Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

Hon. Ummy Hamisi Nderiananga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU (MHE. UMMY H. NDERIANANGA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Awali ya yote nipende kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uzima na afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipekee nimshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuniamini na kuniteua ili niwe Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu ninayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu. Namhakikishia Mheshimiwa Rais Samia kwamba sitamwangusha na kazi iendelee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nitumie fursa hii pia kuwashukuru sana Kamati yetu chini ya Mheshimiwa Mwenyekiti, Fatma Toufiq na Wajumbe, kwa kazi kubwa na nzuri wanayofanya ya kuishauri Serikali katika mapambano dhidi ya Virusi Vya UKIMWI na dawa za kulevya nchini. Niseme kwamba ushauri walioutoa sisi kama Serikali tumeupokea, tutaufanyia kazi na tutaleta maendeleo ya yale tuliyofanyia kazi katika Kamati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala la kuhamasisha wanaume kupima, naomba niseme kwamba Serikali imeendelea na mkakati wa kuwahamasisha wanaume kupima VVU na kujua afya zao. Tuna Mkakati unaitwa Male Engagement Strategy. Kipekee nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa, kwa kukubali kuwa balozi wa kuhamasisha wanaume kupima Virusi Vya UKIMWI. Kazi hiyo imeendelea vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kadri tulivyokuwa tunakwenda mbele tukaona tuboreshe programu hii na kuhakikisha kwamba tumeanzisha plan nyingine ambayo inaitwa Male Involvement Culture Plan ambayo itawajumuisha sasa watu wengi; wanawake, viongozi wa dini, watu ambao ni maarufu katika maeneo yetu kuhakikisha kwamba wanashirikiana na wanaume kuwahamasisha. Nitumie fursa hii kuwahamasisha wanaume mliopo humu Bungeni na ninyi kumuunga mkono Mheshimiwa Waziri Mkuu ili kupima afya zenu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika programu ya vijana Kamati imetushauri vizuri sana na tunawashukuru sana Kamati kwa kutambua na kuona kwamba eneo hili la vijana linatakiwa kupewa mkazo wa hali ya juu. Nipende kuwaambia vijana wote nchini Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali nzima tunawathamini na tunawapenda sana vijana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana hata mimi kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu nilizindua programu maalum ya vijana kwenye redio na tv inaitwa Ongea Programme ipo katika East Africa Radio na Clouds Media tunashirikiana nao pia na mtandao wa Instagram kuhakikisha tunatoa elimu kwa vijana wetu na tutaendelea kuhakikisha kwamba tunawafikia vijana wengi zaidi na zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niwatoe wasiwasi; kazi inaendelea vizuri, Ofisi ya Waziri Mkuu tumejipanga vizuri na maoni yote ya Waheshimiwa Wabunge tumeyachukua na tutayafanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nakushukuru sana. (Makofi)