Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Waziri Mkuu

Hon. Zuberi Mohamedi Kuchauka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Liwale

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Waziri Mkuu

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, naomba kuchangia Wizara hii kwa mambo yafuatayo; kwanza Sheria ya Mfuko wa Maafa, hivi sasa mfuko huu hautumiki au hausaidii maafa yanayotokana na shughuli za uchaguzi jambo ambalo linavunja moyo wa kazi kwa Maafisa Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi, pamoja na wagombea wa ngazi mbalimbali. Mfano katika uchaguzi wa mwaka 2020 katika Wilaya ya Liwale, magari ya Serikali matatu, ya watu binafsi yaliyokodiwa na wasimamizi matatu na magari ya Mbunge matatu, hivyo kufanya magari zaidi ya tisa na mali zingine. Lakini hakuna aliyepata japo kifuta machozi, pamoja na uharibifu huo mkubwa.

Pili, miradi ya kimkakati kwenye Halmashauri zetu nchini; miradi hii ilibuniwa ili kuongeza mapato kwenye Halmashauri zetu, lakini sasa kwenye utekelezaji wa miradi hii inaenda kwa kusuasua sana na pengine haitekelezwi kabisa. Mfano katika Wilaya ya Liwale kulikuwa na mradi wa soko na mradi wa stand. Mradi wa stand fedha zilikuja, kutokana kuchelewa kuanza kwa mradi fedha zilirudishwa Hazina. Hadi leo hatujui hatima ya mradi huu.

Tatu, suala la wanyamapori kwenye vijiji au kata zinazopakana na hifadhi hapa nchini imekuwa ni kero kubwa sana juu ya wanyama hao kujeruhi na kula mazao ya wananchi katika maeneo hayo. Nashauri Serikali ione umuhimu wa kuwa na askari wa wanyamapori katika kila kata zilizoko mipakani na hifadhi kama ilivyo kwa polisi kata ili kusaidia kudhibiti wanyama hao na kupunguza madhara. Jambo hili liende sambamba na kulipa kifuta machozi kwa wakati kwa wale waliopata madhara mbalimbali.