Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Waziri Mkuu

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Waziri Mkuu

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua fursa hii kukushukuru wewe kwa kinipatia nafasi hii ya kutoa mchango wangu katika hotuba hii ya makadirio na mapato ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka fedha 2022/2023.

Mheshimiwa Spika, napenda kuanza mchango wangu kwa kumpongeza Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoongoza nchi yetu kwa umakini mkubwa. Namuombea kila la kheri katika kazi zake.

Pili, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na wafanyakazi wake wote kwa kutayarisha na hatimaye kuiwakilisha hotuba hii katika Bunge lako tukufu kwa ufasaha na umakini mkubwa.

Mheshimiwa Spika, katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo; kwanza ni Benki ya Maendleo ya Kilimo; napenda kutoa shukurani zangu za dhati kuishukuru Serikali yetu inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza mpango wa kuipatia fedha benki hii kwa ajili ya mikopo ya wakulima hasa wadogo wadogo. Benki hii ni mategemeo makubwa kwa wakulima wetu katika ukombozi wa kujinasua kiuchumi.

Ushauri wangu katika jambo hili Serikali iendelee kuhakiki aina ya wakulima wanaostahiii kupata mikopo hiyo ili kuepuka kila mwaka kurejea makundi hayo hayo na kuwaacha wengine.

Mheshimiwa Spika, pili ni kuhusu uvuvi; napenda kuchukua fursa hii kuipongeza Serikali kwa jitihada yake kubwa inayochukua katika kuimarisha sekta hii ya uvuvi. Sekta hii ni miongoni mwa sekta inayowagusa moja kwa moja wananchi wa kipato cha chini. Ushauri wangu kwa Serikali katika sekta hii ya uvuvi ni kuwaendeleza wavuvi hasa wadogo kwa kuwapatia mitaji, aidha kwa njia ya mikopo au kwa ruzuku ili kuweza kujiendeleza na kuweza kujikwamua kiuchumi.

Mheshimiwa Spika, tatu ni uwekezaji; napenda kuipongeza Serikali yetu kwa mipango yake yenye azma ya kutekeleza na kukuza uchumi wa nchi kwa kuvutia wawekezaji katika nchi yetu. Uwekezaji ni jambo jema, likisimamiwa vizuri kwa kuliwekea mazingira mazuri ambayo yatawavutia wawekezaji wa ndani na nje.

Ushauri wangu kwa Serikali juu ya sekta hii ya uwekezaji ni kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji. Bado mpaka leo kuna manung’uniko yasiyo rasmi kwamba upatikanaji wa maeneo ya uwekezaji sio rafiki. Wawekezaji wanachukua muda mrefu kupata maeneo hayo hasa ardhi. Urasimu bado unawasumbua wawekezaji.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.