Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

Hon. Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa ili niweze kuchangia. Nianze kwa kumshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa fedha za madarasa, tumejenga madarasa 73 ya sekondari kule Kilolo, tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitakuwa na mambo machache ya kuchangia kwa haraka kulingana na muda. Kwanza ni suala la Aids Trust Fund, Mfuko ulioko chini ta TACAIDS pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mifuko mingi tunayoianzisha hapa Bungeni huwa ina chanzo mahsusi cha mapato, lakini Mfuko huu ulianzishwa kwa kutegemea kwanza baeti ya Serikali, imetengwa shilingi bilioni moja na ndiyo inayotengwa kila mwaka, harambee pamoja na michango mbalimbali inayotokana na wahisani mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu ni kwamba, kama ilivyo katika Mifuko mingine, uwe Mfuko wa Maji, Barabara na Mifuko mingine mbalimbali, Mfuko huu pia utafutiwe chanzo mahsusi kutokana na tozo au da mbalimbali mahali fulani ambazo tayari zipo ili uweze kuwa stable zaidi. Kwa sababu tunazungumzia jambo ambalo bado mpaka sasa kuna watu 200 wanaambukizwa UKIMWI kila siku, ambayo ni 73,000 kwa mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii bado ni idadi kubwa, lakini hatuko sustainable. Zaidi ya 90% ya bajeti inatokana na misaada na kama ikitokea siku moja wafadhili tukatikisika kidogo tu, hatuna uwezo wa hata 5% wa kuweza kujifadhili. Kwa hiyo, huu mfuko lengo lake tungeujenga taratibu ili wafadhili watakapokuja kutikisika kidogo, basi angalau tuwe stable tuweze kununua angalau paracetamol kwa muda kadhaa wakati tunaendelea kujipanga.

MHE. ENG. STELLA I. MANYANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mtoa taarifa, Mheshimiwa Engineer Stella Manyanya.

T A A R I F A

MHE. ENG. STELLA I. MANYANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba pia nimpe taarifa Mheshimiwa anayechangia kwamba ni kweli kabisa naungana naye katika kuongeza fedha kwenye mfuko huu, kwa sababu katika eneo la kutoa elimu, tuko nyumba sana. Kwa mfano, sasa hivi kuna hatari kubwa inayoendelea kwamba hizo condom tunazosisitiza kwamba watu wawe wanazitumia, kwenye maeneo ya vijijini na siyo vijijini tu, hata mjini, lakini hasa suala hili nimeliona vijijini, unakuta watoto wanachukua hizo condom ndiyo wanageuza kuwa mipira na unakuta mtoto analia kabisa naomba condom yangu, condom yangu, kumbe ameiokota tu kwenye majalala huko. Kwa hiyo, bado inahitajika elimu ya kutosha na iwafikie wananchi wote. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Nyamoga, unapokea taarifa?

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeipokea taarifa hiyo. Sasa naomba kuchangia pia kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza, lakini mimi nitachangia kipengele kimoja kuhusu suala la wataalam wa mazoezi (physiotherapists). Wizara ya Afya inafahamu kwamba chuo kinachotoa taaluma hiyo kwa sasa ni kimoja tu cha KCMC; na hivi tunavyozungumza, tuna Physiotherapist 500 tu ambao wana practice nchi nzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa kawaida, magonjwa kama kisukari, pressure na hayo mengine yanahitaji mazoezi. Hizi Idara kwa sasa hivi, nyingi ziko kwenye ngazi ya Mkoa tu, lakini sasa siyo kama zamani. Zamani vijijini tulikuwa tunapelekewa tu dawa za matumbo, kikohozi na kadhalika; lakini kwa jinsi magonjwa yasiyo ya kuambukizwa yanavyoendelea, hali inahitaji Physiotherapist hadi kwenye Hospitali za Wilaya; na hizi Idara hazipo kwenye Hospitali za Wilaya na ni Idara muhimu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, napendekeza kwamba Wizara ya Afya iangalie kuongeza vyuo vinavyotoa taaluma ya Physiotherapist, yaani wale watu wa mazoezi. Pia katika ikama, wakati wa ujenzi wa hospitali za Wilaya na hata vituo vya afya, tuangalie uwezekanao wa kuweka hizo ili kuweza kuendana sasa na kasi ya maradhi yasiyo ya kuambukiza, yanayohitaji sana hii huduma ya Physiotherapist. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho ninalotaka kuzungumza ni kuhusu bajeti ya maendeleo kwa Tume ya Dawa za Kulevya. Kwasababu tuna chaguzi mbili; au tuwe na watu wengi sana humu ndani (hapa nchini) wanaotumia madawa ya kulevya, au tuzuie yasiingie kwa kiwango kikubwa. Kuzuia ni kwa kununua mitambo kwenye maeneo mbalimbali na mitambo hiyo inahitaji bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, napendekeza bajeti hii iangaliwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. Naunga mkono hoja. (Makofi)