Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge la kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara la Afrika

Hon. Eng. Ezra John Chiwelesa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Azimio la Bunge la kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara la Afrika

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa nichukue nafasi hii kukushukuru kwa kunipa nafasi ya kuwa mchangiaji katika Azimio la Uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara la Afrika. Pia naomba ku-declare interest, mimi ni Mbunge wa Kamati hii ya Viwanda, Biashara na Mazingira, kwa hiyo nitachangia maoni yangu binafsi nikijaribu kukazia kwenye yale ambayo yamewasilishwa na Kamati.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba vile vile nimpongeze Waziri na niipongeze Serikali kwa kuchukua hatua hii muhimu ya kuungana na nchi nyingine 41 za Afrika ambazo tayari zilisharidhia Azimio hili na tayari zenyewe zinaendelea. Hii ni decision ya kishujaa kwa sababu nchi hii ni kubwa, sasa wenzetu wanapokuwa wamefanya jambo la kuendelea, halafu sisi tukabaki nyuma, kwangu niliona ni kama kitu kilikuwa kinaturudisha nyuma kidogo. Kwa hiyo, niipongeze Serikali kwa hatua hii muhimu, lakini niseme yapo maeneo ambayo nimeyaona na nilipenda zaidi kuyaongelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani tumemaliza discussion ya mambo ya mahindi hapa, ni kitu ambacho nimejiandaa kuongea hasa masuala ya kilimo, maana tunayo fursa ya kufanya biashara hasa kwenye mazao ya kilimo, lakini nadhani yameongelewa mengi sana hapa, kwa hiyo nisingependa niingie sana huko. Hata hivyo, kwenye research zangu ambazo nilikuwa nimezifanya kwa siku mbili hizi wakati najiandaa, nilijaribu kuona eneo la tija, kwa sababu kilimo chetu tunapokwenda kuingia sasa katika ushindani mkubwa wa takribani nchi 42 au 41 za Afrika zile ambazo zimeshaingia, ni lazima tujaribu kuangalia sisi tumejipangaje hasa kwenye issue ya tija.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumekuwa tunalima sawa, tunafanya shughuli zetu sawa, lakini ile yield tunachokipata labda kutoka kwenye heka moja unachokipata comparing na wenzetu ambacho wanapata tumekuwa tuko nyuma sana. Sasa ukija ukaangalia cost of production, kwetu inapokuwa kubwa zaidi na tunaingia kwenye ushindani huu mkubwa, wenzetu watatulazimisha tushushe bei ya mazao ili waweze kuuza hapa au na sisi tutakapojaribu kwenda kuuza nje itakuja kuwa shida kidogo. Kwa hiyo, naomba tujikite zaidi kwenye suala hili kwa sababu nilikuwa naangalia average production katika tani moja ya mahindi, kwa mfano, kwa Tanzania, heka moja ya mahindi tumekuwa tunapata karibu gunia sita za kilo mia moja, mia moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ukija ukaangalia kwa wenzetu kwa mfano Zambia, kwa sababu tunaongelea ukanda huu wa kusini ndio unaolima mahindi sana, kwa Zambia ni double, tunaongea kwamba kwa hekta sio heka, kwa hekta moja kwa Tanzania ni 1.5 tons wakati kwa Zambia ni three tons kwa same hector. Ukija ukaangalia kwa South Africa inaenda karibu six. Sasa hawa ni wenzetu ambao ndio tunaoenda kushindana nao kwenye hili soko hasa uzalishaji wa mahindi. Sasa tukijaribu kuangalia competition yetu hasa kwenye bei itakuja kuwa ndogo zaidi, kwa sababu wenzetu watalima kidogo watavuna mengi. Wakishamaliza kuvuna mengi tunaingia kwenye soko moja la kushindana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo unakuja kukuta mbolea aliyoiweka kila kitu alichokiweka kwenye kuandaa shamba ni gharama zile zile sawa na wewe, lakini yeye amevuna magunia mengi zaidi, kwa hiyo atakuwa na uhuru zaidi wa kuuza kwa bei ya chini zaidi. Kwa hiyo hili jambo ningeomba tuliangalie ili tunavyokwenda kwenye ushindani kesho na kesho kutwa soko letu lisipotee, tuhakikishe kwamba hata na Wizara ya Kilimo inatusaidia tuweze kupata mazao mazuri zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kingine kikubwa liko suala la haya mazao ya GMO, hatuwezi kwenda mbali na dunia inapoelekea. Leo tunaingia kwenye ushindani, wenzetu wanalima pamba, tumekuwa tunasikia hapa Kanda ya Ziwa, watu wapo wanalima pamba, lakini pamba ambayo wenzetu leo wanalima ambapo wameshakwenda kwenye GMO technology ni tofauti. Yeye atalima heka moja, hapo unaongelea labda kwenye heka moja utavuna labda tani tano au tani 10, mwenzako labda yuko zaidi ya mara mbili kwa sababu wako kwenye GMO.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nilikuwa naomba kipindi tunaingia kwenye ushindani, kwa sababu nchi nyingine zimesha-advance kwenye teknologia hii, Serikali ijaribu kuangalia kwamba teknologia ya GMO bado tuna wasiwasi, tunajua labda ni genetic modified, tuna wasiwasi bado, lakini kwenye mazao ambayo siyo consumables kama vyakula, mazao yale ambayo tunaenda kushindana na wenzetu kama pamba na vitu vingine hivi vya kuuza kule, hebu tujaribu kuona kama tunaweza tuka-adapt hiyo teknolojia, tuanze kuruhusu baadhi ya vitu tukatumia teknolojia ya GMO. Kesi kubwa hapa ni kuwafanya Watanzania wanaofanya kilimo, kilimo chao kiwe cha tija, kiweze kuwaletea majawabu ambayo watawafanya wapate pesa kwenye rotation yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kwenye suala la masoko, tuna hakika kwamba sisi tuna mifugo hapa, tuna maziwa na uvuvi. Kwa hiyo, kwa sehemu kubwa mkataba huu utaenda kusaidia zaidi vijana wa Kitanzania na hasa Watanzania kuweza ku-embark sasa kwenda kuuza katika nchi za jirani na hatimaye tuweze kujipatia kipato kizuri zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ipo habari ya viwanda. Nadhani sasa hili ni soko ambalo tumekuwa tuna-trade labda sisi wenyewe na watu wa East Africa, hatuzidi watu milioni
200. Leo hii tunaingia kwenye soko la zaidi ya watu bilioni 1.2 iko fursa kubwa zaidi ya kuweza ku-trade na wenzetu, lakini ni lazima Serikali tuweke mguu chini; maana siku hizi vijana wanasema tuweke mguu chini. Maana ya kuweka mguu chini ni nini? Lazima ifikie hatua tujue tunaingia kwenye biashara. Kama tunaingia kwenye biashara, tufanye politics lakini huku tukijua kwamba tunaenda kwenye biashara.

