Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

Hon. Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA - (MWENYEKTI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru sana kwa kunipa fusrasa hii ya kuja kujibu hoja au kutoa maelezo ya ziada kuhusiana na kazi ya Kamati yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashukuru Waheshimiwa wagunge wote ambao walipata fursa ya kuchangia kwenye hoja yetu, tumepata wachangiaji 10 ambao kwa bahati nzuri wote wameunga mkono taarifa ya kamati na kuipongeza, kwa niaba ya Kamati napenda kuzipokea pongezi hizo nasema ahsante sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi hakuna hoja za kujibu kwasababu wajumbe wote waliozungumza wamekubaliana na mambo yaliyosemwa na Kamati, kwamba kama taifa lazima tuhakikishe tunakuwa na utulivu wa uchumi wa nchi yetu na miradi ya umeme ni miradi muhimu kwa ukuaji wa uchumi wetu. Sekta ya mafuta inachango mkubwa katika uchangiaji wa maendeleo ya nchi yetu, kwa hiyo, wote wamejielekeza kwenye maoneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kubwa tunapozuzngumzia sekta ya umeme wote tunakubaliana kwamba tupo nje ya power system master plane yetu, na kwamba lazima tufanye jitihada zote kuhakikisha tunaitekeleza pawer system master plan hii kwa sababu ndio dira yetu inayotuelekeza kwenye ukuzi wa uchumi wa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafurahi kwamba mawaziri wenye dhaman ya kusimamia sekta hizi wameliona hili na wamekubaliana kwamba ipo haja ya kuongeza jitihada za kuhakikisha mambo yanakwenda sawa. Tunajua kazi ambayo Serikali inafanya kwenye mradi wa mwalimu, tunajua mmekanyaga pedo tunaomba muongeze kasi kuhakikisha mradi huu unamalizika. Tunajua jitihada mnazofanya kwa TANESCO ongezeni juhudi ili tuweze kupata mafanikio. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Makamu Mwenyelkiti wangu wakati anachangia alizungumzia suala la miradi ya REA na kwenye taarifa yetu tumezungumza kwamba tuhakikishe miradi hii inakamili, na yeye amekuja na aina nyengine ya kusisitiza, amesema miradi hii ya REA ambayo tumekwisha saini hatutegemei utekelezaji wake uwe chini ya kiwango tulichoingia mikataba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yapo maneno mtaani kwamba huenda wakandarasi wakapunguziwa kazi ambazo walikuwa wamekabidhiwa, tunaiomba sana Serikali hilo lisitokee, na kama tetesi hizo ni kweli basi maelezo hayo yaletwe kwenye kamati ili kuweza kushauriana kwa pamoja, baada ya kusema haya naunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)

Mheshimiwa mwenekiti, naomba kutoa hoja. (Makofi)

MHE. SEIF K. S. GULAMALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.