Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

Hon. Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa nafasi hii ya kuchangia jioni hii. Kipekee nakupongeza sana kwa nafasi hiyo ya Unaibu Spika, kwa kweli Kiti kimepata mwenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesimama kwa ajili ya jambo moja tu; mengi ningeweza nikayasemea, lakini hili naliona ni muhimu sana, nalo ni lile la Universal Health Coverage Insurance. Toka lile Bunge lililopita tulizungumza hapa kwamba Serikali italeta Muswada ili tuweze kupitisha sheria ya kuwa na Bima ya Afya kwa Wote. Jambo hili limeleta kigugumizi, hatuoni kama Serikali iko tayari.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa naomba, kwa jinsi ambavyo Mheshimiwa Rais amejitahidi kutoa na zile fedha za UVIKO 19 zikaenda kumalizia zile dispensaries, vituo vya afya na kuboresha hospitali zetu, lakini jambo hili la insurance kwa wote limeleta kigugumizi. Kwa kupata fedha zile na kumalizia majengo bado hakutakuwa na sababu yoyote, yaani hakutakuwa na impact. Unaweza ukawa na majengo mazuri na hospitali nzuri, lakini wale watu wanaopatiwa huduma wasipatiwe; na wengi wao ni wananchi wa kawaida. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika data zilizoko kwenye nchi yetu, tunaambiwa kwamba National Health Insurance Fund ni 8% na hii ni lazima, anakulipia mwajiri na wewe mwenyewe unachangia. Ikija kwenye CHF ni 23%, hiyo iko kwenye Halmashauri, tayari kuna watu wamejiunga kwenye vikundi vya Vikoba, watu wamejiunga kwenye vikundi vya Kiarano, vikundi vidogo vidogo, lakini wanapata shida kupata huduma. Inakuwaje hiyo? Private sector ni 1% tu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesimama kuiomba Serikali yangu Sikivu, jambo hili lifikiriwe kwa kina, tutakapokuja Bunge lijalo sasa, Muswada huo uje hapa Bungeni tuweze kupitisha hii sheria. Wote hapa nyie Wabunge wenzangu ni mashahidi, kwa siku mnapata simu nyingi kusaidia matibabu kwa wananchi wenu. Tungekuwa na insurance hili lisingekuwa hivi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha, naunga hoja mkono. Ahsante. (Makofi)