Mheshimiwa Naibu Spika, biashara ni ushindani. The moment umefungua, watamwagika Wanaigeria hapa, watamwagika Wakenya hapa; sasa siyo kesho umefungulia, halafu keshokutwa unaanza kulalamika. Tutakuwa na miaka mitano ya kufanya changes, lakini hamtawafukuza kwa sababu watakuwa wamesha-invest.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunachoomba, kesi kubwa ambayo tumekuwa tunaipata upande wa Serikali, ni lazima tuhakikishe tunawa-fever hawa watu wanaofanyabiashara hapa. Tusione mfanyabiashara kama adui. Hiki ndicho kitu ambacho naomba zaidi upande wa Serikali ituangalie. Kodi na tozo zimekuwa nyingi mno kwenye biashara. Hatutaweza kushindana na wenzetu kama kodi na tozo zinaenda kuwa nyingi kiasi hicho. Kwa hiyo, hivi ni vitu ambavyo lazima tujaribu kuangalia. Tunapoingia kwenye uhuru wa soko hili la Afrika, kwa sababu ni market tunayoifungua, una wateja wengi, ukubali kushusha bei, kuondoa baadhi ya tozo, kuzalisha kwa wingi zaidi, kuuza kwa wingi zaidi, ndiyo tutakapopata faida, kuliko kuzalisha kidogo, ukataka kuuza kwa bei kubwa kwa sababu mna tozo nyingi zaidi, hatimaye ukajikuta kwamba umekwama na wenzenu ndiyo wakaanza kuingiza hapo, kwa sababu wao watakuwa wako free.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nilichokuwa naomba kwa upande wa Serikali, tuliangalie sana hili. Wafanyabiashara tusiwaone kama maadui, tuwaone kama partners. Ni lazima kwa upande wetu, hasa Serikali yetu ya Tanzania, Wizara ya Viwanda na Biashara muwe tayari kuwa-support wafanyabiashara wa Kitanzania, pale watakapotaka kwenda nje, watakapotaka kubaki hapa, waone kwamba Serikali iko nyuma yao. Kwa sababu tunavyoingia kwenye hili soko, wenzetu lazima Serikali zao zitakuwa zinawa-support.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninao mfano hapa nilikuwa najaribu kupitia, kuna tangazo la NEMC walilitoa tarehe 7, this one here, nimelitoa kwenye Citizen leo, linasema, “NEMC hits Lake Oil with 3.3 billion Fine” ya vituo 66 vya mafuta. Sasa Waziri wa Viwanda na Biashara uko hapa, Lake Oil wana vituo 66 nchi hii. Leo NEMC anawatangazia kwamba anawapiga faini ya shilingi bilioni 3.3; huyu ni mfanyabiashara ambaye yuko hapa ame-invest kwenye vituo vyote hivyo, anampiga faini ya shilingi bilioni 3.3, over sudden tu anamwambia ndani ya siku 14 alipe. Kesi ni nini? Ni kwamba amefanya vituo vyake hivyo bila kufanya Environmental Impact Assessment. Unajiuliza, mpaka mtu anafungua vituo 66, Serikali ilikuwa wapi? NEMC walikuwa wapi? Au kuna kitu gani ambacho walielewana na NEMC, sasa leo kimeshindikana hapo katikati, wanawageuzia kibao? This is the very big shame! (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo ukiongelea vituo 66, Serikali itapoteza fedha kiasi gani? Yule mtu akisema leo hana, ikaamuliwa vifungwe, Serikali itapoteza pesa kiasi gani? Ajira ngapi za Watanzania zitapotea na vilevile ni scandal. Kwa hiyo, nilikuwa naomba, vitu kama hivi, kama kunakuwa na cases kama hizi; sasa leo unavyotuambia Lake Oil hawana hiyo Environmental Impact Assessment mnawafungia, vituo vingine waliokuwa wanalipa ambao wamefuata taratibu kihalali, wenyewe mliwafunguliaje? Yaani huyu mtu mpaka anajenga vituo 66 alikuwa anajificha wapi mpaka vikamilike 66 ugundue leo? Hivi ni vitu vidogo tu ambavyo baadaye vinam-discourage mtu.

