Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

Hon. Tarimba Gulam Abbas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kinondoni

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi hii na mimi niweze kuchangia kuhusu taarifa za kamati ambazo zimewasilishwa leo. Kwanza kabisa naomba nianze kwa kusema naunga mkono hoja hizi lakini nianze vile vile kwa kumtaja Mwenyezi Mungu na niruhusu niseme Bismillah Rahman Rahim. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nazungumzia maji kama ilivyokwenye ukurasa 27 nikipata muda nitazungumzia page 12 taarifa ya Kamati ya Bajeti. Mimi ni mjumbe wa Kamati ya bajeti na kwa hali hii nazungumza mambo ambayo nayafahamu vizuri zaidi. Juzi tulikuwa na mazungumzo na Mheshimiwa Waziri wa Maji na katika Mazungumzo yale tulizungumzia masuala ya RUWASA, tukaona ugumu wa matatizo ya maji ambayo yako vijiji, tutakaa miaka mingi sana bila ya matatizo ya maji kuweza kupatiwa ufumbuzi wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, na Tanzania hii na Bunge hili hakuna siku ambayo inapita bila Mbunge yoyote kusimama kuzungumzia habari ya maji maswali ya maji yamekuwa ni mengi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Serikali na kwenye hili tuige mfano mzuri wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan alipokwenda kutuletea fedha za mkopo ambazo zimeondoa matatizo ya shule za Sekondari katika Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimemwambia Mheshimiwa Waziri wa Maji kwamba hebu nendeni kwenye kila Wilaya angalieni mahitaji ya maji, angalieni vyanzo vya maji viko wapi tengenezeni mpango ambao utaiangalia Tanzania nzima ni wapi kwenye matatizo ya maji ni wapi maji yanapatikana hata kama ni kumshauri Mheshimiwa Rais akope fedha tumalize masuala ya maji, Bunge hili linaweza likaweka alama kubwa sana Bunge la Kumi na Mbili kwamba angalau asilimia 80, 90 ya matatizo ya maji yanaweza kwenda kumalizwa, tukope, kuna hasara gani ya kwenda kukopa kwa ajili ya mtanzania? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba iingie katika Kumbukumbu na Mheshimiwa Waziri wa Maji sijui kama yuko hapa, lakini hachukue hilo kwamba Bunge hili kwamba limechoka kusikiliza maswali ya maji kila siku wakati tunaweza kupanga tukayaondoa matatizo ya maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jingine kuna kitu ambacho nashangaa sana mwaka 2015 na hili linahusiana na page 12 ambayo inahusiana na hushirikishwaji hafifu wa sekta binafsi. Serikali haifanyi biashara, Serikali kazi yake kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara ili iweze ika-collect Government Revenue fedha kutokana na kodi.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2015/2016 walitengeneza kitu kinaitwa Blue Print na wakakitoa mwaka 2018 mwezi mei na ikaeleza vizuri sana ni jinsi gani inavyokwenda kuboresha maslahi ya ufanyaji biashara kwa madhumuni ya kupata fedha ya kutosha katika Government Revenue. Na wakati ule easy way of doing business, watanzania sisi tulikuwa ni nchi ya 131 mwaka 2015 wakati ikitolewa hii ripoti tulikuwa sisi ya watu 141 katika nchi 190. Maana yake ni nini? Tulikuwa bora kabla ya Blue Print haijatengeneza Blue Print imetengenezwa ndiyo tumeanguka na tatizo lake kamati inasema mpaka leo hii wingi ya mamlaka za udhibiti zinaendelea kuongezewa kila siku. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ukiangalia tozo zimejaa, ukiangalia ada kwenye biashara moja zimejaa, ukiangalia huku matatizo ya kodi siyo rafiki, mimi najiuliza ni kwanini basi tulitumia fedha kutengeneza Blue Print halafu ni sawa saw ana mtu uchonge kinyago halafu kile kinyango ukikiangalia unakiogopa eeh, tunatengeneza Blue Print tumeweka kwenye kabati hatuitumii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Serikali ituletee taarifa kamili ya jinsi ilivyotekeleza Blue Print katika kipindi chote hicho ili tuweze kufanya tathimini na kujiuliza ni kwanini hatutoki katika idadi ile ya 142.

NAIBU SPIKA: Ahsante!

MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana nakushukuru message sent. (Makofi)