Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017

Hon. Joseph Osmund Mbilinyi

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Mbeya Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Madiwani na Wabunge wa upande huu wanachangisha watu, isipokuwa wanachangisha kwa hiari siyo kwa kulazimisha na mgambo, naomba hii niliweke clear. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Spika, nikushukuru kwa ku-recognize mawazo yangu kuhusiana na hili suala kwa sababu kuna watu wanachukulia kama tumewa-pre-empty au vitu kama hivyo lakini no. Tunachojaribu kufanya ni kuboresha kwa sababu hata kama Wizara ya Afya wana sera kwa maana ya mipango, huwezi kuwa na mipango halafu fedha anazo mtu mwingine. Unaweza ukampigia simu kwamba bwana njoo na hizo fedha tutekeleze ile mipango katikati akakabwa na zisifike kwa wewe mwenye mipango. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo tuna confusion. Nafikiri labda kwa sababu sisi ndiyo Bunge labda ifike mahali sasa turudi tujadili upya kwamba hii system ya afya yote irudishwe kwenye mwamvuli mmoja kwa maana kwamba yote iwe chini ya Waziri wa Afya kwa sababu confusion ni kubwa sana. Ukiangalia hata kwenye ajira za madaktari, wengine wanaajiriwa na TAMISEMI, wengine wanaajiriwa na Wizara ya Afya, wengine wanajiona kwamba ndiyo madaktari wa kweli, wengine siyo madaktari wa kweli na hata linapokuja suala la kudai haki zao, wale walioajiriwa na Wizara ya Afya, Mheshimiwa Kigwangalla anajua, alikuwemo humo katika harakati za madaktari, wale walioajiriwa na Wizara ya Afya wakisema tusimame kidogo, tukaze uzi, Serikali isikilize madai yetu, wale wa TAMISEMI hawagomi. Kwa hiyo, tunaharibu hata umoja wa madaktari. Ili madaktari wawe pamoja inabidi wote wawe chini ya mwajiri mmoja, waongee lugha moja. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nikirudi Mbeya kuna suala la Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, mortuary. Nimepokea malalamiko kutoka kwa wafanyakazi wa mortuary Hospitali ya Mbeya kwamba wanafanya kazi kwenye mazingira magumu sana. Kuna friji 15 lakini kwa zaidi ya miaka miwili sasa friji tisa hazifanyi kazi, zinazofanya kazi ni sita tu kiasi kwamba kama ikitokea ajali na miili mingi ikapelekwa inabidi wana rotate (wanaweka mwili baada ya muda ukipoa wanatoa, wanabadilisha mwingine) that’s too bad for big hospital kama hospitali ya Rufaa ya Mbeya. Hata hivyo, pia hata wale wafanyakazi wanaofanya kazi mle katika mazingira magumu wana malalamiko sana kuhusiana na maslahi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, wananiambia wanatakiwa walipwe 150,000 kwenye postmoterm kwa maana ya daktari mtaalam anaitwa pathologist doctor. Daktari mtaalam anachukua shilingi 100,000 wale wanachukua shilingi 50,000, lakini hata hiyo hela kuipata imekuwa kazi na wale wa hospitali ya Rufaa Mbeya kwa zaidi ya miezi tisa sasa hawapewi ile hela kwa namna mbalimbali, wanaambiwa sijui wamefoji PF3 (zile ripoti za polisi), inafikia mahali wanaambiwa ili kuthibitisha; ndugu wa marehemu wawepo pale waangalie. Sasa wenzetu labda wanaweza, lakini katika utamaduni wetu kukaa pale kuona ndugu yako anapasuliwa moyo, nini kinatolewa sidhani kama ni sahihi. Kwa hiyo, tuangalie utaratibu wa kuthibitisha malipo yao kwa sababu kazi wanayofanya ni muhimu na ngumu.