MHE. NICHOLAUS G. NGASSA: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ezra Chiwelesa kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Ngassa.

T A A R I F A

MHE. NICHOLAUS G. NGASSA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumpa taarifa mzungumzaji; ili uweze kipata kibali cha kujenga Kituo cha Mafuta, lazima uwe na certificate kutoka NEMC, ipelekwe Ewura, Ewura ndiyo wakupe kibali. Ili upate kibali cha NEMC, ni lazima uwe umesajili kile Kituo cha Mafuta uweze kufanya hiyo Environment Impact Assessment. Maana yake, anachokiongea Mheshimiwa pale, kutakuwa kuna shida kule ambayo ndiyo imeleta hili tatizo kubwa. Kwa hiyo, hata Serikali waweze kuliangalia. Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ezra Chiwelesa, unapokea taarifa hiyo?

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Naibu Spika, naipokea. Hili ni jambo moja tu ambalo nimesema kwamba ni discouragement upande wa biashara. Ndiyo maana nikasema, Wizara ya Viwanda na Biashara na hasa upande wa Serikali, tuangalie; tunapoingia kwenye ushindani mkubwa namna hii tunakuja kuleta giants hapa, tutaleta giants kwa sababu sisi advantage tuliyonayo hapa, lazima wenzetu watakuja ku-invest tu hapa kwa sababu tuna ardhi nzuri, tuna vitu vingi, tuko kwenye ukanda huu wa bahari, lazima tutapata watu wa kuja ku-invest hapa. Ila kipindi wale investors tunajaribu kuwavuta, ni lazima tujaribu kuangalia kwamba vitu vidogo na vya kukwaza kama hivi visiweze kutuharibia.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuunga mkono azimio. Ahsante sana. (Makofi)