Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2022

Hon. Fakharia Shomar Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2022

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Mwenyekiti ahsante. Kwanza sina budi kuzipongeza Kamati zote zilivyowasilishwa hapo, zimewasilisha vizuri. Vilevile nipongeze na Vikosi vyetu vya Ulinzi ambavyo vinafanya kazi nzuri ya kulinda raia wake waliyokuwepo nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niongelee Magereza kuhusiana na parole. Parole ilikuwa nia yake kupunguza msongamano uliokuwepo Magerezani. Sheria ni nzuri, lakini wanashindwa kufikia mwisho na kwa nini wanashindwa kufikia mwisho na magereza yetu yanakuwa na msongamano wa wafungwa? Ni kwa sababu Bodi inakaa inaangalia, inafanya tathmini inamwona huyu raia alivyo anastahiki kuwa huru, lakini raia yule hawezi kuwa huru kwa sababu sheria inazungumza kwamba lazima mhusika wa kesi ile aliyomshtaki yule mtu aridhike na yeye, kwa sababu yeye ndiye aliyemshtaki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa pili wa ubinadamu mtu ameshakaa Gerezani muda mrefu, Bodi wameunda kisheria na huyu mtu ameshaangaliwa anafaa kutoka, anachukuliwa mtu wa mtaani kwa sababu ndiye aliyemshtaki anakuwa mtu yule ana roho mbaya, siku nyingine anaichukia familia ya yule mtu anakataa, akikataa hawezi kutoka. Sasa hii sheria inafanya kazi gani? Hii sheria wailete tuibadishe au mhusika anayekuwa na ile kesi Bodi wanapokaa wamwalike, ili kama kuna hoja zitoke kule, hawawezi kumfanya yule mtu anakubali mwenzie atoke kutokana na hoja zilizokuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama hii sheria haijaletwa, ikafanyiwa marekebisho kipengele baada ya kipengele, msongamano wawafungwa Magerezani utakuwa unaendelea. Hili lingine nataka nilizungumze kwamba hivi sasa Bodi ya Parole haina Mwenyekiti na pia si mbaya mkaliangalia na hilo ikapata Mwenyekiti, Bodi ikaweza kutimia na ikafanya kazi kihalali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja na hii diplomasia ya kiuchumi. Diplomasia ya Kiuchumi kwa Tanzania itatusaidia sana, lakini tuishinikize Wizara ile Sera ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje itoke, kwa sababu ile sera ndiyo itazidi kuiboresha hii diplomasia ya kiuchumi kwa sababu kuna mambo mengi humo yanataka kuangaliwa. Tunataka kuangalia the diaspora, tunataka kuangalia Wawekezaji wetu watafanya kazi vipi? Tunataka kuona Wizara za Kisekta ambazo nazo zinataka kuchangia ingawa Wizara inasema wanashirikiana na Wizara za Kisekta, lakini mwamko hatuoni. Watakapotoa sera kutakuwa na kanuni, wataweza kuzibana hata hizi Wizara za Kisekta ziweze kufanya kazi na zikiweza kufanya kazi tutajua kwamba hii Sheria itaweza kufanya kazi na diplomasia ya kiuchumi itaweza kunyanyuka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile bila kuwepo sera na kanuni na elimu mikoa yetu haitoweza kufanya kazi kwa sababu jambo lolote literemke chini kwenye mikoa na wilaya lakini hawajui kinachoendelea na hawajui kinachoendelea kwa sababu sera bado haijajipanua, ingawa Wizara wanasema kwamba iko njiani wakati wowote itatolewa. Tungeomba itoke tupate na kanuni ili iweze kufanya kazi na hizi shughuli za kidiplomasia za kiuchumi, tuweze kufanya wafanyabiashara, wawekezaji, wakulima wajue mipaka yao vipi watafanya kazi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja katika hili la wahamiaji haramu nchini. Hili kweli suala zito, hili suala pia tunaongeza msongamano Magereza kwa sababu watu wanatoka nchi nje anaingia ndani Tanzania, anazamia, anakuja tuseme kaja kisheria au kaja kinyume na kisheria, anazamia humu, wanawakamata wanawapeleka Magerezani Serikali ndiyo inaingia gharama, lakini kuna mtazamo Wizara ya Mambo ya Ndani ambao wanauangalia kwamba wanataka wafanye sasa hivi wanaingia kama wameingia kisheria, wanawagongea wapite waende zao itakuwa nzuri au hawakuja kisheria wanaambiwa arejee tena kwao lakini hapa Tanzania asikae kutuongezea msongamano Magerezani, kuwalisha Magerezani, mtu kakaa akiondoka kama alikuja na lilishe duni anaondoka ametengemaa hapa Tanzania. Sasa hata na hilo tunaona liangaliwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, naweza kuzungumzia kidogo tu fedha za maendeleo. Jamani Wizara ya Fedha vioneni vikosi, fedha ya maendeleo hamuwatilii na barua za kuomba wanakuleteeni na barua wakileta, hii tunaingia quarter ya mwisho, kesho kutwa quarter ya mwisho, unampa pesa mwisho aifanye nini? Wakati ilikuwa kuna quarter ya kwanza, ya pili, ya tatu, hata yale malengo yalikuwa kayapangia hayawezi kufanikiwa. Sasa hebu watazameni jamani, kwani Vikosi vimekosa nini Hata hamuwapi? Naomba hili suala jamani tuliangalie, Vikosi wanatusaidia, wanatulinda na ndiyo watu wetu wa karibu katika nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)