Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo kwa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024

Hon. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo kwa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshiniwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii yakuchangia katika mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2023/2024.

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nianze kwa kuishukuru Serikali kwa kuweza kuajiri watumishi wa TRA. Kamati yangu imekuwa ikipigia kelele sana ufanisi wa kazi wa TRA na tuliona kwenye ripoti yetu tuliyoleta, jinsi ambavyo kumekuwa na shida katika kukusanya kodi. Kwa hiyo, unakuta kwamba madai yanaongezeka kutoka trilioni 3.9 mpaka trilioni 7.5 ambayo ilikuwa kama asilimia 95 ya madeni ambayo hayakukusanywa kwa mwaka wa 2020/2021. Najua kwamba Taifa letu linategemea sana kodi na kama hazikukusanywa na hata hii Mipango tunayoongelea haiwezi kufanikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo mimi nataka nichangie tu katika eneo moja, hili eneo liko chini ya sura ya tatu ya maeneo ya kipaumbele kwa mwaka 2023, Namba 332, ambayo inazungumzia kilimo, mifugo na uvuvi, Ukurasa 124. Ni aibu kwa Taifa letu, na ninamuona Waziri Ndaki ananiangalia sana, kwamba, sasahivi Taifa letu hapa tulipofikia na baada ya kuwa na Wizara nzima ya Mifugo bado watu wafugaji, hatuwaiti wafugaji, wachungaji, wanakimbizana na ng’ombe, ng’ombe waliochoka, ng’ombe waliokondeana, halafu ng’ombe hawa wanaenda kulishwa kwenye mashamba ya wakulima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumesema sisi kazi yetu kubwa hapa kwenye Bunge ni kutetea wanyonge. Hakuna watu wanyonge waliozidi wafugaji na wakulima. Sasa unashangaa tunaacha haya makundi mawili yanamalizana. Hivi karibuni tumeshuhudia watu wakikatwa mapanga, watu wakiuana kwa vile makundi ya ng’ombe yanaswagwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine na yanashambulia mashamba ya wakulima. Swali langu najiuliza, hivi tuliunda Wizara nzima ili nini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukifanya cost benefit analysis ya Wizara nzima na kazi inayofanyika sijui kama ita-balance. Mimi nilitegemea, kama kilimo walivyosema, kwamba wanatenga blocks kubwa vivyo hivyo nilitegemea mifugo yetu, wale wafugaji wetu watengewe maeneo. Wale wenye ng’ombe wengi wanaweza kuelezwa wakaambiwa kwamba tunakupa eneo hili kama linakuwa fenced, kama wanapeleka miundombinu na wao wachangie ili waweze kufuga mifugo ya kisasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua kwamba, Rais wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Jakaya Kikwete, alilizungumzia sana hili suala la wachungaji akiwa Rais. Aliomba sana Serikali iangalie namna ya kuondokana na kuswaga ng’ombe tuwe wafugaji badala ya wachungaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ametoka imekuja awamu ya tano na sasa ya sita. Leo ndio tunaona vita vikubwa sana kati ya wakulima na wafugaji halafu Serikali tunaangalia. Unashangaa hivi hawa wafugaji wana nguvu gani kuliko Serikali kiasi mtu anaamua kuswaga ng’ombe na kuingiza kwenye mashamba ya wakulima? Kwa hiyo umasikini wetu huu tunauzungusha wenyewe, vicious circle ya umasikini wetu wa nchi, matokeo yake tutaanza tena kuomba chakula. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mifugo tunajua faida yake kubwa. Kwanza wenzetu wengi walioendelea wageni wanaokuja nchi hii wana-import nyama kutoka Botswana au kutoka nchi zao, nyama yetu ukila hap ani plastic ng’ombe wale walivyo. Sasa tunashindwaje kuweka viwanda kule Shinyanga tukasaidia watu wetu wafugaji kule wakatengewa maeneo, wakafundishwa kuweka majani ya kisasa, wakatengeneza hata bio gas ili wawe na nyumba zile wasiingie hasara za kutumia umeme huu wa grid wakawa na silage ile ambayo wanaweza wakitoa biogas wanaweka kwenye majani, wanaweka kwenye mimea? Ni kazi ngumu gani kuona kwamba, kule tungeweza kuweka viwanda vya ngozi, viwanda vya maziwa na by products nyingine? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu kwato zile zinatengenezea jelly, ile gundi. Sasa sisi Tanzania tunacheza. Angalia wenzetu wa Botswana wameona kwamba sasahivi almasi walikuwa wanaitegemea, Ulaya na Marekani sasahivi wanatengeneza almasi fake, hawana soko, wamezamia kwenye mifugo tu. Na Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Mchemba ametuwekea data jinsi ambavyo wenzetu uchumi umekua katika muda huu mfupi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niombe sana na Waziri wangu wa mifugo namheshimu sana, Waziri Ndaki, hebu angalia tuweke blocks tuchukue vijana wetu hawa waliosomea mambo ya mifugo tuwawezeshe. Hizi fedha zote zinazotolewa kwenye vikundi wapewe, wawezeshwe, watengenezewe maeneo waweze kufuga kisasa. Ahsante sana. (Makofi)