Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

Hon. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii ya kuhitimisha hoja ya Kamati yangu. Natambua kwamba umenipa dakika tano tu; pamoja na kwamba ningependa ni-respond kwa kila mmoja aliyesema, kwa muda wa dakika tano sitaweza kufanya hivyo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nitambue tu kwamba waliochangia upande wa hoja za PAC ni Mheshimiwa Bakar Ahmad, Mheshimiwa Aysharose Mattembe, Mheshimiwa Anatropia Theonest, Mheshimiwa Venant Daudi, Mheshimiwa Aida Khenani, Deus Sanga, Mheshimiwa Samuel Songe na Makamu wangu, Mheshimiwa Japhet Hasunga.

Mheshimiwa Spika, ukiangalia yale yote ambayo Mheshimiwa Japhet Hasunga ameyasema, ni kama ame- summarize hoja yote, tunataka Serikali ikaifanyie kazi. Kwa kutambua kwamba Serikali imeweza kujibu hayo machechi ambayo waliweza kuyajibu; na kwa kuwa tunajua kwamba sisi PAC hatu-rely kwa majibu ya mdomo, ni mpaka tena CAG aende a-verify hayo mliyosema, napenda kusema kwamba nitambue michango yote ya Waheshimiwa Mawaziri ambayo Kamati tumeipokea. Ni imani yetu kwamba Serikali itatimiza wajibu wake ili sasa katika kaguzi zijazo Kamati ifanye ufuatiliaji wa utekelezaji wa Maazimio ya Bunge.

Mheshimiwa Spika, nawashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa kuchangia hoja ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC).

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, naomba kutoa hoja kwamba sasa Bunge lako likubali maoni na mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ili yawe maazimio ya Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Spika, naafiki.