Mheshimiwa Spika, lakini pia hawa wafanyakazi wa mortuary ifike mahali nao wapewe kozi, kama madaktari wanapewa kozi, manesi wanapewa kozi, na wafanyakazi. Isifike mahali unakwenda kuchukua mlevi tu kwa sababu hana sense, ndiyo umpeleke mortuary akafanye kazi kwa kutumia ile hali. Matokeo yake ndiyo unasikia mwili wa Kilimanjaro umepelekwa Mbeya na mwili wa Mbeya umepelekwa Songea, kunakuwa na mchanganyiko kwa sababu wale watu sio professionals wa ile kazi. Kwa kweli katika nchi za watu, mtu anayefanya kazi katika mazingira haya hata hela yake inakuwa ni nzuri sana kwa sababu tu watu wanatambua umuhimu wa zile kazi wanazofanya. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tukienda Hospitali ya Rufaa kuna hili jengo la maabara ya kisasa, linaitwa jengo la mionzi. Jengo hili nimelisemea toka naingia Bunge hili, hiki ni kipindi cha pili sasa. Toka nimeingia Bunge hili ikifikia Wizara ya Afya, nikisimama nalisemea hili jengo. Nikauliza, hivi jengo hili limejengwa na Mzee wangu Mheshimiwa Mwakyusa akiwa Wizara ya Afya, mnataka mpaka tena atokee Waziri kutoka Mbeya ndiyo lile jengo limaliziwe? Hata hivyo, namshukuru Katibu Mkuu sasa hivi anatoka Mbeya labda anaweza akaweka mkazo kidogo kwa sababu haya mambo yapo, hatuwezi kuyakataa, haya mambo yapo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sasa naomba sasa, naona imetengwa shilingi bilioni tano, ninachoomba ni guarantee ya Waziri, Naibu Waziri na Katibu huko aliko mkimpelekea majibu yatakapokuja, naomba guarantee ya hii shilingi bilioni tano, ni fedha za ndani au za nje zile zilizokataliwa kwa sababu ya uchaguzi wa Zanzibar kuchakachuliwa. Naomba nipate guarantee kujua kwamba hizi fedha zinakuja ili lile jengo limalizike.
Mheshimiwa Spika, naambiwa bilioni tatu ni kukamilisha jengo, shilingi bilioni mbili kwa ajili ya vifaa (CT Scan, MRI Scan), jengo lile likamilike ili sasa ile hospitali iongezeke hadhi na itapunguza hata influx ya wagonjwa kutoka eneo lile kuja Muhimbili na mtapunguza ile hekaheka ya kufunga ofisi, iwe wodi kwa sababu influx ya wagonjwa ni wengi, wengine wanaweza wakaishia huko huko ndugu zangu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuna suala la Bima ya Afya, Hospitali ya Rufaa Mbeya sasa hivi wanakusanya takriban shilingi 500,000,000 kwa mwezi kutoka shilingi milioni 70 sijui 80 huko nyuma. Shukurani kwa Mkurugenzi aliyepita na aliyepo sasa. Sasa nataka nijue katika hii shilingi milioni 500, ni ngapi inabaki kwa Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa ajili ya kuboresha maslahi mbalimbali ya wafanyakazi ikiwemo housing allowance za madaktari kama stahiki yao inavyotaka, ikiwemo on call allowance, daktari amekaa, amekuja kwa Mbunge labda mnaongea masuala mengine tu kama mwananchi wetu wa CHADEMA, lakini anapigiwa simu saa nne usiku kwamba unatakiwa hospitali kuna emergency, akienda kule hakuna malipo yoyote. Sasa nataka kujua hii shilingi milioni 500, ni ngapi inabaki hospitali ya Rufaa Mbeya na hata pia iende kwenye allowance kule mortuary ile ya Mbeya kwa wale wafanyakazi ambao wako frustrated kwa kweli.
Mheshimiwa Spika, mmoja akaniambia, siku moja Waziri alienda pale akamwambia Waziri kwamba hivi ndivyo tunavyolaza wagonjwa kwenye mochwari na bahati mbaya upate ajali, ukifa, ukiletwa hapa ntakulaza chini na wewe ili uone uchungu kama utakuwa na sense zozote.
Sasa kama mfanyakazi anafikia kusema hivyo, hizo ni kauli za mtu aliyekata tamaa na sio vizuri kuwa na wafanyakazi ambao Serikali imewaajiri, waliokata tamaa.
Mheshimiwa Spika, mwisho niseme Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu tulieni, you are vibrant young ones, sister you know energetic, naomba sana tulieni, mshaurini Rais namna ya kutekeleza sekta ya afya iwe bora. Msihofu, msiende kwa mizuka, maana tukisema mnaenda kwa mizuka wengine wanabisha, lakini hivi vitu vipo. Kwa hiyo msihofu, tulieni.
Mheshimiwa Spika, nilisikitika sana mimi binafsi kumwona Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya amebeba stuli, amebeba meza eti anahamisha wakati naamini kwamba huo muda anaofanya hivyo wangeweza kufanya vijana, wako vibarua pale Muhimbili, wangeweza kuhamisha stuli na droo wakati Waziri amekaa ofisini anapitia ripoti mbalimbali zikiwemo ripoti za mortuary ya Mbeya ambayo fridge tisa zimekufa, hazifanyi kazi. Angekuwa amekaa ofisini anafuatilia ripoti za nchi nzima badala ya kutumia muda huo muhimu wa mtu kama Katibu Mkuu msomi kubeba stuli.
Mheshimiwa Spika, ahsante.