Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Shughuli zake kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Shughuli zake kwa Mwaka 2021

Hon. Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Shughuli zake kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Shughuli zake kwa Mwaka 2021

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nikupongeze wewe kwa kuendesha Bunge hili. Awali ya yote, namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutupa afya njema na uzima.

Leo hii tumepata wasilisho la kamati mbili; nampongeza sana Comred Mheshimiwa Chaurembo, ndugu yangu wa Mbagala, wa Mbande, wa Chamazi na kule maeneo ya Maji Matitu. Vile vile nampongeza sana Comred Dkt. Joseph Mhagama; Daktari huyu mpya mpya sana, Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Katiba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hii pia kumshukuru sana Mwenyezi Mungu, kama nilivyosema awali na pia kumpongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwenendo na utaratibu wa utendaji kazi ambao kila Mbunge anashuhudia. Katika Kamati yetu ya Katiba na Sheria kama mnavyofahamu ni kwamba inashughulika vilevile na suala la Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hoja za Kamati kwa kweli nami napenda kuchangia humo. Kwanza naipongeza Kamati kwa kazi kubwa sana ambayo imeendelea kuifanya. Kamati hii imechambua mambo mengi, lakini niseme kwamba, Kamati hii imefanya kazi kubwa sana katika suala zima la kudumisha Muungano wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tunavyofahamu, Baba wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Amri Abeid Karume walivyoasisi Muungano wetu, umeweza kupita katika vipindi mbalimbali na viongozi wetu wote wamefanya mambo makubwa. Viongozi waliopita tokea Awamu ya Kwanza mpaka sasa Awamu ya Nane na Awamu ya Sita, kazi kubwa sana imeendelea kufanyika. Tunapozungumzia katika kipindi cha sasa hivi, naishukuru sana Kamati, hasa kwa maelekezo yake muhimu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshuhudia tulikuwa na kero takribani 20 hadi 35 za Muungano. Katika kero hizo tuliweza kufanikisha kutoa kero saba mpaka mwaka 2010. Tulibakiza kero 18. Nawashukuru sana viongozi wetu wa Taifa, Mama yetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi. Kazi kubwa waliyoifanya katika kutuekeza, ambapo ndani ya muda mfupi tumeweza kufanikisha kuondoa kero 11 za Muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hoja ya Kamati hilo mmelizungumzia. Naishukuru sana Kamati yako, imeweka legacy na kwamba chini ya usimamizi wa Kamati yenu tumeweza kuondoa kero 11 za Muungano. Tunashukuru sana katika hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutaendelea kuhakikisha kwamba mustakabali wa Taifa letu la Muungano tunaenda kulifanyia kazi hasa, kama Kamati ilivyozungumza ajenda mbalimbali na hasa kushughulikia yale mambo mengine ambayo ni kero ndogo ndogo za kimuungano, lazima tuweze kuziondoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mnafahamu Wabunge wengi sasa hivi kuna vitu petty; mfano, anakuja pale bandarini, ana pasi yake, ana TV yake, anakamatwa, inazuiliwa. Hizi ndizo kero ndogo ndogo ambazo kati ya kero saba ndani yake ndiyo ziko hizo nyingine ndogo ndogo. Imani yetu ni kwamba, kama maelekezo ya Kamati ilivyotoa, tutaenda kuzishughulikia hizi. Kama tumefanya 11, sasa tunaenda kuhangaika na hizi kero saba zilizobakia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, imani yangu kubwa ni kwamba, trend tunayoondokanayo, tunaenda vizuri. Mpangokazi wetu ni kwamba, kama Kamati ilivyoelekeza, ndani ya mwaka huu 2022 tuna imani tutaenda kufanya mambo makubwa sana. Yale mambo ambayo yamekuwa ni kadhia siku zote, inawezekana mengi yao yataweza kuondoka. kubwa zaidi, katika mchango wa Kamati hii ni nini wanajadili kwa kina na hasa kero za Wabunge wanaotoka Zanzibar, hasa katika Mfuko wa Jimbo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unafahamu, leo hii nilikuwa na Mheshimiwa Sheikh Kassim na Mheshimiwa Zahor, wameniambia mambo mengi sana. Mambo haya mengine tunaenda kuyafanyia kazi kwanza. Kwa mfano, fedha za Mfuko wa Jimbo, mwaka jana 2021 tulifanya kazi kuhakikisha kwamba zile zilizotoka Desemba, baadaye sasa tukahangaika mwezi wa sita zikatoka. Mwaka huu tulihakikisha kwamba fedha za Mfuko wa Jimbo zote zinatoka katika muda unaofanana. Bahati nzuri kwa mara ya kwanza fedha zote zimetoka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nimepata taarifa kwamba, bado upelekaji wa fedha hizi kule kwa Wabunge katika Halmashauri kuna changamoto kidogo. Hili nikuhakikishie tutaenda kulifanyia kazi. Sisi tunachotaka ni kwamba, kila Mbunge ajisikie ana raha katika Bunge lake hili, afanye kazio vizuri. Maana yetu ni nini? Tunapoudumisha muungano wetu, tuhakikishe kwamba, yale mambo ambayo ni madogo madogo yamekuwa kadhia, tuweze kuyaondoa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni imani yangu kwamba, Kamati ilivyotoa maelekezo, sisi jukumu letu Wizara ya Muungano ni kuhakikisha kwamba yale mambo yote iliyotolea maelekezo tunaenda kuyafanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ufupi tu, naomba niwashukuru Wabunge wote, lakini na Wabunge kutoka upande wa Zanzibar kwa mara nyingine. Kwa kweli wamekuwa na mchango mkubwa sana kwa yale mambo mbalimbali kuweza kuyatatua. Ndiyo maana siku ile kaka yangu Mheshimiwa Ahmed Idrissa Abdul Wakil tulifanya kazi kubwa sana, na amenikaribisha kuzindua lile jengo. Nitakuja kaka yangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashukuru Wabunge wote kwa kweli. Niwaambie Wabunge kutoka Zanzibar, kwa sababu mimi kazi yangu ni huku Bara na Visiwani; nimepata taarifa kwamba, wakati mwingine hata tukitoa taarifa Wabunge wa Majimbo hawapati taarifa. Tutahakikisha kwamba ziara zetu zile tunazofanya kila ziara Mbunge anapata taarifa. Lengo kubwa ni ionekane kazi ya Mbunge, anafanya nini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Kwa haya machache, naunga mkono hoja za Kamati zote mbili zilizowasilishwa hapa. Ahsante sana. (Makofi)