Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

Hon. Twaha Ally Mpembenwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibiti

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi kuweza kuchangia taarifa ambayo imewasilishwa mbele yako. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kabla sijaanza kuchangia taarifa hii kwanza nilikuwa naomba nichukue nafasi hii kukupongeza kwa kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lakini sambamba na hilo nimpongeze Mheshimiwa Rais mama yetu Samia Suluhu Hassan jinsi anavyoweza kuendelea kufanya kazi kupeleka fedha katika halmashauri zetu zote nchini na kuweza kuona maendeleo yanakwenda kufanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kipekee nishukuru fursa hii kuwapongeza Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kwa kazi kubwa na nzuri ambazo wanazifanya ili kuweza kusimamia fedha hizo. Sambamba na hilo shukrani za dhati kabisa ziende kwa Mkuu wangu wa Mkoa wa Pwani, Alhaji Abubakar Kunenge kwa kusimamizi wake mzuri kabisa wa fedha katika Mkoa wa Pwani na Wilaya zote kwa ujumla wake. Lakini bila kumsahau Mkuu wangu wa Wilaya Kanali Ahmed Abbas kwa kazi kubwa na nzuri wambayo anaifanya ndani ya Jimbo la Kibiti katika kuweza kusimamia halmashauri, miradi ya maendeleo na fedha vilevile ndani ya halmashauri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni mjumbe wa Kamati la LAC, kwa hiyo, nimesimama hapa kuchangia taarifa iliyokuwa imewasilishwa na Mwenyekiti wangu mama Grace Tendega ambayo imewasilisha taarifa hiyo in very majestic way. Ahsante sana Mheshimiwa Mwenyekiti. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nichangie nukta mbili tu, lakini katika nukta hiyo nitaigusa sana katika sehemu nzima masuala ya upotevu wa mapato ndani ya halmashauri zetu.

Mheshimiwa Spika, tumeona ndai ya taarifa yetu lakini tumeona vilevile wakati tulipokuwa tunafanya suala zima la ukaguzi na kuwahoji wale maafisa masuhuli. Kuna upotevu mkubwa sana wa mapato ya ndani ukizingatia kwamba mfumo unaotumika wa POS unautata mkubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, inatokea halmashauri moja au nyingine siku karibia 254 mashine ya POS inakuwa iko off, halafu hakuna taarifa zozote za kifedha ambazo zinaweza zikasoma katika halmashauri husika au kule TAMISEMI. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mbali ya hiyo kuna tatizo lingine la msingi ambalo linapatikana katika upotevu wa fedha, tatizo hilo ni kwamba kuna kitu kinaitwa adjustment. Watu wa halmashauri wanachokifanya ni sawasawa kwamba mtu amekwenda kukatiwa risiti ya shilingi milioni moja, halafu baadae anakuja kufanya adjustment kwamba amekata risiti ya shilingi laki moja. Katika taarifa ambayo ilikuwa imesomwa na Mwenyekiti wangu hapa fedha takriban shilingi bilioni 4.5 zimeweza kuonekana zimefanyiwa adjustment katika kipindi cha mwaka 2019/2020. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nini ushauri wangu, ushauri wangu kwa Serikali kuna shida pale katika kitengo cha TEHAMA – TAMISEMI, lazima suala hili liweze kushughulikia kwa sababu haiyumkiniki halmashauri 35 adjustment zilizokuwa zimeweza kufanyika bilioni 4.5 kama zingekuwa halmashauri zote 86 zingeweza kufanyika adjustment za kiasi gani. Kwa hiyo, pale TAMISEMI katika Kitengo cha TEHAMA kuna tatizo la msingi zaidi. Kwa hiyo, ni vema Serikali muweze kuangalia nini mnachoweza kukifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini katika eneo lingine ambalo nilikuwa naomba nitoe ushauri. Kuna shida kubwa kidogo kwa wataalam wetu katika suala zima la kuweza kuwasilisha mahesabu au kuandaa mahesebu. Wataalam hawa tunajua wana professional zao, lakini nilikuwa naomba kuishauri Serikali waendelee kuwafanyia training kwa sababu wanachokuwa wanakifanya zile financial statement ambazo zinakuja zinakuwa na mapungufu mengi sana; na kwa tafsiri hiyo hiyo maana yake ni nini? Inakwenda kusababisha madhara kwa watumizi wengine wa financia statement. Kwa hiyo, nilikuwa naishauri Serikali waweze kuangalia uwezekano ni jinsi gani watakavyoweza kufanya training kwa wataalam wetu ambao wanafanya shughuli hizo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika eneo lingine la msingi zaidi ambalo nilikuwa naomba nilichangie, halmashauri zetu nyingi sana zina madeni. Na madeni haya yanasababishwa na suala zima la uandaaji wa financial statement. Kwenye accounts kuna kitu kimoja kinaitwa massaging the figure au window dressing, wanachokuwa wanakifanya ni kwamba financial statement inaandaliwa inakwenda kuwa-impress other users ambao wanakuwa kama vile financial institution. Halmashauri inatoka inakwenda kuomba mkopo, lakini kutokana na kwamba ile financial statement imechezewa, kinachofanyika pale ni kwamba wanakwenda kupata mkopo, ambapo mkopo huo hawawezi kuumudu. Kwa hiyo, kwa kufanya hivyo maana yake ni nini? Tunaziweka halmashauri katika matatizo mengi sana ya msingi. Halmashauri nyingi sana zinakuwa zinakesi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa heshima na taadhima na unyenyekevu wa hali ya juu kabisa naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)