Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022

Hon. David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022

MHE. DAVID M. KIHENZILE – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashukuru Waheshimiwa Wabunge waliochangia hoja mbali za kamati yetu lakini ikiwa ni pamoja nakuunga mkono maazimio yetu. Sitaenda kwa mtu mmoja mmoja lakini waliochangia karibu wajumbe 10 ambao wametoa maoni mbalimbali. Cha kwanza nishukuru Serikali kupitia mawaziri kwa kukubali kufanyia kazi hoja zetu ambazo tumezitoa, kuanzia Mheshimiwa Waziri wa Mazingira Mheshimiwa Jafo, lakini pia na Mheshimiwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mheshimiwa Ashatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hoja zake kuu za mwishoni ikiwa ni pamoja na kutoa commitment ya Serikali kulipa bilioni 15 kama fidia kwa wananchi waliopo kule Ludewa kwenye mradi huu wa Liganga na Mchuchuma. Vilevile kutoa kauli ya Serikali juu ya majina mabaya yanayopewa wafanyabiashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye hili nataka niseme kidogo kama tuko serious kama Taifa tunahitaji kuvutia uwekezaji nchini, tujue tuna kazi kubwa sana ya kuvutia watu waje kuwekeza kwenye nchi yetu wasiende kwenye nchi nyingine. Kuwambia wafanyabiashara wenye option ya kwenda kwenye nchi hii au nchi nyingine ni wezi, ni mafisadi ni kuwa-discourage. Matokeo yake hawatokuja kwetu, watakwenda kwenye nchi nyingine halafu tutabaki tunaulizana hapa kwa nini nchi yetu katika wafanyaji biashara ni ya141 kati ya nchi 190. Kwa hiyo, nimshukuru Mheshimiwa Waziri na tuone utekelezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, iko hoja nyingine ambayo kidogo niifafanue ya Liganga na Mchuchuma. Sote ni mashahidi Liganga na Mchuchuma Makaa ya Mawe yaligundulika mwaka 1860 wakati Liganga mwaka 1898 ukipiga hesabu kwa mfano Makaa ya Mawe tangu yagundulike mpaka leo ni miaka 185 tunaendelea bado kufanya jitihada. Umuhimu wa Liganga na mchuchuma kwa maslahi ya watanzania hauyumkuniki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano makaa ya mawe yana deposit ya tani Milioni 428 ambapo tukianza mradi huu kama case study tutapata makaa ya mawe karibu Milioni tatu kila mwaka. Pili, moja ya changamoto kubwa ambayo taifa letu linapata kwa sasa ni kuagiza chuma kutoka nje ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa ninazo takwimu kwa miaka mitano peke yake Taifa la Tanzania limetumia takribani trilioni tano kuagiza chuma kutoka nje. Fedha hizo zimeagizwa kwa njia ya USD dolla za kimarekani. Kwa mfano mwaka 2018, takribani dola 400,100/= tulitumia kuagiza chuma, 2019, 1.1 trilioni. Ukiangalia mapato hayo ni takribani sawa na fedha ambazo tunazikusanya za TRA kwa mwaka kwa miaka hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, umuhimu wa mradi huu hauyumkiniki, ukija kwa mfano kwenye aspect namba tatu, tulisema mradi huu ukikamilika utasaidia kujenga barabara za lami kutoka Njombe mpaka kwenye eneo la mradi kwa zaidi ya kilomita 221. Tutajenga reli, tutajenga bandari lakini kama haitioshi tutaingiza kwenye gridi ya Taifa Megawatt 600. Sisi Kamati ya Viwanfda na Biashara tumefanya ziara kwenye viwanda, tumekuta baadhi ya viwanda wanalalamika umeme umekatika Zaidi ya mara 20 kwa mwezi mmoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi ni Megawatt nyingi tulielezwa kati ya Megawatt 600, takribani Megawatt 250 ingetumika kwenda kuchakata chuma, 350 ingeingizwa kwenye gridi ya Taifa. Kutoka mwaka 2015 mpaka 2020 tumeongeza takribani Megawatt 300 kutoka 1300 mpaka 1600. Hivyo umuhimu wa jambo hili hauna mjadala. Hata hivyo kama kamati tunaendelea kusimamia lazima tuweke maslahi ya Taifa mbele. Haiwezekani, haikubaliki na haiwezi kuvumiliwa na watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtu anakuja na dolla Millioni 600 anatumia dhamana za Taifa letu 2.4 bilioni halafu anapata mgao wa 80 percent ninyi mnapata asilimia 20. Hii biashara haiwezi kuwepo. Sisi kama kamati hatukubali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kama kamati haikubaliani, hii ni sawa na mikataba ya zamani ya akina Mangungu wa Msovero. Ndio maana tunaungana na Serikali walipoamua kufanya review upya, kupitia terms, kupitia vivutio kipi kilikubalika. Kama tulikubaliana kwenye awamu ya kwanza tulikosea kwa hiyo, twende kwenye awamu ya pili tukubali? Haiwezekani! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tunaiunga mkono Serikali, hata hivyo mambo mawili au matatu kaa tulivyo andika kwenye ripoti yetu: -

(i) Uharakishwaji ufanywe kwenye mjadala huo. Aidha kwa mkandarasi huyo au mwingine ili wananchi wa Taifa hili waache kuagiza chuma kutoka nje, wananchi wa Taifa hili wapate umeme tunaouhitaji, taifa hili tujengewe lami, ile southern corridor iweze kuwa improved;

(ii) Fidia, wale wananchi wasio na hatia ambao hawahusiki hata kwenye mijadala yetu ni vema walipwe fidia yao mara moja. Tunaipongeza Serikali kwa mambo mawili; moja, kwa kufanya review kwa sababu uthamini wa kwanza ulikuwa unaonesha bilioni 13, lakini wakasema tukiwalipa thirteen billion itakuwa ni kuwaonea kwa mujibu wa Sheria. Wamefanya review na sasa imeonekana ni bilioni 15 tunaiomba Serikali illipe mara moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayo na kwa sababu na mengine nimeshazungumza kwa umoja wake pamoja na ushauri ambao umetolewa na Wabunge mblimbali naomba sasa kutoa hoja.

MHE. ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.