tutaliingiza Taifa hili hasara kubwa sana. Huyu mtu hajafanyiwa due diligence na average ya mikataba yote imechukua muda mrefu sana zaidi ya siku 450 amezidisha kwenye ku-implement huu mradi, leo hii tumepitisha kwenye Bunge hili tuna miezi 18, sitarajii baada ya miezi 18 tuje tuanze kufanya the same post-mortem ndani ya Bunge hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, huku ndiyo tunaona Watanzania wote kwenye kilimo kwenye umwagiliaji hawakuishia hapo wameendelea miradi mingine mitatu waka-award contract walivyo-award contact Tume hii ya Taifa ya umwagiliaji baadae wakasaini mkataba na Wakandarasi hawa watatu, walivyosaini mtakaba kesho yake wasema hatuna fedha tuna-terminate hizi contract. Sasa kuna litigation issue, legal status ya mambo haya iko wapi? Mtapelekwa Mahakamani kama Wizara! Kama mlijua hamna fedha nani aliwatuma mkatangaze tenda na Sheria ya Manunuzi iko very clear. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hautakiwa ku-initiate procurement proceedings kama hamna availability of budget, full stop. Sasa mlienda sijui wapi. Baada ya muda mfupi wakatangaza tena upya, kuna Tender Board zinakaa hapo ni cost za walipakodi tena Wizara maskini kama Wizara ya Kilimo ya watu ambao ni wanyonge, mnakaa Tender Board mna-award mnasaini mikataba na mikataba kwa sababu ni mikubwa ni ya Mabilioni inaenda mpaka kwa AG. AG naye kule anaenda kufanya vetting inarudi mnakuja pale kwamba sisi tume tume-cancel kesho tunatangaza upya tenda! Taifa hili linachezewa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hawakuishia hapo, baada ya ku-award wameendelea na michezo hiyo wakawa-award tena Wakandarasi wengine mikataba mitatu iko hapa, walivyowa-award wale watu hawaku-perform wakashindwa, Tume ikasema kwamba basi jamani, safi ninyi ni Watanzania meshindwa tupeni, wakaenda kufanya kwa force account wakatumia tena fedha zilezile za Tume ya Umwagiliaji ku- implement miradi ile ile kwa force account wakati kuna Mkandarasi walimpa. Hatujawahi kusikia kwamba Mkandarasi alipelekwa Mahakamani kwa ajili ya liquidated damages, hatujawahi kuona kwamba kuna hatua zozote kali zimechukuliwa, business as usual, maisha yanaendelea tumepewa Bilioni 300, na nampa alert Mheshimiwa Bashe hatutaki tena baadae story kama hizi. (Makofi)

MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Naibu Spika, Taarifa.

NAIBU SPIKA: Taarifa.

T A A R I F A

MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na mchango mzuri anaoendelea nao kuzungumza mzungumzaji, nilitaka nimpe tu taarifa kwamba changamoto unayoiona sasa hiyo kwenye Tume ya Umwagiliaji Fungu 05, tayari kwenye fedha za ECF nilizokuwa nazizungumza wamepewa bilioni 215, sasa changamoto ikija hiyo sasa sijui kama tutaendelea kupewa zile Awamu Sita zilizobakia.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni hiyo tu taarifa niliyokuwa nampa. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Deus.

MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, naipokea taarifa. Leo sina mambo mengi nilikuwa mime- focus tu kwenye Tume ya Umwagiliaji na rafiki yangu Mheshimiwa Bashe Waziri wa Kilimo, umenipa mradi mkubwa nashukuru lakini jambo hili tusimame pamoja tukaisimamie hii Tume ya Umwagiliaji. Nakuamini sana, nakuomba sana pesa zote wanachezea huku tunapiga kelele sawa, mmefanya reshuffle mmemuweka MD mpya na nini. Tunaomba muende mpaka chini, wataalam Maafisa Manunuzi wadogo mnawaacha... (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)